Benki ya Barclays naipenda ila nina wasiwasi fulani. Kuna kipindi baadhi ya wafanyakazi wake walivuta mamilioni ya mihela na wakakamatwa. Pia kumekuwa na manun'gunikonun'guniko kwa baadhi ya wateja waliochukua mkopo kutoka benki hii. Skendo iliyotokea makao makuu ya Barclays Uingereza benki 'kuwaibia' wateja ndilo limenichanganya. Naomba benki irekebishe kasoro zilizopo ili kujenga imani kwa wateja wake.