Wanabodi,
- Maofisa Kuwekwa Pembeni Kusubiri Kupangiwa Kazi Nyingine. Mfano wanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa ku boost political mileage yake, na hivi ndivyo wafanyavyo ma populist leaders dunia nzima, boosting their political mileage tuu ila kiuchumi inatuumiza na kuliumiza taifa!. Magufuli analibebesha taifa hili mzigo mkubwa wa gharama kuliko hata serikali ya JK!. Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote zile, anaendelea kulipwa mshahara wake wote ule ule kamili, bali marupurupu ndio yanaondolewa!. Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo tuu atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa kabisa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!. Tangu rais Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa kazi, wala aliyeshitakiwa, wote wamesimamishwa tuu kazi na kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, au wengine teuzi zao zimetenguliwa huku wote wakiendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.
- Makatibu Wakuu Wanaolipwa Bila Kazi!. Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale Makatibu Wakuu wote ambao Ukatibu wao Mkuu haukutenguliwa, au wameachwa tuu bila kupangiwa kazi nyingine yoyote, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ya makatibu wakuu kusubiria ama kupangiwa kazi nyingine, ama kustaafu kwa umri, au kustaafishwa kwa manufaa ya umma, lakini wakati huu wote wanaosubiria, walalipwa na kupatiwa haki na stahiki zote za level ya Katibu Mkuu!.
Hitimisho
Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema kabisa, zikiachwa tuu hivi hivi jinsi hii hii inavyo fanyika, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora rais Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu au kustaafisha kwa manufaa ya umma!. Anapounda baraza jipya na kuteua makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walipaswa kustaafishwa there and then na mishahara yao inasimamishwa kuanzia pale pale walipostaafishwa!.
Hili ninalolisema leo, wengine mtakuja kuliona mwezi Juni /July wakati wa kusomwa kwa bajeti kuu ya serikali, mtashuhudia kuongezeka kwa bajeti ya uendeshaji wa serikali ikiwemo wage bill badala ya kupungua na mbele ya safari mtashuhudia mabadiliko mengi ya baraza za mawaziri au kwa kuwaongeza, au kuzipunguza vizara alizoziunganisha kwa kuziachanisha!. Na kila siku mawaziri watateuliwa na kutumbuliwa kama kubadili nguo, kwa sababu Magufuli huyu ambaye sasa ndie rais wetu, ni Magufuli huyu huyu niliyemzungumza hapa
Wanabodi, Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha...
Happy New Year
Paskali.
Rejea
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.
Jee Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?- Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?.
Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!
P