Wasomaji kabla ya kuchangia, jaribu kujua tofauti kati ya cardiac arrest na cardiac (heart) attack. Taarifa inayoongelewa hapa haisemi Mkapa amekufa kwa heart attack. Msitake kuongeza maneno ambayo hayakusemwa na Erio na kwa hiyo hayapo kwenye death certificate ya Mkapa.
Mkuu kama hufahamu kuhusu Cardiac Arrest ni bora ujifunze tu kabla ya kuandika ulichosema..
Moja ya sababu kuu ya Cardiac Arrest ni Heart Attack ambayo nayo husababishwa na ugonjwa wa moyo uitwao Coronary Heart Disease.
Heart Attack na Cardiac Arrest are not the same.
Mimi nimejifunza masuala ya kutoa huduma ya kwanza ambayo ni sehemu ya kozi maalum ndefu nilipokuwa chuo fulani hivi, suala la cardiac arrest linaweza kudhibitiwa.
Mtu anapopata cardiac Arrest anakuwa amepoteza fahamu na hawezi kusikia chochote yaani "unresponsive".
Kisha mgonjwa anashindwa kupumua uzuri yaani anakuwa apumua kwa shida na kutoa sauti ndogo sana huitwa "gasping noise"
Sasa kama ni hospitali ya maana mgonjwa anakuwa amewekewa kifaa maalum cha kutoa alarm au "panick alarm" ili kuwaita madaktari au manesi ambao wataona taa ya njano ikiashiria kuwa chumba fulani kuna shida.
Sasa hapo manesi na madaktari watakwenda kwenye chumba cha mgonjwa wakiwa na chombo chaitwa "Defibrillator" ili kumfanyia mgonjwa kitu chaitwa CPR yaani "cardiopulmonary Resuscitation" .
Wagonjwa wengi hufariki kwa Cardiac Arrest kutokana na kukosekana miundombinu mizuri ya kihospitali na pia kukosa hivyo vifaa nilivyovitaja hapo juu kutokana na kugharimu mamilioni ya fedha kuwa navyo.
Pia huweza kuwepo manesi au madkatari ambao kufanya CPR inaweza kuwa mgogoro kutokana na hali ya mgonjwa.
Hivyo ukilazwa hospitali isiyojulikana na ukapatwa na tatizo hilo la cardiac Arrest basi huwa shida.
Naomba niishie hapo.
RIP mzee Ben Mkapa.