Kumbe Nyerere alikuwa mzalendo kiasi hiki? Leo tuna matapeli tu

Kumbe Nyerere alikuwa mzalendo kiasi hiki? Leo tuna matapeli tu

Magufuli 05

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2023
Posts
1,433
Reaction score
2,791
1.Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.

10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika.
 

Attachments

  • Screenshot_2024_0121_124140.png
    Screenshot_2024_0121_124140.png
    218.4 KB · Views: 5
Hizo ni ahadi za mwana TANU enzi za utawala wa chama kimoja!
 
Back
Top Bottom