Kumbe tulimsifu Hayati Magufuli kwa kubana matumizi huku Serikali ikiwa na matumizi ya ovyo hivi?

Kati ya vitu ambavyo Magufuli alikuwa akiimbwa navyo ni kubana matumizi ya Serikali

Ila leo baada ya kumsikiliza Mwigulu akiweka mikakati mipya ya kubana matumizi, nimeona kumbe Serikali ina matumizi ya hovyo ambayo hata huyo Magufuli aliendelea nayo hadi sasa Samia ndio anakuja kuyapunguza

Mojawapo ya lililonishtua ni kuwa Mkurugenzi au Katibu Mkuu akitumbuliwa bado anaendelea kulipwa mshahara uleule aliokuwa nao, akasema kuwa inawezekana hata ukakuta kuna wizara 15 tu lakini ukakuta kuna watu 50 wanalipwa mshahara wa katibu mkuu, ama kuna halmashauri 100 lakini wanaolipwa kama wakurugenzi ni 500.

Aisee
Kumbe watu walikuwa wanakosa tu ile heshima ya ukuu ila mshahara unaingia kama kawa.
 
Acha kujikosha,kwa hiyo wewe unabishana na Serikali aunhujaelewa?

Mfano unamtoa mtu kama demotion Kutoka kuwa mkubwa wa Taasisi fulani unampeleka kwa RAS harafu anaenda na salary aliyotoka nayo kule kwenye Taasisi,hii Sio sawa..

Mkuu unajua sheria inasemaje kuhusu mishahara?
 
Dalili za maendeleo kwa watz:
1. Kujadili hoja na sio muwasilisha hoja
2. Kupigania mipango ya maendeleo ya nchi na sio mipango ya wagombea, kama umoja kwenye vita vya kagera kutokana na masimulizi mbali mbali.
 
Kati ya vitu ambavyo Magufuli alikuwa akiimbwa navyo ni kubana matumizi ya Serikali

Ila leo baada ya kumsikiliza Mwigulu akiweka mikakati mipya ya kubana matumizi, nimeona kumbe Serikali ina matumizi ya hovyo ambayo hata huyo Magufuli aliendelea nayo hadi sasa Samia ndio anakuja kuyapunguza

Mojawapo ya lililonishtua ni kuwa Mkurugenzi au Katibu Mkuu akitumbuliwa bado anaendelea kulipwa mshahara uleule aliokuwa nao, akasema kuwa inawezekana hata ukakuta kuna wizara 15 tu lakini ukakuta kuna watu 50 wanalipwa mshahara wa katibu mkuu, ama kuna halmashauri 100 lakini wanaolipwa kama wakurugenzi ni 500.

Aisee
Ndio maana hawatako ccm itoke madarakani sio bure ti
 
Kwa hiyo wale makatibu wakuu wote waliobadilishwa baada ya kuingia awamu mpya bado wanaokea mshahara ule ule?? angalia vizuri taarifa zako kabla ya kutoa maoni
 
Itoshe kusema , Magufuli alikuwa raisi bora Baada ya Nyerere.

Kuchafuliwa kwa noti , hakuipunguzii thamani
Kweli alikua bora maana hakuajiri mtu, akuongeza mishahara alikopa mikopo ya riba kubwa about 30% y a mikopo yake yote, alianzisha miradi mikubwa aliyoiacha ikiwa imefikia 10% tu, Ni rais aliyeogopa kusafiri kwenda kunegotiate na wenziwe,
N. B, Ubora wa kiongozi Bora yoyote duniani ni kuweza kutoa ajira kubuni ajira na it's citizen welfare, healthy an alike.
 
Ili jambo la kuwalipa kulingana na vyeo ata ukitolewa kazini lilikuwapo kabla ata ya serikali ya awamu ya tano.

Sema ni jambo jema maana mtu anakaa nyumbani bila kufanya kazi huku anaendelea vuta mshahara mnene
Hakuna mtu anayelipwa mshahara bila kufanya kazi
 
..lakini sheria huwa haigusi waliohusika kabla haijabadilishwa.

..watu walikuwa wanashangilia Jpm anavyotumbua watu serikalini, kumbe mwisho wake ni watu hao kulipwa mishahara bila kufanya kazi.
Siyo wote walikuwa hawafanyi kazi. Asilimia kubwa (more than 90%) walikuwa wanarudi kwenye kazi walizokuwa wanafanya kabla ya uteuzi.
 
Kati ya vitu ambavyo Magufuli alikuwa akiimbwa navyo ni kubana matumizi ya Serikali

Ila leo baada ya kumsikiliza Mwigulu akiweka mikakati mipya ya kubana matumizi, nimeona kumbe Serikali ina matumizi ya hovyo ambayo hata huyo Magufuli aliendelea nayo hadi sasa Samia ndio anakuja kuyapunguza

Mojawapo ya lililonishtua ni kuwa Mkurugenzi au Katibu Mkuu akitumbuliwa bado anaendelea kulipwa mshahara uleule aliokuwa nao, akasema kuwa inawezekana hata ukakuta kuna wizara 15 tu lakini ukakuta kuna watu 50 wanalipwa mshahara wa katibu mkuu, ama kuna halmashauri 100 lakini wanaolipwa kama wakurugenzi ni 500.

Aisee
Mkuu Johnny Sack , kumbe hili wewe ndio umelijua jana!, karibu angalia tarehe ya bandiko hili uone watu tulisema nini na lini
Nilisema
Wanabodi,
  1. Maofisa Kuwekwa Pembeni Kusubiri Kupangiwa Kazi Nyingine. Mfano wanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa ku boost political mileage yake, na hivi ndivyo wafanyavyo ma populist leaders dunia nzima, boosting their political mileage tuu ila kiuchumi inatuumiza na kuliumiza taifa!. Magufuli analibebesha taifa hili mzigo mkubwa wa gharama kuliko hata serikali ya JK!. Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote zile, anaendelea kulipwa mshahara wake wote ule ule kamili, bali marupurupu ndio yanaondolewa!. Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo tuu atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa kabisa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!. Tangu rais Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa kazi, wala aliyeshitakiwa, wote wamesimamishwa tuu kazi na kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, au wengine teuzi zao zimetenguliwa huku wote wakiendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.
  2. Makatibu Wakuu Wanaolipwa Bila Kazi!. Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale Makatibu Wakuu wote ambao Ukatibu wao Mkuu haukutenguliwa, au wameachwa tuu bila kupangiwa kazi nyingine yoyote, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ya makatibu wakuu kusubiria ama kupangiwa kazi nyingine, ama kustaafu kwa umri, au kustaafishwa kwa manufaa ya umma, lakini wakati huu wote wanaosubiria, walalipwa na kupatiwa haki na stahiki zote za level ya Katibu Mkuu!.
Hitimisho
Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema kabisa, zikiachwa tuu hivi hivi jinsi hii hii inavyo fanyika, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora rais Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu au kustaafisha kwa manufaa ya umma!. Anapounda baraza jipya na kuteua makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walipaswa kustaafishwa there and then na mishahara yao inasimamishwa kuanzia pale pale walipostaafishwa!.

Hili ninalolisema leo, wengine mtakuja kuliona mwezi Juni /July wakati wa kusomwa kwa bajeti kuu ya serikali, mtashuhudia kuongezeka kwa bajeti ya uendeshaji wa serikali ikiwemo wage bill badala ya kupungua na mbele ya safari mtashuhudia mabadiliko mengi ya baraza za mawaziri au kwa kuwaongeza, au kuzipunguza vizara alizoziunganisha kwa kuziachanisha!. Na kila siku mawaziri watateuliwa na kutumbuliwa kama kubadili nguo, kwa sababu Magufuli huyu ambaye sasa ndie rais wetu, ni Magufuli huyu huyu niliyemzungumza hapa

Happy New Year
Paskali.
Rejea
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

Jee Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?- Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?.

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

P
P.
 
Kati ya vitu ambavyo Magufuli alikuwa akiimbwa navyo ni kubana matumizi ya Serikali

Ila leo baada ya kumsikiliza Mwigulu akiweka mikakati mipya ya kubana matumizi, nimeona kumbe Serikali ina matumizi ya hovyo ambayo hata huyo Magufuli aliendelea nayo hadi sasa Samia ndio anakuja kuyapunguza

Mojawapo ya lililonishtua ni kuwa Mkurugenzi au Katibu Mkuu akitumbuliwa bado anaendelea kulipwa mshahara uleule aliokuwa nao, akasema kuwa inawezekana hata ukakuta kuna wizara 15 tu lakini ukakuta kuna watu 50 wanalipwa mshahara wa katibu mkuu, ama kuna halmashauri 100 lakini wanaolipwa kama wakurugenzi ni 500.

Aisee
Hili tulishasema sn mkuu miaka ya 2017-2020 sema labda ulikuwa bado hujawa member
 
Back
Top Bottom