Kumbe kuna scenario ambapo ukijificha Mungu hakuoni!!

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
2,650
Reaction score
4,065
Ukisoma katika biblia takatifu hasa kitabu cha mwanzo baada ya adamu kula tunda lile walilokatazwa kula Mungu aliwayafuta bustanini asiwaone.

Kumbe kuna wakati mungu Ukijificha hakuoni. Basi nikitaka kuzini nitakuwa najificha ili asinione
 
Hapana siyo kwamba hakuoni ila yeye hutaka ile sababu ya kwanini wewe ujifiche wakati kila siku akikuita huwa unakuwa kweupe kwahiyo Mungu yeye atakuuliza uko wapi ili wewe mwenyewe ujiseme nipo huku , atakuuliza tena japo anajua sababu ya wewe kujificha ila atataka wewe uongee mwenyewe kwa ulimi wako hapo sasa ndo inakuja ile confession Baada yapo yeye sasa ndo ataamua akusamehe au akupe adhabu
 
Walijipaka majani fulani ili wasionekane. Ni lile jani nyoka analotumia kumtibu mwenzake.
 
SIO KWELI...
(soma hii itakusaidia kuelewa)
 
Ukisoma katika biblia takatifu hasa kitabu cha mwanzo baada ya adamu kula tunda lile walilokatazwa kula Mungu aliwayafuta bustanini asiwaone.

Kumbe kuna wakati mungu Ukijificha hakuoni. Basi nikitaka kuzini nitakuwa najificha ili asinione
Kumbe ulikuwa hujui hata hilo! Kaa gizani haoni 😂🤓🤠
 
SIO KWELI...
(soma hii itakusaidia kuelewa)
KWA LUGHA RAHISI ADAMU NA MUNGU walikuwa na ushurika wa Kiroho ,NAFASI ya kiroho aliyokuwa nayo Adamu ilikuwa ni ya UKARIBU /JIRANI na MUNGU.
BIBLIA INASEMA ..."dhambi inakutenga na Mungu=dhambi ni mauti""* dhambi ni roho ya chafu inayo ondoa ushirika na Mungu na inakuunganisha na ushirika na shetani.

Baada ya tu ya ADAMU kutenda dhambi KIROHO akawa ,amefungilia mlango wa kutawaliwa kuwa chini ya utawala wa shetani(yaani kaondoa ushirika na Mungu kaunga ushirika na shetani).

MUNGU anapomuuliza ADAMU UKO WAPI??? kwa nini siku zote kabla ya Afamu kutenda dhambi ...Mungu hajawahi kumuuliza UKO WAPI??

Kwa nini baada ya kula tunda ADAMU anajiona kuwa yuko UCHI??..dhambi ni inakuweka uchi..kuwa uchi kiroho mana yake ni nini?
Kwa nini baada tu ya kutenda dhambi anatafuta kujificha???

MUNGU ANAPOULIZA KITU SIO KWAMBA HAJUI JIBU AU HAJAONA..
Mfano ..Mungu anamuuliza KAINI yuko wapi ndugu yako??(ABELI)??

ANATAKA KAINI AJIBU??(anajua Kaini kamuua ABELI na damu ya ABELI inamlilia ,Mungu anasikia mpaka sauti ya damu ,damu ya Abeli aliyedhulumiwa uhai inaongea ina mlilia...LAKINI pamoja na kuyajua nankuyaona na kusikia sauti ..BADO akamuuliza KAINI ,YUKO WAPI ABELI NDUGU YAKO??(..huku anajua kuwa KAINI kamuua ndugu yake ABELI??
 
Na ndio maana wakristo tuna madhehebu zaidi ya 3000. Yaani andiko hata liwe wazi kiasi gani ila kila mtu atajidai kuja na tafsiri yake na kila mmoja anajiona yeye ndio anajua zaidi kwamba Mungu alimaanisha nini..!

Nafikiri wewe umeandika mawazo yako ILA
kwa mujibu wa biblia, Mungu hakuwaona; ikabidi aite Adam, Adam, uko wapi?
 
KWA LUGHA RAHISI ADAMU NA MUNGU walikuwa na ushurika wa Kiroho ,NAFASI ya kiroho aliyokuwa nayo Adamu ilikuwa ni ya UKARIBU /JIRANI na MUNGU.
BIBLIA INASEMA ..."dhambi inakutenga na Mungu=dhambi ni mauti""* dhambi ni roho ya chafu inayo ondoa ushirika na Mungu na inakuunganisha na ushirika na shetani.

Baada ya tu ya ADAMU kutenda dhambi KIROHO akawa ,amefungilia mlango wa kutawaliwa kuwa chini ya utawala wa shetani(yaani kaondoa ushirika na Mungu kaunga ushirika na shetani).

MUNGU anapomuuliza ADAMU UKO WAPI??? kwa nini siku zote kabla ya Afamu kutenda dhambi ...Mungu hajawahi kumuuliza UKO WAPI??

Kwa nini baada ya kula tunda ADAMU anajiona kuwa yuko UCHI??..dhambi ni inakuweka uchi..kuwa uchi kiroho mana yake ni nini?
Kwa nini baada tu ya kutenda dhambi anatafuta kujificha???

MUNGU ANAPOULIZA KITU SIO KWAMBA HAJUI JIBU AU HAJAONA..
Mfano ..Mungu anamuuliza KAINI yuko wapi ndugu yako??(ABELI)??

ANATAKA KAINI AJIBU??(anajua Kaini kamuua ABELI na damu ya ABELI inamlilia ,Mungu anasikia mpaka sauti ya damu ,damu ya Abeli aliyedhulumiwa uhai inaongea ina mlilia...LAKINI pamoja na kuyajua nankuyaona na kusikia sauti ..BADO akamuuliza KAINI ,YUKO WAPI ABELI NDUGU YAKO??(..huku anajua kuwa KAINI kamuua ndugu yake ABELI??
Kwa hiyo Mungu ana maswali ya ki mitego
 
Kwa hiyo Mungu ana maswali ya ki mitego

HAPANA ILA SHETANI ndiye mwenye kuuliza maswali ya kimtego,
yeye ndiye anauliza akiwa anajua jibu KWA LENGO LA KUKUTEGA...
mfano shetani akiwa katika umbo la nyoka. ndani ya bustani ya EDENI.
alimuuliza swali EVA

Swali: ETI??hivi ndivyo alivyosema MUNGU kuwa msile matunda yote ya humu bustanini...????

ETI???(Anawatega..)

Na matokeo ya mtego wake alifanikiwa KUWADANGANYA na ndio LENGO la kuwatega ILI AWADANGANYE (mana shetani ni baba wa uongo..bingwa wa UONGO)

Kinyume kabisa na matendo ya MUNGU.

N:B Kulitaja bure jina la Mungu kwa lengo la kufanya midhaha,au kukejeli ni kukufuru na ni dhambi.Tulitaje jina la Mungu endapo kuna umuhimu/ulazima na kwa mambo ya maana(ILI TUSIJE HESABIWA DHAMBI)

Midhahaha na kejeli kwa Mungu ni dhambi.
 
Ukisoma katika biblia takatifu hasa kitabu cha mwanzo baada ya adamu kula tunda lile walilokatazwa kula Mungu aliwayafuta bustanini asiwaone.

Kumbe kuna wakati mungu Ukijificha hakuoni. Basi nikitaka kuzini nitakuwa najificha ili asinione
Utoto raha sana, unaingiza kiçhwa kwenye maji, mknd uko nje unajua huonekani.
 
Ukisoma katika biblia takatifu hasa kitabu cha mwanzo baada ya adamu kula tunda lile walilokatazwa kula Mungu aliwayafuta bustanini asiwaone.

Kumbe kuna wakati mungu Ukijificha hakuoni. Basi nikitaka kuzini nitakuwa najificha ili asinione
Ukifanya dhambi unakosa kuonekana kwenye utukufu na ile favor ya kimungu na ndio maana ya kutoonekana na Mungu. Na usiombe hilo litokee kwa yeyote ni balaa kubwa!
 
Maana yake haupo SEHEMU aliyokuweka kiroho,maana yake HAUPO KATIKA NAFASI yaki KIROHO..Mana yake umekufa(dhambi ni mauti)kimwili upo hai kiroho umekufa.
Mana yake UPO GIZANI ufalme wa giza umetoka NURUNI umeingia gizani.
Maana yake umepotea UMEPOTEA upo njia isiyo sahihi. tena upo uchi,UMETOKA KWENYE MSTARI NAFASI YAKO....?
 
Ukisoma katika biblia takatifu hasa kitabu cha mwanzo baada ya adamu kula tunda lile walilokatazwa kula Mungu aliwayafuta bustanini asiwaone.

Kumbe kuna wakati mungu Ukijificha hakuoni. Basi nikitaka kuzini nitakuwa najificha ili asinione
Aliwatega ajue kama watamdanganya
 
mi nafikiri Mungu ni wa HAKI (mwenye haki)
(HAKIMU WA HAKI)
Aliwapatia nafasi ya KUJITETEA kwanza,.
aliwapatia nafasi ya kuwasikiliza kusikiliza utetezi wao
KABLA YA KUACHILIA AU KUTOA HUKUMU YA HAKI.

MUGU hawezi kumtega mtu.

Anayeweka mitego ili kutunasa tuangukie dhambini ni SHETANI.
 
KWA LUGHA RAHISI ADAMU NA MUNGU walikuwa na ushurika wa Kiroho ,NAFASI ya kiroho aliyokuwa nayo Adamu ilikuwa ni ya UKARIBU /JIRANI na MUNGU.
BIBLIA INASEMA ..."dhambi inakutenga na Mungu=dhambi ni mauti""* dhambi ni roho ya chafu inayo ondoa ushirika na Mungu na inakuunganisha na ushirika na shetani.

Baada ya tu ya ADAMU kutenda dhambi KIROHO akawa ,amefungilia mlango wa kutawaliwa kuwa chini ya utawala wa shetani(yaani kaondoa ushirika na Mungu kaunga ushirika na shetani).

MUNGU anapomuuliza ADAMU UKO WAPI??? kwa nini siku zote kabla ya Afamu kutenda dhambi ...Mungu hajawahi kumuuliza UKO WAPI??

Kwa nini baada ya kula tunda ADAMU anajiona kuwa yuko UCHI??..dhambi ni inakuweka uchi..kuwa uchi kiroho mana yake ni nini?
Kwa nini baada tu ya kutenda dhambi anatafuta kujificha???

MUNGU ANAPOULIZA KITU SIO KWAMBA HAJUI JIBU AU HAJAONA..
Mfano ..Mungu anamuuliza KAINI yuko wapi ndugu yako??(ABELI)??

ANATAKA KAINI AJIBU??(anajua Kaini kamuua ABELI na damu ya ABELI inamlilia ,Mungu anasikia mpaka sauti ya damu ,damu ya Abeli aliyedhulumiwa uhai inaongea ina mlilia...LAKINI pamoja na kuyajua nankuyaona na kusikia sauti ..BADO akamuuliza KAINI ,YUKO WAPI ABELI NDUGU YAKO??(..huku anajua kuwa KAINI kamuua ndugu yake ABELI??
Kwenye hivyo vinavyoitwa vitabu vitakatifu kuna mambo ya kustaajabisha sana. Nyoka anaongea na mwanamke kumshawishi ale tunda, Mungu anajawa na hasira kali na bila huruma anawafukuza watu aliowaumba kwa hiari yake kutoka bustanini, mwanamke anaadhibiwa kwa kuzaa kwa uchungu na mwanamme kutoka jasho ili ahudumie familia yake. Kisa ni kula tunda tu. Wangeukata mti sijui ingekuwaje.

Sehemu nyingine mungu anashawishiwa na shetani na anamruhusu amtende Ayubu kwa kuangamiza mifugo na watoto wake na kumpiga kwa gonjwa baya la majipu eti ili kupima imani ya mtu wake kwake.

Kisa cha Lutu, mpwa wake Ibrahamu, nacho kinashangaza. Kwamba ili kuwalinda wageni wake wasilawitiwe na mafidhuli ya Sofoma, Lutu anawatoa mabinti zake vigoli wabakwe. Hilo halikuonekana ni kosa kwa Mungu, bali lilikuwa kosa kubwa kwa mkewe Lutu kugeuka na kutazama jinsi vijiji vya Sodoma na Gomora vilivyokuwa vinateketea kwa moto, kiasi kwamba alistahili adhabu ya kugeuzwa mhimili wa chumvi!

Ibrahimu anapewa taji la kuwa ‘baba wa imani’ kwa kutii agizo la mungu la kumteketeza mwanawe kama sadaka. Hatuelezwi ni nini zilikuwa hisia za mtoto alipokuwa amefungwa kwenye lundo la kuni na kuona baba yake akinyoosha mkono akitaka kuondoa uhai wake.

Kwenye kitabu cha Kumbukumbu la Torati kuna maagizo ya kutamahusha ambayo huwezi kwa akili ya kawaida kufikiri yametolewa na mungu huyu mwenye upendo na aliyejawa na huruma.

Kuna mengi ya kushangaza yanayompa mungu taswira ya ukatili, hasira, wivu uliopitiliza na hata uovu. Ila hatutakiwi huhoji au kusoma kwa kutafakari bali kwa ufunuo wa roho!
 
Back
Top Bottom