Magufuli kama aliamua kupambana na hao jamaa angepambana nao mwanzo mwisho, kuliko kuwa na nia, uwezo, na sababu lakini akaacha kwa lengo la kuwalinda wastaafu.
Hata kama sheria inawalinda, lakini jamaa wangeweza kwenda mahakamani kama mashahidi, coz sio wao walioshtakiwa, kitendo cha JPM kuwaacha ndio aliharibu, leo wako mitandaoni wanamsema kila siku.
Wangepandishwa kizimbani watoe ushahidi, Karamagi kwenye utetezi wake angewataja, wenye akili timamu wangejua nani alikuwa muhusika mkuu hata kama sheria inamlinda.