Kumbe TikTok sio ya kinyonge, sikutegemea itakuwa ya kiharakati namna ile

Kumbe TikTok sio ya kinyonge, sikutegemea itakuwa ya kiharakati namna ile

Mashamba Makubwa Nalima

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2024
Posts
7,656
Reaction score
3,785
wamenishangaza, sikutegemea, nilijua content zao ni za SOFT life na udaku pekee, wamenifurahisha.

Kumbe vijana mnapenda HAKI, kumbe vijana unapenda DEMOKRASIA, basi mmetisha.

Hakuna ubaya kuwa na mizuka na mambo mengine, ila kupotezea kabisa mambo ya nchi na maisha yako ni upumbavu zaidi na hauhitaji kutetewa.

Mmenifurahisha

Mods poleni kwa likizo.

Uzi tayari.
 
Gen Z wa 2010 kuendelea ndio watakomboa nchi kutoka kwa majangili na vibaka wa CCM maana kaaelimu kanawafikia na maisha yalivyokuwa magumu milio lazima iwatoke sie kaka zao wa 1990s kazi imetushinda ila nitawapa full support
Kabisa, baada kuondoka kile kizazi kilichokuwa active kipindi cha Kikwete nikawa na wasi wasi ila nina imani
 
wamenishangaza, sikutegemea, nilijua content zao ni za SOFT life na udaku pekee, wamenifurahisha.

Kumbe vijana mnapenda HAKI, kumbe vijana unapenda DEMOKRASIA, basi mmetisha.

Hakuna ubaya kuwa na mizuka na mambo mengine, ila kupotezea kabisa mambo ya nchi na maisha yako ni upumbavu zaidi na hauhitaji kutetewa.

Mmenifurahisha

Mods poleni kwa likizo.

Uzi tayari.
Wataifungia nayo,vitu vingine muwe mnayamaza tu,umbe wa nini.
 
Mimi huwa napaita ni University ina mambo mengiya kujifunza na kupaaa
Nilipoanza kuyajua nilijua mengi na ukipata kuyajua mule ni sehemu ya kupata mapato ila bila kusahau kuwa na mengine unajiongeza kando
ni sehemu ya kujiongeza pia usibaki nyuma
Maana hao ukikosea tu ni bai bai
 
Sasa hivi kila ukiingia unakutana na Live za kutosha za kuhamasisha maandamano ya amani, tofauti na awali vijana walikalia live kuongea mada za wapenzi na kutafuta wachumba.
 
Back
Top Bottom