JPM alikuwa msanii sana. Mikataba mibovu ilianza wakati wa JK akiwa waziri wa nishati na madini na yeye alikuwa analijua hilo. Sasa miaka yote hiyo 5 kwa nini hakumuajibisha?
Issue ya gesi Mtwara ilipitishwa na Bunge kwa hati ya dharura huku Chadema wakitolewa nje ya kikao hicho. JPM hilo alilifahamu na kwa miaka 5 hakuchukua hatua yoyote wala hakutaka kabisa kubadilisha mikataba yote mibovu iliyosainiwa na watangulizi wake akawa anapambana na watu aliohisi ni matajiri na wasio na mtetezi .
Ukiona kiongozi anahusudu sana kupendwa (populist) lazima mtaishia kubaya.