G
guest-1787677623
Guest
Hii ni kumbukizi ambayo natamani kusherehekea nanyi wana JF. Hili ni tukio binafsi lililonikuta miaka 15 iliyopita. Nitasimulia kwa ufupi nanyi mjifunze kitu, pia hata kama utakuwa unanifahanu au urahisi mi ni nani, acha haya mambo hukuhuku mtandaoni.
Nikiwa nimemaliza chuo kikuu kimoja hapa Tanzania, nilipata kazi kwenye kambi ya wakimbizi mkoa mmoja hapa Tanzania. Kambi hiyo ipo nje ya mji yalipo makao makuu ya huo mkoa nilipokuwa nafanya kazi za UNHCR hivyo nilipanga nyumba mjini na wakati mwingine tunalala huko kambini.
Tukiwa mjini, kuna mahali nilikuwa nakula kila siku jioni na kuangalia mechi za EPL kwenye ukumbi mmoja maarufu hapo town kwa ajili ya kuonesha Mpira.
Pale nilipokuwa nakula kulikuwa na binti mmoja mhudumu wa chakula, nikavutiwa naye nikawa napiga hapo kimya kimya. Nikanogewa na kuanza kupiga peku, mwishowe naambiwa ana mimba yangu.
Sikupata nikatunza Mimba, tukapata mtoto wa kike ambaye ni copyright na mimi. Sikumkataa nikaamua kumvuta na kuishi naye mtoto alipofunga miezi miwili ili turehe mtoto wetu.
Baada ya miezi 6, mzee wangu akaona sio vyema tukae bila kulipia Mali wala kujitambulisha. Akafunga safari na kuja ninapoishi. Ikaandaliwa siku ambayo wahenga wangeenda pamoja na baba na mimi kwa ajili ya kujitambulisha na kumaliza kila kitu.
Siku ikawadia tukaenda ukweli baada ya washenga kutangulia siku 1 kabla tukiwa tumebeba vitu hitajika. Zoezi lilienda vizuri, tukamaliza tukio salama so mi nikarudi kwangu na mzee akaondoka asubuhi ya kesho kurudi nyumbani.
Nilipomfikisha mzee stendi na kuondoka, nikaanza kuumwa tumbo ile Mbaya. Tumbo liliuma huku nikiwa naharisha wakati sikuwa nimekula chakula zaidi ya kile tulichokula ukweni. Nikampigia mzee wangu kumuulizia anasema yeye hana changamoto yoyote. Nikawapigia wale washenga nao hawana changamoto yoyote.
Kufika saa 4, hali ikawa tete. Nikawapigia simu jamaa wakanipeleka hospitali kwani nilikuwa naumwa tumbo, naharisha na kutapika sana. Pale Hospitali wakanipa dawa na kuniwekea dripu baada ya vipimo vyao. Hali ikatulia na nikalazwa pale siku ya kwanza.
Siku ya pili niliamka salama na jamaa pamoja na mke na nduguze wakaja kuniona na nilishinda salama. Ilipofika saa 12 jioni nikiwa na dereva wa shirika aliyekuja kuniona, nikakumbuka kauli moja niliongeaga naye siku 1 kwa utani kuwa "Mi nikifa, msije weka jeneza langu na kulifunga juu ya carrier ya gari kwani nitakunja miguu na gari halitaenda "
Ghafla, nikaanza kuona mawenge na nikawa kama naweweseka, moyo ukawa unapiga kwa nguvu mpaka unausikia ukipiga pa, pa, pa. Dereva akashtuka, akamuita Dr. Dr alinipima pale, akasema Pressure imepanda ghafla na sukari kushuka ghafla. Sikuwahi kiwa na shida ya pressure wala sukari wala sijui vipimo vyake vinapimwaje. Ndio mara yangu ya kwanza kukutwa na hilo tatizo ila lilikiwa ghafla. Nikawa naweweseka na kupiga kelele kuwa nakufa. Nikaanza kuomba toba kwa wale niliowakosea hapa duniani huku nalia.
Kiukweli, sijui ilikuwaje. Nikajikuta nakemea na kuikataa ile Roho ya Mauti kipindi jamaa wamenishika mikono na miguu kwa kunituliza pale kitandani kwa kusema "KWA JINA LA YESU SIFI BALI NITAISHI KUTANGAZA MATENDO MAKUU YA MUNGU ALIYONITENDEA"
Kipindi hiko, sikuwa nasali wala kwenda kanisani japo nimekulia kwenye malezi ya Kilutheri kwani wazazi wangu walikuwa Walutheri. Dunia ilinimeza sana na sikuwa naamini wala muamini Mungu tokana na mahangaiko ya ujana.
Baada ya kukemea hali, nikatulia na hali ya kuweweseka na kuona maruweruwe ikiisha ghafla. Baada ya lisaa limoja nikawa sawa. Nikalala hapo na kesho asubuhi wakaniruhusu niondoke kurudi nyumbani kwani sikuonekana tena na tatizo lolote.
Nimeona nishare nanyi hiki kitu kilichonitokeaga miaka 15 iliyopita. Shida ilikuwa nini, nitaeleza siku nyingine.