Kumbe uozo wa Benki ya Barclays uko hata Ulaya?

Kumbe uozo wa Benki ya Barclays uko hata Ulaya?

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Posts
5,602
Reaction score
3,845
Benki ya Barclays naipenda ila nina wasiwasi fulani. Kuna kipindi baadhi ya wafanyakazi wake walivuta mamilioni ya mihela na wakakamatwa. Pia kumekuwa na manun'gunikonun'guniko kwa baadhi ya wateja waliochukua mkopo kutoka benki hii. Skendo iliyotokea makao makuu ya Barclays Uingereza benki 'kuwaibia' wateja ndilo limenichanganya. Naomba benki irekebishe kasoro zilizopo ili kujenga imani kwa wateja wake.
 
Ungesema hayo matatizo yao ndo ingekuwa vizuri, watu wangepata pakuanzia kuchangia.
 
Benki ya Barclays naipenda ila nina wasiwasi fulani. Kuna kipindi baadhi ya wafanyakazi wake walivuta mamilioni ya mihela na wakakamatwa. Pia kumekuwa na manun'gunikonun'guniko kwa baadhi ya wateja waliochukua mkopo kutoka benki hii. Nilidhani watu wanaongeza chumvi lakini hili la makao makuu ya Barclays Uingereza benki 'kuwaibia' wateja ndilo limenifumbua macho - kumbe benki hii ina matatizo na inawezekana hata hapa kwetu wateja 'wanaibiwa'. Yaani, ni matatizo toka juu hadi chini au toka North to South. Naomba benki irekebishe kasoro zilizopo ili kujenga imani kwa wateja wake.
1. Kuna manun'guniko ya charges2. Wengine wanadai ukichukua mkopo na kumaliza marejesho wanaendelea kukukata3. Matatizo niliyolenga hasa ni hayo ya UK na huku kwetu nimesema inawezekana yapo pia. Kwa mantiki kwamba kama yanafanyika kule ambako kuna efficiency kubwa, je kwetu huku haiwezikani? Ni tahadhari. Kama yapo yarekebishwe na kama hayapo benki iendelee kuboresha huduma.4. Pale makao makuu (DSM) wanaweka tellers wachache, ukienda unapoteza muda mwingi kwa kitu ambacho kingemalizika ndani ya dakika chache.
 
ni KWELI kabisa! Barclays ni wezi sana! Mie nilishawahi kuibiwa huku Arusha, nikawahama!
 
Kwani Ulaya Mbinguni...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mie hadi sasa nahangaika yaani nilishamaliza mkopo lakini wanaendelea kukata kila mwezi! nawahama
 
Back
Top Bottom