Benki ya Barclays naipenda ila nina wasiwasi fulani. Kuna kipindi baadhi ya wafanyakazi wake walivuta mamilioni ya mihela na wakakamatwa. Pia kumekuwa na manun'gunikonun'guniko kwa baadhi ya wateja waliochukua mkopo kutoka benki hii. Nilidhani watu wanaongeza chumvi lakini hili la makao makuu ya Barclays Uingereza benki 'kuwaibia' wateja ndilo limenifumbua macho - kumbe benki hii ina matatizo na inawezekana hata hapa kwetu wateja 'wanaibiwa'. Yaani, ni matatizo toka juu hadi chini au toka North to South. Naomba benki irekebishe kasoro zilizopo ili kujenga imani kwa wateja wake.