Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kumbe sababu ya kifo cha Mpendwa wetu, Benjamin William Mkapa ni Cardiac Arrest!.

Asante sana Mwanafamilia wa familia ya Mkapa, William Erio, kuusema ukweli huu na kumaliza rasmi ile sintofahamu ya chanzo cha kifo, ambayo imezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo JF.

Kama Tangazo la kifo lingezingatia sheria tangu pale mwanzo, wala kusingetokea sintofahamu yoyote!.

Hivyo japo haijasemwa ni JF, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Japo yanalaumiwa kwa kuonekana watu wana mind vitu vidogo vidogo ambayo sio vya msingi, lakini yanasaidia.

Chanzo cha kifo cha ghafla cha any state leader ambaye hajawahi kutamkwa kusumbuliwa na maradhi yoyote, automatically kita send a shock wave kwenda viral.

Baada ya kauli hii, sasa minongo yote kuhusu chanzo cha kifo imemalizwa rasmi.
Naombeni sana, wanabodi, tuwe na heshima kwa viongozi wetu na tuwe na heshima kwa marehemu, mkiisha ambiwa ukweli wa familia, then tuupokee ukweli huu, tuuamini, na kumheshimu Marehemu kwa kuto toa comments zozote negative based on hisia!.

RIP, Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

Paskali
 
Sijui wataalamu, cardiac arrest ni mara moja tu, sio upate jumatano ufariki Ijumaa

Mbili, issue cardiac nilitegemea angepelekwa Hospitali yetu ya mabingwa wa moyo pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute na sio Hospitali Mzna

Tungeacha tu kujadili tumzike Mzee wetu tuendelee na mengine maana tunazidi kuleta mkanganyiko
 
Hujui kwamba hapo EMMH walikua na department ya Moyo kabla hata JK hajawahengea wamatumbi JKCI

Toka yeye alivyopata lile Tatizo la kuanguka siku moja kabla ya Uchaguzi
 
Sijui wataalamu, cardiac arrest ni mara moja tu, sio upate jumatano ufariki Ijumaa

Mbili, issue cardiac nilitegemea angepelekwa Hospitali yetu ya mabingwa wa moyo pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute na sio Hospitali Mzna

Tungeacha tu kujadili tumzike Mzee wetu tuendelee na mengine maana tunazidi kuleta mkanganyiko
Hiyo kitu ilimpata jamaa yangu mmoja hiv alifia hapo hapo. Na hakuwa na historia ya ugonjwa wowote. Imepita miaka 5 sasa
 
Still connecting the relation of Malaria with Cardiac arrest sipati jibu? but kuna uhusiano mkubwa kati ya upumuaji na shambulio la moyo.

Jiongezeni wakubwa, Israel mtoa roho bado anawinda roho za watu wenye shingo ngumu.
 
Pascal Mayalla,

Tuwaulize Wataalam Madajtari cardiac arrest huwa inasababishwa na nini??
1. stroke- leading herniation on the brainstem
2. Respiratory failure leading to overwhelming compansation of cardiac output

3. Electrolyte imbalance

4..........
5.......

Hii ni kwa mujibu wa Google.

Ngoja tusikie wataalam madaktari
 
Sijui wataalamu, cardiac arrest ni mara moja tu, sio upate jumatano ufariki Ijumaa

Mbili, issue cardiac nilitegemea angepelekwa Hospitali yetu ya mabingwa wa moyo pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute na sio Hospitali Mzna

Tungeacha tu kujadili tumzike Mzee wetu tuendelee na mengine maana tunazidi kuleta mkanganyiko
Alilazwa kutokana na malaria
 
Hivi cardiac arrest huwa mgonjwa analazwa hospitali, anapiga stori na wanaomtembelea wee ndipo inamuua? Hapa kuna walakini. Itoshe tu kusema RIP Mkapa. Mambo mengine wanafamilia waendelee kuyafanya siri yao, wasiingie kwenye mtego wa kutuliza uvumi unaoendelea.
 
Back
Top Bottom