Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Hivi cardiac arrest huwa mgonjwa analazwa hospitali, anapiga stori na wanaomtembelea wee ndipo inamuua? Hapa kuna walakini. Itoshe tu kusema RIP Mkapa. Mambo mengine wanafamilia waendelee kuyafanya siri yao, wasiingie kwenye mtego wa kutuliza uvumi unaoendelea.
Shambulio la moyo mara nyingi mtu huwa yupo kwenye coma na anakuwa chini ya uangalizi wa madaktari muda wa kuzungumza zaidi ya saa zima anatoa wapi...

Naona awamu hii shambulio la moyo ndio kimbilio..
 
Mkuu, mimi nina uelewa kiasi kidogo wa haya mambo. Ukiangalia vyeti vyote vya kifo, kuna kitu kinaitwa "immediate cause of death". Immediate cause ya vifo vyote duniani ni cardio-pulmonary arrest. Ufe kwa cancer, COVID-19, HIV/AIDS, kuishiwa damu wakati wa kujifungua nk, ili ufe ni lazima hivi visababishi visabibishe "cardio-pulmonary arrest" (moyo na mapafu kutokufanya kazi ama moyo kufa). Alichotakiwa kusema Erio ni nini kimesababisha cardiac arrest kwa mzee wetu. Hicho pengine hatokisema.

Nikupe mfano. Ni kama mtu kasema nyumba imebomoka bila kutoa chanzo chake. Inaweza kubomoka kwa maporomoko, kubomolewa na grader kwa vile umejenga barabarani nk. Nadhani umeelewa.

Update: Kwa mujibu wa wachangiaji wengi humu wanasema ni malaria. Kwa hiyo malaria ndio pengine imesababisha "cardic arrest" kwa mzee. Lakini kusema tu "cardiac arrest" ni sawa na kusema kifo chake kimesababishwa na kifo.
Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana Mwanafamilia William Erio Kumaliza Sintofahamu Hii!
 
Siasa isitugawe jamani, mavi-jana ya Tanzania mbona mnataka kuwa wapumbavu na malofa namna hiyo? Kwani kabla ya Corona watu walikuwa hawafi kwa heart attack? Majitu yamekomalia eti tuongeze na zetu, zipi hizo? Tuache umazwazwa!!
 
Hivi cardiac arrest huwa mgonjwa analazwa hospitali, anapiga stori na wanaomtembelea wee ndipo inamuua? Hapa kuna walakini. Itoshe tu kusema RIP Mkapa. Mambo mengine wanafamilia waendelee kuyafanya siri yao, wasiingie kwenye mtego wa kutuliza uvumi unaoendelea.
Hivi umesikia alichosema Errio

Amesema hivi "..... Mzee Mkapa alilazwa kwa Malaria wakati akiendelea na matibabu ndio akapata shambulio la moyo na kufariki..."

Shambulio la Moyo hutokea ghafla kama ilivyo kwa Mzee Mkapa
 
Wewe P Ulisikiaje minongono hii,au na wewe ni wale jamaa wa systerm wa kuweka mambo sawa?
Well done, Hoja yako jana ilikuwa ya msingi sana
Kweli Ikulu walikurupuka kutowa taarifa pumgufu.
Huku mtaani kwangu Tayari speculation zilikuwepo ya kuwa eti 'Magu hakuufurahia ushauri wa Mkapa wa Tume huru''
Na kwa hiyo Mkapa alimnunia Magu,
Na kwa hiyo Magu kamtumia wale jamaa wasiojulikana
Na kwa hiyo wamemkolimba.
Haya ndio maneno yaliyokuwa yanaanza kusambaa mtaani,
Kisa nini Taarifa ya msiba kutolewa pungufu.
Naona sasa mambo yako sawa.
Thank You P.
 
Bado kuna mkanganyiko kikwete anasema mkapa alimwambia kinachosumbua ni tumbo leo tunaambiwa malaria na moyo
 
Hivi cardiac arrest huwa mgonjwa analazwa hospitali, anapiga stori na wanaomtembelea wee ndipo inamuua? Hapa kuna walakini. Itoshe tu kusema RIP Mkapa. Mambo mengine wanafamilia waendelee kuyafanya siri yao, wasiingie kwenye mtego wa kutuliza uvumi unaoendelea.
Muwe mnaelewa kwanza kabla ya kubisha. Maelezo ni kuwa aliugua malaria kwanza ndiyo akalazwa. Sasa hiyo cardial arrest ilimpata ghafla wakati amelazwa. Pengine ungehoji labda dawa au matibabu aliyopata ndiyo yalileta hiyo hali? Au ilikuwa ni coincidence tu?
 
Back
Top Bottom