Kumbe huu ndo mtazamo wa Wazungu kuhusu watawala nchi za kiafrika?

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
2,887
Reaction score
5,687
Nilikaa sehemu hivi hapa Morogoro sehemu inaitwa Amadia nikisubiri passport size pictures nilizokua nimepiga moja ya studio maeneo haya.

Pembeni alikua amekaa Mzungu mzee wa makamo 70 years + kumkadiria.
Nikamsalimia na yakaanza maongezi ya hapa na pale.
Kuna mambo kadhaa aliongea yalinifikirisha sana;

1. Alisema watu Smart wenye uwezo wa kuongoza na kuzipaisha inchi kimaendeleo huwa hawapewi nafasi hivyo inchi za kiafrika na zingine za Dunia ya tatu zinaongozwa na watu wenye uwezo mdogo ambao Wana easy access kwenye leadership circle kwasababu ya rushwa , kupendeleana nk hivyo inchi husika kuendelea ku lag behind kwenye Kila nyanja ya maendeleo.

2. Kuhusu tatizo la umeme alisema , amezunguka tz nzima . Vyanzo vinavyoweza kumaliza tatizo la umeme ni a) sea waves b) wind turbines c) geothermal d) hydroelectric E) kataja makaa ya mawe, f. Solar na nyingine nimesahau, na akaorodhesha faida na Short fall ya Kila mojawapo

3. Baadaye akabadili story akanipa assignment 2.
A) nikasome astronomical potential of tuareg tribe
B) underground tunnels inchini marekani.

Ukiacha yote ile kusema watu wenye uwezo wa uongozi hawapewi nafasi kupelekea African counties kuongozwa na watu wenye uwezo mdogo ilinifikirisha sana
 
Hapo kwenye viongozi naweza kukubaliana naye
 
Sema viongozi wa wazungu wanafahamu kuwa Africa's raw materials are cheap tofauti na sehemu nyingine duniani kutokana na technological backwardness, hivyo uchumi wa Ulaya unategemeana sana na Africa ndo maana Ufaransa bado anaikomalia Niger.

Hata GDP data za nchi za Afrika hizi zinazotoka kila baada ya quarter fulani huwa haziongelei uhalisia wa ubovu wa uchumi wa Africa.
 
Nilikaa sehemu hivi hapa Morogoro sehemu inaitwa Amadia nikisubiri passport size pictures nilizokua nimepiga moja ya studio maeneo haya.

Pembeni alikua amekaa Mzungu mzee wa makamo 70 years + kumkadiria.
Nikamsalimia na yakaanza maongezi ya hapa na pale.
Kuna mambo kadhaa aliongea yalinifikirisha sana;

1. Alisema watu Smart wenye uwezo wa kuongoza na kuzipaisha inchi kimaendeleo huwa hawapewi nafasi hivyo inchi za kiafrika na zingine za Dunia ya tatu zinaongozwa na watu wenye uwezo mdogo ambao Wana easy access kwenye leadership circle kwasababu ya rushwa , kupendeleana nk hivyo inchi husika kuendelea ku lag behind kwenye Kila nyanja ya maendeleo.

2. Kuhusu tatizo la umeme alisema , amezunguka tz nzima . Vyanzo vinavyoweza kumaliza tatizo la umeme ni a) sea waves b) wind turbines c) geothermal d) hydroelectric E) kataja makaa ya mawe, f. Solar na nyingine nimesahau, na akaorodhesha faida na Short fall ya Kila mojawapo

3. Baadaye akabadili story akanipa assignment 2.
A) nikasome astronomical potential of tuareg tribe
B) underground tunnels inchini marekani.

Ukiacha yote ile kusema watu wenye uwezo wa uongozi hawapewi nafasi kupelekea African counties kuongozwa na watu wenye uwezo mdogo ilinifikirisha sana
Nafikiri huyo Mzungu wako anazungumzia wastani wa viongozi waliojitokezakulingana na takwimu; lakini hutokea mmoja au wawili wakawa na akili nzuri tu kama akina Mandela, Nyerere walivyotokea. Kwa ujumla mtu mwenye akili nzuri hagombei uongozi na hili siyo tatizo la Bara la Afrika tu hata kwingineko iko hivyo hivyo. Kuongoza nchi ni tofauti na kungoza kampuni. Uongozi wa nchi unahusu siasa. Siasa nyingi ni chafu, uongo mwingi na unaowangoza wako matabaka mengi mno yenye utashi tofauti na uwezo tofauti wa kujua kinachotakiwa kufanywa na serikali na kipi ni wajibu wao wananchi. Binafsi sipendi uongozi wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom