Kumbe kufanya mazoezi ni raha hivi

Kumbe kufanya mazoezi ni raha hivi

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Helloo JF!!

Hili sikulijua kabla au nililichukulia poa. Ni week ya tatu tangu nianze ratiba ya ufanyaji mazoezi kila siku tatu za juma saa 11 alfajiri. Hii ni baada ya siku moja kulazimika kukimbia kidogo umbali wa kama mita 180 hivi kuuwahi usafiri.

Nikajikuta natweta mno kama moyo uchomoke. Hapo ndio akili ikashtuka nikagundua mwili nimeuachia mno ingawa si mnene lkn pumzi sina kabisa.

Ikanifanya niweke palepale alarm kwenye simu yangu siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa saa 11 kufanya jogging kidogo kwa dkk 30. Nilichagua hizi siku sababu haziangukii weekend so, ni rahisi kutoharibu hii ratiba.

Siku ya kwanza na ya pili nikakimbia round kumi kuzunguka uwanja. Siku zilizofata nakimbia round kumi za kawaida(speed ya kawaida) na round tano za kasi kidogo.

Kwa sasa kiukweli naona tofauti yaani nikimaliza najisikia poa sana ni kama mwili umerelax vyema. Hata kwenye shughuli zangu naona tofauti ilikuwa nikifika nakuwa na uchovu mno asubuhi mwili unakawia mno kuchangamka. Kwa sasa hata usingizi nalala mzuri.

Nimeamua hii kwa sasa iwe moja ya ratiba ya maisha yangu.
 
Hongera
Wale wa nitafanya kesho tujuane😂😂
weka nia, ukizoea utajikuta umekuwa mlevi wa kupiga tizi. fanya mazoezi simple tu kukimbia, kuruka kamba etc. si lazma uende kwenye yale majumba yenye trainer na AC.

Tena ukiwa na bae yananoga zaidi. weka tu ratiba isiyokubana hata mara mbili kwa week.
 
weka nia, ukizoea utajikuta umekuwa mlevi wa kupiga tizi. fanya mazoezi simple tu kukimbia, kuruka kamba etc. si lazma uende kwenye yale majumba yenye trainer na AC.
Tena ukiwa na bae yananoga zaidi. weka tu ratiba isiyokubana hata mara mbili kwa week.
Ahsante sana ..nitajitahidi nianze
😂😂Mazoezi na babe!!!...🤣🤣 Sawa .
 
Mwanaume akiwa na kitambi ka dushelele kanakuwa kadogo kama njiti.

Basi ukishakuwa hivyo kuna option mbili tu

1:kukiondoa haraka sana
2: kuwa na pesa ya maana ili uongezewe hii sifa

" ana kibamia ila anajua kukitumia"

Mazoezi ni afya pesa ni maisha
 
Back
Top Bottom