Kumbe maisha ni bure kabisa, kuanzia leo sitajisumbua kwa lolote

Kumbe maisha ni bure kabisa, kuanzia leo sitajisumbua kwa lolote

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Habari zenu?
Nakumbuka 2014 kipindi naingia Dar es salaam rasmi kutafuta maisha nilitamani angalau nami ifike siku niwe nimepanga hata chumba cha giza.

2015 nikapanga chumba Keko cha 30. Muda kidogo nikapanga cha 35, then nikapanga chumba na sebule kwa 100k. Then nikanunua viwanja na nimejenga nyumba 2 moja Pugu na nyingine Mvuti Ilala.N Nimenunuapikipiki na sasa gari ya kutembelea.

Vyote hivyo bado naona kama sina kitu, sina utofauti na kipindi kile nimekuja Dar naishi kwa ndugu kwa masimango.

Nilichogundua maisha ni yaleyale, hata uwe na nini huna utofauti na yule ambaye anaishi mtaroni.
Kila hatua unayoifikia utaiona nothing na utatamani hatua imayofuata, huo ndio mchezo utakaoufanya until you die.
Binafsi nitaendelea kufanya kazi ila sitahangaika au kupaparikia maisha.

Jiulize bilionea kama Mo Dewj and so bado wanaendelea kusaka fedha.
Duuuuh
 
We jomba hujapata bhana

Ila umepatikana

Mwenyew nacho hajimwambafy hivo,
 
Yan ni kupiga kazi hamna namna,watu bado wanalala kwenye stoo za mafuta ya petroli na dizeli....ngoja tupige kazi tu
 
Wazee wetu furaha yao walikua wanaipata kwenye utu, upendo na kusidiana kwa hali na mali bila kujali huyu ni masikini au tajiri.
Sisi furaha yetu tunaitafuta kupitia vitu, tunajiaminisha tukiwa na magari mazuri, majumba mazuri, Mke/mume mzuri, pesa nyingi ndio tutakua na furaha kumbe ni ubatili mtupu.
 
Back
Top Bottom