Kumbe serikali kupitia jeshi la polisi waliwazuia CHADEMA kama chama kuingia Katesh - Hanang kufariji wahanga wa maafa na kutoa misaada?

Kumbe serikali kupitia jeshi la polisi waliwazuia CHADEMA kama chama kuingia Katesh - Hanang kufariji wahanga wa maafa na kutoa misaada?

Hao Mapolisi walipokea maagizo kutoka juu swali la kujiuliza ni nani huko juu?
Polisi wenyewe ndiyo wajinga na wapumbavu...

Sheria inayoongoza utendaji kazi wa polisi wa siku Kwa siku zipo, lakini hawazifuati badala yake wanafuata maagizo na maelekezo ya viongozi wa kisiasa yenye maslahi ya wanasiasa hao huku wakitupa sheria na miongozo ya utendaji kazi wao pembeni...

Kama huo sio ujinga na upumbavu wa jeshi hili, tuite ni kitu gani eti?

Kwa mwenendo huu wa jeshi hili, Wala sio hata kufikiria kuwa walipewa order na kiongozi fulani huko juu. Hawa wanaweza kupewa order iliyo nje ya sheria Police General Orders (PGOs) hata na balozi wa nyumba kumi ili mradi ni WA CCM na wakaifuata na kuitekeleza..!
 
Anaandika Malisa G.J toka FB page yake

Baada ya msafara wa Mbowe kuzuiwa na jeshi la polisi kwenda wilayani Hanan'g kwenye eneo lililokumbwa na maafa, Mbowe alilaumu kitendo hicho kuwa si cha kiiungwana na kinawagawa watanzania kwani wahanga wa Hanan'g wanahitaji faraja ya watu wote.

Mbowe alitaka kuahirisha ziara yake, lakini viongozi waandamizi wa Serikali, na viongozi waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama walimpigia na kumsihi asikatishe ziara hiyo. Viongozi hao walimjulisha RPC Manyara kuwa serikali imefuta maagizo yake na kwamba viongozi wa Chadema waruhusiwe kwenda Hanan'g.

Baada ya kuondolewa kwa zuio hilo batili na la "kipumbavu" la Polisi, hatimaye Mbowe na msafara wake wamefika Hanan'g na kutembelea Kata za Katesh, Ganana na Jorodom ambazo zimeathirika zaidi na maafa hayo. Viongozi hao wametembelea baadhi ya kaya na kutoa pole pamoja na kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu.

Mhe.Mbowe amesema, "...Tulikusudia kusitisha ziara yetu lakini viongozi kadhaa waandamizi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wametusihi tusikatishe ziara na wametengua zuio la polisi. Tumetafakari na viongozi wenzangu. Hekima imetuelekeza kuwa wahanga wa maafa ya Hanan'g ni Watanzania wenzetu na wanahitaji faraja ya kila mmoja wetu. Nia yetu njema ya kuwapa faraja haiwezi kuzuiliwa na amri batili ya polisi. Tumekubali kuendelea na ziara kama ilivyopangwa awali..."

NOTE:
Sasa naelewa ni kwanini chawa wa CCM wakiongozwa na Lucas mwashambwa walisambaa mitandaoni kurusha propaganda nyingi kuihusu CHADEMA wakiuliza maswali kama;

"...Nani kawaona CHADEMA wamesema au kwenda Hanang kushiriki faraja na kutoa pole kwa wahanga..."

Kumbe haya majamaa yalishafika polisi Manyara na kumtisha RPC na kisha kumpa order ya kijinga na kipumbavu wawazuie CHADEMA kufanya au kuingia Hanang kulia na kufarijiana na ndugu zao waliofiwa na kuathiriwa na janga la maporomoko...

CCM na chawa wao wana tabia mbaya sana zilizojaa ushetani wakionekana kama binadamu hivi lakini tabia, mwenendo na matendo yao ni mashetani ktk sura za binadamu!!
Naomba kujua ni msaada gani chadema walioutoa huko Hanang

CC Erythrocyte
 
Back
Top Bottom