Kumbe mlenda sio mboga

Kumbe mlenda sio mboga

Watu Wa Tabora wanataabu

Tabu ipi tena mkuu? Kula swalu au ulimaanisha kula nsansa na msusa? Hizo ni mboga za asili mkuu zinathamani yake si tabu ni starehe tu kwi kwi kwi karibu sana
 
Napenda mlenda ukiwa umemixiwa na nyama au maharage,lakini nikikuta umekaa single hakuliki hapo

Vikikosekana hivyo hapo juu basi angalau mtindi pembeni nikitoka hapo natafuta sehemu ya kuweka tumbo
 

attachment.php
 
Kwangu mimi ni mboga namba moja nikiwa nyumbani lazima nipike swalu jina lingine kirumbu lingine ndalu na lingine lilende kwi kwi kwi naupenda

Aaale mwana idodomiya,
HUKU WENZIO wanauita MOROROI.
Wairaqw wanaijua
 
Kwangu mimi ni mboga namba moja nikiwa nyumbani lazima nipike swalu jina lingine kirumbu lingine ndalu na lingine lilende kwi kwi kwi naupenda
kama unakula na ugali si mboga ni kisababishi
 
Amavubi hebu nipikie mlenda walau nijue ladha yake inafananaje sijawahi kula hii kitu nasikia tu
 
Last edited by a moderator:
Amavumbi hebu nipikie mlenda walau nijue ladha yake inafananaje sijawahi kula hii kitu nasikia tu

Upo mkavu ukatwangwa na karanga, ila wewe pika hivi; chukua majani ya maboga kumi na tano na bamia tano za wastani hata sita OSHA chemsha maji ktk sufuria mdogo maji vikombe viwili au kadiria katakata bamia na majani ya maboga kidogo kidogo kama unavyokata kabichi maji yakichemka weka hayo majani na bamia ukipenda weka magadi kidogo ukitaka weka nyanya na karanga acha iive taratibu chumvi weka baadae kidogo baada ya muda ipua mlenda tayari kuliwa na ugali. Nakuamia wewe ni mpishi hushindwi kuvanya hivyo
 
Last edited by a moderator:
Nimetoka kijijini irangi majuzi Kati hapa bibi alipika na ugali aisee wacha kabisaa.ni tamuu
 
Back
Top Bottom