Kumbe tulimsifu Hayati Magufuli kwa kubana matumizi huku Serikali ikiwa na matumizi ya ovyo hivi?

Kumbe tulimsifu Hayati Magufuli kwa kubana matumizi huku Serikali ikiwa na matumizi ya ovyo hivi?

Kati ya vitu ambavyo Magufuli alikuwa akiimbwa navyo ni kubana matumizi ya Serikali

Ila leo baada ya kumsikiliza Mwigulu akiweka mikakati mipya ya kubana matumizi, nimeona kumbe Serikali ina matumizi ya hovyo ambayo hata huyo Magufuli aliendelea nayo hadi sasa Samia ndio anakuja kuyapunguza

Mojawapo ya lililonishtua ni kuwa Mkurugenzi au Katibu Mkuu akitumbuliwa bado anaendelea kulipwa mshahara uleule aliokuwa nao, akasema kuwa inawezekana hata ukakuta kuna wizara 15 tu lakini ukakuta kuna watu 50 wanalipwa mshahara wa katibu mkuu, ama kuna halmashauri 100 lakini wanaolipwa kama wakurugenzi ni 500.

Aisee
Wajinga.ndio mlikuwa mnamsifu..

Samia atawaaibisha Sana na kufunika kile mnaita legacy..

Nadhani mukeona bajeti ya SSH
 
Lakini Barabara zilijengwa miradi iliyobadilosha taswira ya Tanzania ilijengwa hapakuwa na ziara za kijinga nje ya nchi miundombinu ya afya elimu bure n.k iliomekana!
Hakuna kitu kiligwa? Miaka 5 alikuwa anafanya nini ikiwa SSH kwa mwaka mmja anafanya mambo makubwa kiasi hiki?
 
Lakini Barabara zilijengwa miradi iliyobadilosha taswira ya Tanzania ilijengwa hapakuwa na ziara za kijinga nje ya nchi miundombinu ya afya elimu bure n.k iliomekana!
Alikopa kuliko rais yoyote Tz na miradi mingi haijakamilika
 
Ili jambo la kuwalipa kulingana na vyeo ata ukitolewa kazini lilikuwapo kabla ata ya serikali ya awamu ya tano.

Sema ni jambo jema maana mtu anakaa nyumbani bila kufanya kazi huku anaendelea vuta mshahara mnene
Acha kujikosha,kwa hiyo wewe unabishana na Serikali aunhujaelewa?

Mfano unamtoa mtu kama demotion Kutoka kuwa mkubwa wa Taasisi fulani unampeleka kwa RAS harafu anaenda na salary aliyotoka nayo kule kwenye Taasisi,hii Sio sawa..
 
Mwigulu kasema hilo lonafanywa kwa sababu lipo kisheria na Samia itabidi wabadili sheria kwanza....So kipindi cha Magufuli walikuwa bado wanalipwa sababu sheria hazikubadilishwa

..lakini sheria huwa haigusi waliohusika kabla haijabadilishwa.

..watu walikuwa wanashangilia Jpm anavyotumbua watu serikalini, kumbe mwisho wake ni watu hao kulipwa mishahara bila kufanya kazi.
 
Kati ya vitu ambavyo Magufuli alikuwa akiimbwa navyo ni kubana matumizi ya Serikali

Ila leo baada ya kumsikiliza Mwigulu akiweka mikakati mipya ya kubana matumizi, nimeona kumbe Serikali ina matumizi ya hovyo ambayo hata huyo Magufuli aliendelea nayo hadi sasa Samia ndio anakuja kuyapunguza

Mojawapo ya lililonishtua ni kuwa Mkurugenzi au Katibu Mkuu akitumbuliwa bado anaendelea kulipwa mshahara uleule aliokuwa nao, akasema kuwa inawezekana hata ukakuta kuna wizara 15 tu lakini ukakuta kuna watu 50 wanalipwa mshahara wa katibu mkuu, ama kuna halmashauri 100 lakini wanaolipwa kama wakurugenzi ni 500.

Aisee
Tulimsifu JPM kwa kubana matumizi, ni pamoja na kutozurula nchi za nje!

Ni pamoja na usimamizi mzuri na wakaribu wa fedha kidogo iliyokuwa ikikusanywa
 
Tulimsifu JPM kwa kubana matumizi, ni pamoja na kutozurula nchi za nje!

Ni pamoja na usimamizi mzuri na wakaribu wa fedha kidogo iliyokuwa ikikusanywa
Hakuna Rais ambaye hasafiri, nchi yoyote duniani, kutokusafiri ni ushamba sio ujanja
 
Yaani huo ni mfano tu, unakuta mnaona wizara chache lakini makatibu wakuu wanalimbikizana kwenye payroll sababu wakitumbuliwa bado wanalipwa kama makatibu wakuu
Wametumbuliwa wangapi?

Mbona yeye anawalipa wa vyeti feki
 
Back
Top Bottom