Sishangai kusikia karibia asilimia tisini ya wabongo ni washirikina, sio kwenye SOKA...SIASA..BONGO MUVI....BONGO FLEVA yaani mambo ni vululu vululu, Vita ya mauaji ya albino inakuwa ngumu kwa sababu za ujinga huu. Inafikia wakati mwanainchi wa kawaida mtaani anaulizwa na mtangazaji na anaongea bila kuficha wala kuona aibu. utamsikia mwanamama anasema..."Hela yangu ilipotea ndani nikaenda kwa mganga akaniambia ni wifi ndio amechukua"....jamani taifa linaangamia..watu wajiamini kwa vipaji vyao..na kama uganga ungekuwa na msaada Tungekuwa na soka la juu kuliko hata Hispania....maana huko kwenye soka nako ni balaa... MAFANIKIO NI JUHUDI na KUMUOMBA MUNGU...