Hebu nisaidiwe hapa.....ninavyofahamu mimi ni "Uma" na si "Umma".....Ile ya kwanza ni chombo kwa matumizi ya nyumbani na hii ya pili ni ile tunayotumia kumaanisha kundi la watu mfano umma wa watanzania.
Au nimekosea? Kama ni hii ya pili yaani "Umma" basi wingi wake ni "Umma" na ile ya Kwanza "Uma" wingi wake ndio "Nyuma".......
Naombwa kurekebishwa kama nakosea ili nisiendelee kukosea kwa kuwaza niko sahihi............
Dada wa chipsi, naomba niletee na nyuma maana mie chipsi bila nyuma ngumu kushuka...........hahahaa, lol