Ukiweka ahadi lazima uitimize..Ukiweka nadhiri ni lazima uitangue la sivyo itakutesa kifikra na kudai utanguzi.
Mwaka wa jana kwenye post moja, tukiwa na mjadala, tulimjadili gwiji wa falsafa maizi Hayati Munga Tehnan na nikaahidi kuna na mada maalum kwa ajili yake kumuenzi. Naomba sasa nitangue nadhiri na ahadi yangu hii kupitia mada hii.
Kwa wengi wasiomfahamu ndio alikuwa Mmiliki wa gazeti la utambuzi liitwalo JITAMBUE na MSHAURI. Humo ndani kulijaa madini tupu ya falsafa kindakindaki, saikolijia, mambo ya kiroho kijamii hata utani na simulizi za kufurahisha sana.
Mimi ni mmoja wa shabiki na mwanafunzi wake mkubwa... Wengine ninaoweza kuwakumbuka kwa haraka ni
pasco na
Mtambuzi ..Natambua list ni ndefu na kila mmoja atakuja na mchango wake
Uzi utakuwa updated kutokana na kadiri maudhui yatakavyokuwa yanapatikana ili hatimaye tuwe na mada iliyoshiba kumhusu Munga Tehnan.
Naamini kati yetu kuna wanaojua historia yake, maana mtandaoni haupatikani.
Ombi kwa
Moderator Kama kuna uwezekano wa kuziweka mada zake pamoja kwenye mada moja kuu, zile zenye maudhui ya kufanana.
Ombi kwa wana JF kama kuna mwenye hard copy ya kazi zake kupitia JITAMBUE pls share.