Nilidhania utasema importation. Sababu imports huwa zinauwa mambo mengi sana mfano viwanda, lakini pia bei zinakuja kwa thamani ya pesa ya kigeni hivyo inasababisha kuongezeka matumizi.
So mfano malumalu, na vifaa vya ujenzi kipindi cha nyuma tulikuwa tunachukua sana nje ambapo ukipiga hesabu kuna kodi, tozo, usafiri wa meli ukijumlisha hela inakuwa kubwa sana ila sasa vinatengenezwa hapa hapa tazama bei zilivyoshuka kwa zaidi ya asilimia 70.
Kwa upande wa export ni tofauti export ndio huwa mkombozi wa uchumi wa sisi mataifa ya dunia ya chini.
Korosho bongo naweza uza kilo mwisho 2000 ila nje kilo nitauza 12,000 sasa huoni hiyo income kwa bidhaaa ile ile na hii itasaidia mimi kuongeza uwekezaji wangu uwe imara katika kilimo cha korosho.
So nadhani ungejielimisha kidogo kuhusu kilimo.