Kumbe mafuta ya kula kenya ni cheap

Mkuu Wakenya wengi hawana address wengi waliokua wanapeleka bidhaa Kenya wametapeliwa sana na wengine walikopa Bank wale jamaa watu wanafanya nao biashara ya kuchukua bidhaa kwao na si kupeleka kwao na ndio maana sasa hivi wanakuja wenyewe kuchukua bidhaa zinazohitajika kwao...
 
Address kivipi boss
 
Address kivipi boss
Nazungumzia Address ya makazi ya kudumu wengi unakutana nao Nairobi ila sio wakaaji wa Nairobi wakishatapeli wanarudi makwao tofauti na Tanzania ukimkuta mfanyabiashara Mbeya,Dar au Kilimanjaro ni mkazi wa maeneo hayo mfumo wa TIN unatubana wao hawabanwi na hivi ni matapeli hao jamaa hatari ndio maana ni rahisi na salama kununua mzigo kwao ila sio kuuza..Arusha watu wengi ni wabishi sana ila wameliwa vichwa na hao tena wengine wametafuniwa hadi mikopo ya Bank...
 
Okay mi nafanya nilipe nisepe na mi niko hapa mpakani kabisa
 
Okay mi nafanya nilipe nisepe na mi niko hapa mpakani kabisa
Hapo utafanikiwa kwa kufanya nao biashara hao watu ni shida Mimi ni mzoefu wa mipaka mingi sijui Tarakea,Holili,Namanga,Tunduma,Sumbawanga mpaka huko Kasumulu mimi mipaka ya Rwanda,Burundi na Uganda sijapita kibiashara...kuna mwaka nilipakia mahindi Swanga nikaenda kulipwa Holili hapo na msomali alidhani ataniacha kirahisi kumbe mimi nawajua vizuri...
 
Wale wasomali ni matapeli kwelii, afu hiyo mipaka ya Rwanda, Burundi iko easy Basi ukijaribu huko utawin
 
Wale wasomali ni matapeli kwelii, afu hiyo mipaka ya Rwanda, Burundi iko easy Basi ukijaribu huko utawin
Dereva wangu alidai msomali anapiga mkeka sana ikifika muda anaomba gari isimame apige mkeka na Mbeya alilipa nusu akadai gari ikifika Moshi anachukua nusu amalize akashushiwe tuu kufika Moshi anamwambia mpaka Holili wamefika Holili yeye ndio anamlipia kila kitu Dereva anamwambia asiwe na shida wachukue vibali gari ikashushe tuu atalipwa huko huko alipinipigia simu nikamwambia unatapeliwa akulipe hapo hapo usitoe gari msomali alivyoona dili limebuma ikabidi aende Nairobi aje na mteja wakauziana mzigo ukiwa kwenye ghara ilibidi Mimi ndio nikamalize mchezo kwa kusafiri maana nikawaambia washushe ghara lolote alipie kwa siku kadhaa msomali alichemka na mbinu yake mbovu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…