Taharuki iliyotokea jana Miss Gonzalez nafikiri umeiona hata wewe na Magori ilibidi muingilie kati kutoa maneno ya faraja huko twitter na instagram na bado leo pia na wewe umerusha vijembe vya kiaina
Yote haya ni kutokana na jinsi team inavyopwaya nafasi muhimu za namba 9 na namba 6 mlizokuwa na karibu miezi 3 kuzihangaikia MKAZIPUUZA, imani kwenu imepungua sana mmekuwa kama yule kiongozi mkubwa serikalini tena shabiki wa simba anayeongeaga mambo ya uongo uongo kila siku ambaye hata akikuambia kesho jua litawaka unajiuliza mara mbilimbii kama ni kweli
Shukuruni sana huyo manzoki inaonekana ka calculate kuja kutengeneza ufalme wake simba na siyo kuuchukua wa mayele na pia yanga wameonyesha kwamba wakitaka kitu kizuri ubahili kwao ni msamiati ni vile tu jamaa kawakatalia
Ndugu zangu YANGA LEO SAA TANO WANAMTAMBULISHA KEVIN TWISSA NA JACKSON GROUP YAKE kusimamia digital marketing and branding, smart move sana.
========