Elections 2010 Kumbe hata January anajua babake mropokaji!?

Ramos

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2010
Posts
498
Reaction score
130
Akihojiwa na Clouds FM leo, January aliulizwa kama alimshirikisha baba yake katika azma yake ya kwenda kuomba uteuzi...

Wakati anajibu aliweka sentensi kuwa 'nilimwambia kuwa ...baba naenda kugombea, naomba usiniharibie... maana najua yele Mzee anaweza kwenda kule akazungumza neno, ikawa tena bas, ameshaharibu'..
 
Duh nami nilimsikia kijana nikashangaaa kumbee anaweza kuanikaa vilee udhaifuu wa mzee wake...January anaaonekana kujiamni sana labda kwa fursa aliyopata ya kuwa karibu NA Mh Raisi na kutumia vema kodi zetu katika mizungukoooooo....
 
Mtoto wa nyoka anaweza kuwa chura? Mwembe unazaa maembe na si mapera!
 
Shauri yake hajui Otober 14 bado haijafika..Mzee atakula kichwa..vitu vingine unamezea haswa inapokuja family issue..
 
Naye kumbe mropokaji kama baba yake, kwa nini kaanika udhaifu wa baba yake!
 
Tatizo watu wanapenda na kufurahia sana kudanganywa. Januari kawa mkweli kwa kuanika tabia ya baba yake ya kuropoka ,lakini ajabu sasa yeye naye anaonekana kuwa ni mropokaji!!!!!????. Mimi naona huyu ni jasiri na mkweli kwa kuanika ukweli juu ya tabia ya baba yake. Hongera Januari kwa kuuthibitishia umma kwamba baba yako ni mropokaji.
 
Wasiomjua January watamshangaa ila mimi simshangai, possibly hapo alipokuwa anaongea clouds hajapata supu na kuzimua na gambe moja ndio maana akili ilikuwa haijakaa supa.Anyway hao ndio wabunge wetu wa nchi hii, ngojani muone dogo atakavyo kuwa anafuka moshi.
 
kila mtu ana udhaifu wake,Watanzania tumezoea kunyooshea wenzetu vidole ingali vingine vinaturudia,ama kweli NYANI HAONI KUNDULE!!!
 
Dogo anaonekaanaa ni mropokajii zaidi ya mzee wake na hapo hajapata madaraka ya umma makubwa..

ni kijana na ameonyeshaa ukosefu wa nidhamu kwa mzazi wake je kwa watanzaniaa itakuwajee????
 
Jamani JF sometime tunasahau vitu muhimu, this young spoiled brat wass the architecture behind "mbayuwayu speech" na "mimba za watoto wa shule ni viherehere vyao" so what can we expect from him, subiri bumburi wabumburike :mad2:
 
UROPOKAJI ni tabia binafsi ya mtu na haiwezi kumpima mtu ufanisi wake wa kiutendaji...kama atahukumiwa kwa kusema alilosema fine but hilo pia ni la kifamilia zaidi sidhani kama chama au wanajamii wanaweza kumhukumu moja kwa moja kwa kumnyima fursa ya kuongoza....anapomwomba baba asimharibie inaweza kutafsiriwa kuwa kwa madaraka ya baba chamani basi anaeza kusema kijana bado hajakomaa au baba akatumia nafasi yake kusema "kijana wangu anagombea" na hiyo ikamharibia katika harakati ukaonekana ni mpango wa baba kurithisha mwana ufalme...mi niliielewa tofauti kabisa na nadhani kuna wengine pia wameelewa hivyo kama hawajahusisha itikadi za kisiasa katika kauli hiyo
 
Akihojiwa na Clouds FM leo, January aliulizwa kama alimshirikisha baba yake katika azma yake ya kwenda kuomba uteuzi...

Wakati anajibu aliweka sentensi kuwa 'nilimwambia kuwa ...baba naenda kugombea, naomba usiniharibie... maana najua yele Mzee anaweza kwenda kule akazungumza neno, ikawa tena bas, ameshaharibu'..

Hii kauli mimi naichukulia katika mtazamo tofauti kidogo.
Nadhani ameongea hivyo ili kudhihirisha kuwa hajabebwa na baba yake.
na katika uteuzi wake watu waelewe kuwa hakuna mkono wa baba yake.
Na ndio maana anataka jamii iamini kuwa tangu alivyomwambia baba yake kuwa anaenda kugombea, baba yake alikuwa kimya tu, hakushughulika naye. alimwacha ahangaike yeye mwenyewe.
Ni kauli ya Kisiasa zaidi, Haimaanishi.
 
Like Father : Like son - Hapo na yeye (Januari) ameropoka!
 
Hii kauli mimi naichukulia katika mtazamo tofauti kidogo.
Nadhani ameongea hivyo ili kudhihirisha kuwa hajabebwa na baba yake.
na katika uteuzi wake watu waelewe kuwa hakuna mkono wa baba yake.
Na ndio maana anataka jamii iamini kuwa tangu alivyomwambia baba yake kuwa anaenda kugombea, baba yake alikuwa kimya tu, hakushughulika naye. alimwacha ahangaike yeye mwenyewe.
Ni kauli ya Kisiasa zaidi, Haimaanishi.

Inawezekana ndio alimaanisha hivyo. Lakini kama alichukua jukumu la kumfundisha baba yake anachotakiwa kutofanya, si ina maana alihofu kuwa baba anaweza kufanya yasiyotakiwa?
 
UROPOKAJI ni tabia binafsi ya mtu na haiwezi kumpima mtu ufanisi wake wa kiutendaji...kama atahukumiwa kwa kusema alilosema fine but hilo pia ni la kifamilia zaidi sidhani kama chama au wanajamii wanaweza kumhukumu moja kwa moja kwa kumnyima fursa ya kuongoza....anapomwomba baba asimharibie inaweza kutafsiriwa kuwa kwa madaraka ya baba chamani basi anaeza kusema kijana bado hajakomaa au baba akatumia nafasi yake kusema "kijana wangu anagombea" na hiyo ikamharibia katika harakati ukaonekana ni mpango wa baba kurithisha mwana ufalme...mi niliielewa tofauti kabisa na nadhani kuna wengine pia wameelewa hivyo kama hawajahusisha itikadi za kisiasa katika kauli hiyo

Kama angekuwa baba mwenye busara unadhani angeweza kusema hivyo. Au kama January angemchukulia mzee kama mtu mwenye busara unadhani angeamua kumfundisha ya kufanya?
 
Back
Top Bottom