Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Siku zote nimekuwa naamini kuwa mfumuko wa bei ni kitu kibaya hadi juzi kati nilipoona kinyume chake kwenye kitabu kimoja. Kabrasha hilo linasema kuwa mfumuko wa bei hadi wa 20 percent unasaidia kukuza uchumi.
Huu unasaidia kutengeneza ajira na kuchangamsha shughuli za kiuchumi. Linaendelea kudai kuwa mfumuko hadi wa 40% hauna athari zozote mbaya kwenye uchumi. Ila Aidi ya hapo ndipo kunakuwa na hyperflation ambao ni sumu kwa uchumi.
Muandishi anashauri kuwa nchi maskini zinatakiwa kumantain mfumuko wa bei hadi wa 20% ili kukuza uchumi wao. Anatoa ni mifano wa nchi ambazo ziliona ukuaji mkubwa wa uchumi wakati zina mfumuko mkubwa na jinsi ukuaji ulivyoshuka baada ya kudhibiti mfumuko.
Hii ni tofauti kabisa na IMF wanavyozilazimisha nchi maskini kuwa na mfumuko wa bei wa single digit. Unakuta hadi serikali zinajisifu kuwa mfumuko wa bei ni 5%, au 4%.
Anasema kuwa watu pekee ambao huathirika na mfumuko wa bei wa hadi 40% ni watu ambao wana kipato fixed kama waajiriwa, lakini anasema kuwa hata nao wanaweza kufaidika kwa ukuaji wa uchumi.
Kumbe mfumuko wa bei ni kitu kizuri!