#COVID19 Kumbe Zanzibar imepata Tsh 200 bilioni tu katika ule mkopo wa COVID tofauti na inavyoelezwa na Wanasiasa uchwara!

#COVID19 Kumbe Zanzibar imepata Tsh 200 bilioni tu katika ule mkopo wa COVID tofauti na inavyoelezwa na Wanasiasa uchwara!

Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr Sada Mkuya amesema wamepokea dolla milioni 100 za kimarekani sawa na tsh billion 200 na ushee ambazo zitatumika kuimarisha miundombinu.

Dr Mkuya amesema watajenga madarasa na hospitali katika wilaya zote Unguja na Pemba.

Mapinduzi Daima!
Wewe umejuaje kuwa wamepokea hizi pekee?
 
Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr Sada Mkuya amesema wamepokea dolla milioni 100 za kimarekani sawa na tsh billion 200 na ushee ambazo zitatumika kuimarisha miundombinu.

Dr Mkuya amesema watajenga madarasa na hospitali katika wilaya zote Unguja na Pemba.

Mapinduzi Daima!
Sasa Zanzibar peke yake bil.200, Dar Es Salaam yenye watu mil. 6 imepata kiasi gani?
 
Zanzibar inapata mgao kama nchi.

Hapana uwiano uliona wapi muungano ambao wao wana uraia pacha yaani wakiwa kwao hujiita wazanzibar na wakiwa huku hujiita watanzanai kinafiki ili kutupumbaza, hakuna usawa hapo Tanganyika ina watu milioni karibu 60 , wao wako milioni moja na laki tano lakini tunawahudumia msidhani hatuoni kwa uchumi upi walionao watalipa hiyo bilioni 200 wakati bajeti yao hawatengi pesa kulipa mikopo ya nje
 
Bora ya Chato; kwani iko Tanganyika, Chato wanachangia mfuko mkuu wa hazina (through kodi ya TRA) lakini kinachokusanywa Zanzibar hubaki Zanzibar
Hata hicho kinachokusanywa na hiyo Chato international Airport kinachangia maendeleo ya zenji
 
Ukiangalia ukubwa wa Zanzibar na Tanganyika uwiano huo unaziona kidogo hizo?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Bilioni 200 kwa Zanzibar pekee ni hela nyingi mno

Kwa upande wa Tanzania bara mkoa moja unapata average ya Bilioni 15

Kwa hizo Bilioni 200 kwa Tanzania bara ingepata mikoa takribani 10
 
Back
Top Bottom