Kumbe nilikuwa nakosea sana kuwadharau Wanawake kwenye Uongozi

Kumbe nilikuwa nakosea sana kuwadharau Wanawake kwenye Uongozi

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Hakika waswahili hawakukosea waliposema mmzaniaye ndiye kumbe siye, maisha yangu yote sikuwahi kudhani au kuwaza kuwa mwanamke anaweza kusimamia vitu vikaenda sawa sawa bila kasoro.

Ila kwa kinachoendelea sasa hakika wanaume tunaona aibu kwakeli tumetawala hii nchi kwa miaka 60 lakini huyu mama ametawala kwa siku 100 tu na ameonesha uwezo mkubwa sana wa kiutawala.

Yaani kwa sasa mama anafanya mambo mpaka unafurahi nchi imekaa kwenye mstari vizuri sana, yanayofanywa na mwanamama huyu yanahitaji pongezi, nakiri kwamba toka tupate uhuru huyu rais wetu pekee mwanamke anatufundisha namna mwanamke anavyoweza kuwa hazina kwenye uongozi yaani nchi inasimamiwa na mwanamke na inakaa sawa kabisa.

Kuanzia leo wanawake nitakuwa nawatilia maanani sana hasa kwenye utawala na uongozi.

Kakikaka wanawake Mungu awabariki na hongerenii saana.
 
Ameongelea jana hiyo program ya kuitangaza nchi, akitumia maneno rebranding. Naamini yupo vizuri katika masuala ya mawasiliano, anao uwezo wa kukaribisha mtu kwa lugha ya muonekano bila hata ya yeye kuzungumza na hiyo ni sifa nzuri kwa kiongozi wa nchi kuwa nayo.

Mtihani mkubwa upo kwa watendaji wa wizara na taasisi zetu. Uzembe mwingi na ile incompetence inaonekana kutopungua. Hayati JPM alijitahidi sana kupambana na uzembe na upungufu wa uwajibikaji lakini tatizo bado lipo.

Akiweza kupata ushirikiano wa kiutendaji kwa maana ya uwepo wa wepesi wa maamuzi ya kiserikali anaweza kuja kuipaisha Tanzania ikafika mahali fulani pa kuheshimiwa.
 
Historically,women are natural leaders. Wanawake wanakwamishwa na mifumo mibovu na udhaifu wa kimaumbile na sababu za kibaolojia. Lakini wamefanya makubwa sana kwenye tawala za kale.
hakika mkuu wanawake ni jeshi kubwa..
 
Ione Germany chini ya Angela Merkel. Nchi imetulia na inafanya makubwa kabisa.

Nadhani baada ya Mama Samia tumpe Ummy Mwalimu. Wanaume tukae pembeni kwanza. pumbavu sana yule mtu, miaka mitano ameharibu kila kitu, siku100 mama kafanya makubwa.

Roast in hell jiwe.
 
Ione Germany chini ya Angela Merkel. Nchi imetulia na inafanya makubwa kabisa.

Nadhani baada ya Mama Samia tumpe Ummy Mwalimu. Wanaume tukae pembeni kwanza. pumbavu sana yule mtu, miaka mitano ameharibu kila kitu, siku100 mama kafanya makubwa.

Roast in hell jiwe.
Hapa ndio naposhangaa, kwa hiyo lissu basi tena?
 
Bado mapema sana hata Magufuli siku za mwanzo alikuwa akiambiwa hivi.

Nachoona ni kama bado watu wana hang-over ya mwendazake, hangover ikiisha ndio picha halisi itaoonekana.

Hata kipindi JK ametoka madarakani miezi ya mwanzo watu walikuwa na hangover yake, hivyo kila alichofanya Magufuli kilionekana dhahabu Ila baada ya muda ukweli ukaonekana.

Tusubiri
 
Unajua uongozi pia unataka utulivu wa akili, hekima na busara. Mhe Samia ametulia sana hata ukimuangalia usoni, hana mihemko.. Tumuombee kwa Mungu asibadilike na asipate kiburi na majivuno kama Mwendazake...
 
Hakika waswahili hawakukosea waliposema mmzaniaye ndiye kumbe siye, maisha yangu yote sikuwahi kudhani au kuwaza kuwa mwanamke anaweza kusimamia vitu vikaenda sawa sawa bila kasoro...
Mwanamke ni kiumbe mmoja very strong.

Ndio maana hata kwenye familia mwanamke akiwa hajielewi hata hiyo familia yenyewe inakufa.

Kuna nyumba ( homes ) za watu ambao kila mtu anakuwa anajua pale kwa fulani ila ndoa zikivunjika au mwanamke kupotoka, hilo eneo ukipita unakuta nyumba yenyewe imeshaanguka na eneo limegeuka shamba.

Ni rahisi sana kwa single mother kumlea mwanaye kwa ufanisi mkubwa kuliko single father kufanya hizo.

In short Mungu aliiumba hii dunia very perfect, ni basi tu sisi binadamu ubishi na udadisi umekuwa mwingi mpaka unavuka mipaka.
 
Bado nchi yetu haijafika level za kuongozwa na wanawake sio kwamba wanawake hawewezi uongozi. Ila makuzi ya wanawake hapa Tanzania ni kumsikiliza mwanaume tena kama wanawake waliozaliwa kabla ya mwaka 2021.

Makuzi yao ni kumsikiliza mwanaume so hata tukiwa na kiongozi wa kike wanaume wa3 wakimzunguka tuu wanambadilisha mawazo faster inshort msimamo wa wanawake inatokana na maamuzi ya wanaume.

Ukibisha kaa chini mwangalie mkeo, mama yako au dada yako huwa anamsikiliza nani zaidi
 
Bado nchi yetu haijafika level za kuongozwa na wanawake sio kwamba wanawake hawewezi uongozi. Ila makuzi ya wanawake hapa Tanzania ni kumsikiliza mwanaume tena kama wanawake waliozaliwa kabla ya mwaka 2021, makuzi yao ni kumsikiliza mwanaume so hata tukiwa na kiongozi wa kike wanaume wa3 wakimzunguka tuu wanambadilisha mawazo faster inshort msimamo wa wanawake inatokana na maamuzi ya wanaume.
Ukibisha kaa chini mwangalie mkeo, mama yako au dada yako huwa anamsikiliza nani zaidi
Kumsikiliza mtu haijawahi kuwa jambo baya.

Jambo la msingi na wewe ukishasikiliza watu na wewe unakaa unaona kipi ni sahihi.

Serikali ni dubwana kubwa na katili lenye mchanganyiko wa kila kitu. Kwahiyo wewe mtu mmoja mwenye kichwa huwezi kuwa mtaalamu wa kila kitu.
 
Historically,women are natural leaders. Wanawake wanakwamishwa na mifumo mibovu na udhaifu wa kimaumbile na sababu za kibaolojia. Lakini wamefanya makubwa sana kwenye tawala za kale.
hiyo historia y wapi wanawake ni viongoz iko wapi? acha kupotosha jamii, mwanamke kaumbwa kuzaa,kutunza na kulea familia tu, sio kuongoza group la watu wakiwepo wanaume, ndiomaana viongz weng wa kike wanakosa confidence na maamuzi magumu maana hawana haiba ya kuongozs bali kuongozwa, rudi chekechea ukasome upya history
 
Kumsikiliza haijawahi kuwa jambo baya.

Jambo la msingi na wewe ukishasikiliza watu na wewe unakaa unaona kipi ni sahihi.

Serikali ni dubwana kubwa na katili lenye mchanganyiko wa kila kitu. Kwahiyo wewe mtu mmoja mwenye kichwa huwezi kuwa mtaalamu wa kila kitu.
Nchi yetu kiongozi ndio kila kitu watu wanafanya viongozi wanavyofanya... Kiongozi akiwa tapeli nchi nzima inakuwa matapeli
 
Back
Top Bottom