Kumbe wanawake walianza kusuka nywele za rasta miaka 3,300 iliyopita

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,378
Reaction score
3,383

Ugunduzi huu utaondoa yale masimango tunayoyapata wanawake pale tunaosuka rasta (Hair Extention) au kuweka weave.

Ni kwamba hivi karibuni watafiti katika mji mpya unaojengwa huko nchini Misri wa Amarna wamegundua mabaki ya mwili wa mwanamke aliyezikwa miaka 3,300 iliyopita ambapo fuvu lake lilikutwa likiwa limesukwa kwa nywele bandia maarufu kama rasta siku hizi.

Mwili wa mwanamke huyo haukuwa umehifadhiwa kwenye kasha maalum walilokuwa wakitumia Wamisri wa kale kuhifadhi mwili wa mtu aliyekufa, bali ulikuwa umeviringishwa kwenye mkeka.

Sasa nimeamini kwamba, kumbe haya mambo ni kama yanajirudia, urembo kwa wanawake ulianza miaka dahari iliopita, lakini siku hizi tukipendeza wanaume maneno yanawatoka hawana hata simile wakati urembo ulikuwepo tangu Enzi na Enzi.

http://www.livescience.com/47875-ancient-egyptian-woman-with-hair-extensions.html

Rasta zilikuwepo miaka mingi sana nyuma. Zaidi ya hiyo miaka 3300 ulioitaja. Kumbuka Samson,mwamuzi wa Israel,aliyesalitiwa na mwanamke Delilah na anbaye aliwasumbua sana wafilistine. Alikua na rasta toka utoto wake.
 
Ukweli ni kwamba huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo. Lakini swali la kujiuliza ni je miaka hiyo kulikuwa na viwanda au kiwanda cha kutengeneza rasta? (snythetic hair). Mimi nafikiri kama hiyo picha ya fuvu ni ya ukweli basi hizo nywele ni nywele zake original na siyo rasta.
 
labda jipya lije liwe mwanadamu kuzuia kifo kisitokee kabisa/yani mtu asikate roho...
mengineyo machache sana ndo mapya!
 
Rasta zilikuwepo miaka mingi sana nyuma. Zaidi ya hiyo miaka 3300 ulioitaja. Kumbuka Samson,mwamuzi wa Israel,aliyesalitiwa na mwanamke Delilah na anbaye aliwasumbua sana wafilistine. Alikua na rasta toka utoto wake.

Nakubaliana na wewe mkuu,lakini usiseme au usiite rasta…nafikiri useme style ya misuko ya rasta ilikuwepo toka enzi hizo za wakina Delilah na Cleopatra…hawa enzi hizo walifuga nywele zao za asili na wakazisuka au kuzisokota style ya msuko kama wa rasta. kumbuka rasta ni aina ya nywele (snythetic hair) inayotengenezwa viwandani na kazi yake maalumu ni kusukia mitindo tofauti tofauti ya nywele…kuna rasta za Darling,Angel, Abuja na Prima.
 
Rasta zilikuwepo miaka mingi sana nyuma. Zaidi ya hiyo miaka 3300 ulioitaja. Kumbuka Samson,mwamuzi wa Israel,aliyesalitiwa na mwanamke Delilah na anbaye aliwasumbua sana wafilistine. Alikua na rasta toka utoto wake.

Alikuwa na rasta za bandia????
 
hii habari ni mpya na nimefurahi sana kuijua! rasta tangu miaka 3300 iliyopita!safi sana.
 
mkuu hiizo ni rasta na sio nyele za bandia.... hapa tunaongelea matumizi ya nywele za asili sio nywele zilizokuwa imported kama tunazotumia kufunikia vipilipili vyetu waafrica! kwa nini tusijivunie tulivyoooooooo!
 
Hakuna jipya kwa sasa twafanya marudio bali yapo modified zaidi ila yote yalishafanyoka huko nyuma
 
mkuu hiizo ni rasta na sio nyele za bandia.... hapa tunaongelea matumizi ya nywele za asili sio nywele zilizokuwa imported kama tunazotumia kufunikia vipilipili vyetu waafrica! kwa nini tusijivunie tulivyoooooooo!

Basi kama ni hivyo huo msuko unaitwa MABUTU STYLE na siyo rasta style. Kumbuka ukiwa na nywele ndefu za asili unaweza kusuka mabutu na ukinunuwa rasta kutoka dukani unaweza pia kusuka mabutu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…