Kwanini hutaki kukubaliana na ukweli kwamba huyu jamaa alipeleka kesi ya kudai haki yake katika MAHAKAMA za Tanzania na alishinda kesi na serikali ya Tanzania kuamriwa kumlipa $36M?, hata baada ya serikali ya Tanzania kukata rufaa MAHAKAMA ya rufaa pia lishindwa?
Huyu jamaa kwenda huko South Afrika, alikwenda kukazia hukumu, kwenda kuomba nchi zingine kimsaidia kuishindikiza serikali ya Tanzania kumlipa kile walichoamuriwa na MAHAKAMA za Tanzania, wala sio mahakama za nje, tatizo lipo wapi kama mtu anapigania kulipwa haki yake halali aliyopewa na mahakamani?, huu ni uzalendo gani wa kushabikia serikali kukiuka amri za MAHAKAMA heti kwa sababu ni mzungu?
Hata wanasheria wetu hawakanishi kwamba hatudaiwi, wao wanachodai ni kwamba, kisheria alipaswa kutumia mahakama za Tanzania. Kitu cha kushangaza ni kwamba, hao wanasheria wetu wanaomkosoa huyu jamaa kwa kutotumia mahakama za Tanzania, ndio hao hao ambao wamekua wakipuuza AMRI za MAHAKAMA hizo hizo za Tanzania.
Huu wimbo wa "Mabeberu hawatutakii mema" unapendeza zaidi tukiuimba kwa kuangalia "Muktadha" na mazingira, huwezi kuimba nyimbo za "Bongo flava" katika msiba, japo ni wimbo MZURI, ila mazingira yake hayaruhusu.