KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

Namkumbuka Marehemu kuna Warsha/Semina au maonyesho ya watu ambao hawatumii nyama yalifanyika Diamond Jubilee miaka hiyo na nikiwa kijana mdogo nami nilienda hapo , pia kukiwa na mapishi mbalimbali ya Vegans & Vegetarians

Nikapata wasaa wa kuongea na Munga na bahati mbaya kwangu ni mimi ndo alinipa nafasi ya kunisikiliza zaidi kuliko yeye kujieleza ( anyway nafikiri ni ujana wangu na ujuaji na kuwa na taarifa nyingi bila mpangilio [emoji23]) japokuwa nilipaswa mimi kumsikiliza zaidi sababu nilikuja kugundua baadae nilikuwa naongea na Nguli wa Elimu ya utambuzi

Nafikiri alitaka sana kujua kutoka kwangu ilikuwaje nikawa nina shauku ya kutaka kujua mambo ambayo kwa mtizamo wa kawaida na wa kijamii sikuwa naonekana kama nita kuwa nina ufahamu wa hiyo Dunia, kwanza nilikuwa naonekana bwana mdogo mdogo sana kwa umri afu pia na kwa mtizamo wa nje nilikuwa nina ule muonekano wa wale vijana wa mjini mjini hivi

Nikamuambia mambo ya Mantra, meditation ya pumzi nayo fanya pia moja ya vitabu vilivyonipa hamasa kuanza kuutafuta ukweli kutoka ndani yangu, na kimoja ya hivyo vitabu ni kitabu nilichonunua tu randomly kwenye zile ‘corridors’ za posta mpya wanao panga panga chini vitabu ambavyo vingi vimechakaa chakaa cha mwana dada wa kimarekani kama sikosei na jina lake Shirley MacLaine/ Maclain (Kama sijakosea jina) na jina la kitabu ni ‘ Going Within’

Kipindi hicho tunaongea bado nilikuwa sijaanza rasmi kujitafuta zaidi ya kusoma vitabu mbalimbali vya utambuzi na meditation ya pumzi na ya maneno ( Mantra)


Baadae sana ndo nikaanza kufuatilia Magazeti ya Jitambue yalivyo anza kutoka na nikaanza kuujua ukubwa wa Nguli Tehenan

Ni mmoja wa watu/wana habari ambao walikuja ki tofauti zaidi na alijitahidi kuleta uelewa mkubwa kumuhusu binaadam na nguvu alizonazo za kuweza kuumba na kuharibu ( ambazo kila mtu anazo ni namna ya kuzijua na ku tap hiyo energy iliyo ndani ya kila mmoja wetu) na kujua kwamba ni binaadam anaweza umba/ tengeneza hatima na majaliwa yake

Pia nilisikia pia nae alikuwa influenced na mtu mmoja anaitwa Rashid Mbughuni ( sina uhakika na jina na hiyo tetesi) maana sikuwa karibu sana na Munga zaidi ya siku hiyo na sijakutana nae tena mpaka niliposikia amefariki na niliomboleza kimya kimya kuondokewa na mtu mkubwa ktk ngazi ya ufahamu

RIP Munga Tehenani

Asante sana Mshana Jr kutuletea kumbukizi tena ya huyu mwamba na tusherehekee Maisha yake na jitihada zake za kutaka tuujue ukubwa wetu, Barikiwa sana
 
Mtaalam na mwalimu wa Utambuzi Munga Tehenan alifariki tarehe 5 Mei 2008 na kuzikwa pale makaburi ya Kisutu. Siku chache kabla ya kufariki aliandika makala isemayo 'HII NI MAITI YA NANI?'. Hii ilikuwa kama utabiri wa kitakachotokea na kwa waliokuwepo msibani wanaelewa kuwa kulitokea kama makala ilivyoeleza

HII MAITI NI YA NANI?
Nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari, niliwahi kushuhudia mwili wa mwanafunzi mwenzetu ukigombewa na wazazi wake. Huyu mwanafunzi mwenzetu alifariki ghafla shuleni na ikabidi wazazi wake wafahamishwe ili waseme maiti isafirishwe kwenda wapi.Mama alisema, maiti ya mwanaye ibaki hapo alipofia, kwani atakuja kuichukua na kuisafirisha kuipeleka kwao (mama) kwa mazishi. Baba naye alisema hivyo hivyo. Walimu wakaamini kwamba, baba na mama wanazungumza jambo lilelile. Lakini walipowasili pale shuleni, ndipo walipogundua kwamba, hawakuwa wanawasiliana na watu walio pamoja.Baba alikuwa na dini nyingine na mama alikuwa wa dini nyingine na walishaachana kitambo.

Tangu walipoachana wazazi hawa, kila mmoja akawa anamvutia mtoto aingie au afuate dini yake. Kwa jinsi tulivyokuwa tunamfahamu marehemu, hakuwa hasa mtu wa dini fulani. Wakati wa vipindi vya dini, huyu mwenzetu alikuwa anaingia mara kwenye madarasa ya waislamu, mara wakristo na alikuwa anaingia kwenye madhehebu mbalimbali.Basi, wazazi hawa walikuwa kila mmoja akitaka kuchukua mwili wa marehemu. Kila mmoja alikuwa akitoa maelezo ni kwa nini yeye ndiye anayestahili kumzika mtoto kwa dini yake. Malumbano haya yalikuwa makubwa mpaka vyombo vya dola vikahusishwa. Nakumbuka alikuja afisa mmoja wa upelelezi kwenye malumbano hayo. Katika kujaribu kutafuta muafaka, afisa huyu alizungumza kama vile kwa kuhutubia akisema: Inasikitisha kwamba, kijana wetu mpendwa, anaingizwa kwemye choyo na ubabe wa kuoneshana nani zaidi, katika hali hii ambapo hawezi kujitetea.

Naamini, huyu marehemu kwa sasa anawachukia wazazi wake wote, kwani anajua wazi hakuna anayempenda hata mmoja, bali wanatumia kifo chake kama uwanja tu wa mapambano ya kujitosha kwao.Naamini, hivi sasa marehemu angeombwa kuchagua rafiki na ndugu wa kweli, angechagua wanafunzi wenzake na walimu wa dini. Hii inatokana na ukweli kwamba, hawa hawakutaka kumpangia aabudu au kuifuata imani gani ya dini. Tunaambiwa aliingia kwa waislamu, na aliingia kwa wakristo pia, hakuzuiwa au kusemewa, alikuwa huru.

Kuwa na dini ni kuwa na uhuru. Kuwa na dini ni kuwapa wengine uhuru wa kuwa wao. Kuwa na dini siyo kutumia tatizo la mwingine kujifaharisha, kuonesha ubabe na urijali ulionao. Hiyo ni kibri ambayo kwa mtu aliyepoteza mwili kama huyu kijana wetu anaiona na kuijua vizuri, haipendi hali hii..Hotuba hiyo ilisaidia sana, kwani hatimaye ndugu wa upande wa mama na wale wa upade wa baba walikaa chini wakiwa na adabu mpya na kujadili. Hatimaye walikubaliana kijana azikwe kwa dini ya mama yake.

Miaka 30 baadaye, nakutana tena na watu wanaogombea maiti, watu wanaoamini kwamba mzoga wa binadamu una maana yoyote. Sijawahi kuona mtu akitoa shati au gauni kwenye mfuko wa nailoni na kuvaa mfuko huo badala ya kuvaa shati au gauni, nimesema sijawahi kuona, huko ni kujidanganya. Nimekuwa nikiona sana jambo hilo, ambapo ni pale watu wanapogombea mwili.Inaonesha wazi kwamba, binadamu. bado ni mjinga sana juu ya maisha yake.

Mwili, mwili ni nini, na hadi wapi? Kama mwili ungekuwa na maana sana, baada ya mtu kufariki usingekimbizwa mochuari, usingepakwa asali au usingechomwa sindano ili usiharibike na kuleta usumbufu wa harufu na maradhi. Mwili siyo mimi wala wewe. Mwili haujawahi kuwa mwenye mwili na hautakuja kuwa. Mwili ni kama tochi tu, ambayo umeiazima ili iweze kukusaidia kufika kijiji cha pili, kutokana na giza na njia ya uchochoro ambayo unatakiwa kuipita ili kufika kijiji hicho cha pili. Mwili ni kifaa na siyo wewe, bali wewe unakitumia kifaa hicho Binadamu anajibainisha kwenye maisha haya ya hapa duniani kupitia mwili wake, lakini yeye siyo mwili. Mwili ni ubainisho, ni chombo cha kutumika kwa kusudi la kidunia tu. Baada ya muda mwili hukoma kuwepo, hujimaliza wenyewe au kumalizwa, ili binadamu amudu kuingia hatua nyingine ya maisha ambayo haitumii au haihitaji mwili.

Tangu ulipozaliwa umeoneshwa na kufundishwa kwamba, wewe ni mwili kwa njia zote. Akili yako imeshika kutu kwa kuamini kwamba, mwili ni wewe na wewe ni mwili. Huna uwezo tena wa kuuona ukweli, kwa sababu vipimo vyako vyote kuhusu maisha vinaishia kwenye akili, ambayo nayo pia haikuhusu, siyo yako, umepachikwa tu. Kwa ujinga huu wa kutojua mwili ni nini na sisi ni nani, ndipo ambapo tunaingia kwenye ujinga wa kuendeshwa na miili yetu, hisia zetu na akili. Kila mmoja anaamini kwamba, mwili wake ukipotea, ukishindwa kutumika, yaani akifa, basi huo ndiyo mwisho wake. Kama hiyo ni kweli, ina maana binadamu hana maana kabisa, ni upuuzi usiofaa kuelezewa!Yaani binadamu amekuwepo ili awepo kwa mwezi mmoja, miaka kumi, hamsini, sabini, tisini, au mia tu. Halafu baada ya hapo basi. Huu ni uongo mkubwa sana, unaoweza kukubaliwa na akili makapi ya kulishwa tu! Anayetafakari zaidi kidogo, atabaini kwamba, mwili ni mwili tu, ni kasha tu. Ni kasha ambalo muda wake wa kutumika ukiisha mtumiaji au [wewe] analiacha kwa sababu haliwezi kukidhi kile anachokihitaji hapa duniani.

Mtumiaji anachukua kingine ambacho kinakidhi wakati huo [baada ya kifo] . Kwa hiyo, binadamu hafi bali mwili ndiyo unaofikia ukomo wa muda wake wa matumizi kwa sababu mbalimbali.Anapokufa John au Hamisi, haina tofauti. Anapokufa mkulima hohehahe au tajiri kuliko wote duniani, pia haina tofauti. Wote wanapita kwenye hatua muhimu ya mabadiliko, ambapo wanaacha matumizi ya kifaa kilicho kuwa ndicho pekee kinachoweza kuwabainisha na wengine hapa duniani na kuchukua kingine ambacho hakiwezi kuwabainisha tena na wale wenye miili bado. Anapokufa John au Hamisi, haijalishi kama amezikwa kwa jeneza la dhahabu na mizinga 100 au kwa masululu butu na kaniki. Kuzikwa ni utaratibu wa kimazoea wa kuhifadhi mwili ambao sasa ni mzoga tu, ili usisumbue watu wengine kwa harufu na maradhi. Kuzika haina maana kwamba, kunambadili aliyekuwa akitumia mwili huo [marehemu], la hasha.

Kama unadhani kwamba Mungu anahesabu umezikwa na dini gani, umezikwa na shehe au padri gani, ndiyo afanye uamuzi wa kukupokea mbinguni au hapana, ujue unahitaji msaada wa haraka, kama siyo kupelekwa milembe. Ujue hujui chochote ingawa umekuwa ukujidanganya kwamba unajua.Mungu wa kweli hahangaiki na mzoga, bali sisi kwa ufinyu wetu ndiyo tunaodhani kwamba, mizoga au[maiti] hii ina maana. Mara nyingi nimekuwa nikiwaambia jamaa zangu, ‘nikifa, mtaangalia ni mazingira gani ni rahisi kwenu kuutupa au kuuhifadhi mwili wangu. Kwa nini? Kwa sababu, kama sikuwa karibu na Mungu wakati nikiwa na mwili, huo, ukaribu utaletwa leo wakati nimeupoteza mwili huo kwa sababu tu, mwili wangu umezikwa kwa dini ya babu yangu? Ukosefu wa ufahamu wa kiwango kikubwa sana. Kama nilikuwa karibu na Mungu wakati wa uhai wangu, basi hata nikitupwa chooni baada ya kufa, ukaribu huo hautakufa. Mungu hayatazami mambo kama Abdallah Juma au John Maiko! Kwani kuzika hasa ni kitu gani.

Hatuziki watu ili waende mbinguni. Kama ni hivyo, wanaoliwa na wanyama, kuungua na kuteketea kabisa, wao Mbinguni hawatafika? Kama hawatafika, watahukumiwa vipi siku ya mwisho? Mwili hautakiwi Mbinguni, hauna kazi huko, kwani huko siyo makazi ya miili. Mwili unafaa tu duniani Kuna zile jamii ambapo mtu akifa mwili wake huchomwa moto na kuteketezwa kabisa Unadhani hizi jamii hazimjui Mungu kama wewe unavyomjua? Zinamjua, tena pengine vizuri zaidi yako. Lakini, zimeng’amua kwamba, mwili ni kasha tu, likishindwa kufanya kazi, ni sawa na taka nyingine, hutupwa dampo na kuteketezwa kwa moto. Mtu akishauacha mwili wake [kufa] hana tena uhusiano na mwili huo. Mtu huyo anakuwa ameingia kwenye awamu nyingine ya maisha ambayo haihitaji mwili na ambayo haihitaji kujua huo mwili umezikwa na nani na wapi. Ni akili isiosogea ndiyo ambayo inashindwa kufanya mikokotoo midogo kama hii.Ukiona watu wanagombea maiti, jua kwamba, hata kama wamevaa masuti na kubandika digrii zao kwenye kila ukuta, ni watoto wadogo kiufahamu.

Ukiona mtu pia anaacha wosia mrefu wa namna anavyotaka akifa azikwe, naye huyo ni mpujufu tu wa ufahamu. Kwa nini? Unagombea kuuzika mwili wa fulani ili upate kitu gani, ili huyo marehemu naye apate nini? Hata usipouzika, kumbuka kwamba, ameshakufa na ukiuzika, ameshakufa pia. Haifanyi tofauti yoyote kwa kweli. Kama nilivyosema awali, huuziki mwili ili uende Mbinguni kwa sababu mbingu haiko ardhini. Unaufukia ili usisumbue kwa harufu.Ukienda kwenye nchi zenye vita hasa vya wenyewe kwa wenyewe, utagundua kirahisi kwamba, maiti hana maana, maiti ni msumbufu kwa kunuka na kusambaza magonjwa.

Tunazika kwa sababu tuna nafasi ya kuhifadhi mwili kwa heshima na taratibu ambazo zinaonesha kujali mwili wa mwenzetu ambao ulitumika kufanya mema au maovu. Kwenye kizuizi na misukosuko au vita, hakuna anayeweza kukumbuka, siyo kuzika bali hata kufukia maiti. Kila mmoja anafikiria kuendelea kubaki na mwili wake kwanza. Aliyepoteza wake, basi hakuna anayemjali, kwani haina maana kabisa kumjali. Hata aina nyingine za mazishi zinaonesha tu ujinga na utoto wa binadamu. Mazishi ya kifahari yenye kuhusisha majeneza ya dhahabu na vyakula na vinywaji vya bei mbaya. Ni ujinga uliopindukia kwa sababu, inawezekana kabisa marehemu au wanaotoa fedha hizo hawajawahi kumsaidia aliye hai hata kwa chupi ya mguu.

Sasa kusaidia huo mzoga kwa mapambo inaongeza kitu gani? Nimesema unapoona mtu anaacha wosia ili azikwe vipi, wosia ambao wakati mwingine ni kero tupu, ujue huyo naye ni mtoto wa miaka sita, bila kujali anamiliki au amesoma hadi kiwago gani. Ni utoto kwa sababu, unapoacha mwili, siyo kazi yako kusema huo mwili ufanyiwe kitu gani. Waliobaki, wanaweza kuamua kuuchoma mishikaki [kama wanakula watu], wanaweza kuukausha na kuuweka kwa maonesho, wanaweza kuufukia kwenye kijishimo cha futi tano na ukafukuliwa na fisi usiku, na wanaweza kuuzika kwa matarumbeta na sanduku la dhahamu. Ni hiari yao. Ukishauacha mwili huna mamlaka nao tena. Ni wale waliobaki ndiyo wanaolimbuka nao tu.

Nimekuwa nikitazama hii tabia ya kugombea maiti kwa jicho lenye mashaka na ufahamu wa binadamu, hofu zake na ufisadi wa nafsi alionao. Mtu amekufa, wewe unasema nataka nimzike mimi, sawa. Kwani mbona huendi hospitalini ukaulizia maiti ambazo hazina ndugu na kuzichukua ili ukazizike? Wewe si unapenda kuzika na unaamini kumzika mtu kwa dini yako ni jambo kubwa na la maana sana? Pia hospitalini, utapewa maiti nyingi zisizo na ndugu. Ukishazipata zibadili majina na kuziingiza kwenye dini yako kwa mujibu wa utaratibu wa dini yako. Halafu zika! Hiyo huitaki kwa sababu haina maslahi, haina kuonesha ubabe ambao umefundishwa na wazazi, na jamii na pengine hata na dini yako hiyohiyo. Kugombea maiti ni kujiogopa.

Kugombea maiti ni kujitafuta kimakosa. Kugombea maiti ni kutojua dini. Kugombea maiti ni kudhani mtu anaweza kuwa na uhuru wa kuwa mtu mwingine. Kugombea maiti ni kufikiri wewe ni mwili, Kugombea maiti ni njaa ya mali au haja ya kupanda kithamani. Kwa ujumla ni ubabe wa kimtaa zaidi. Mara nyingi imeshatokea, anapookotwa maiti na watu wakaanza kuulizana, jamani maiti hii ni ya nani? Ujue maiti hiyo itazikwa na serikali. Hakuna mtu au kundi la kidini la eneo hilo ambalo litajitokeza kuichukua na kuizika maiti hiyo kwa imani yake. Hilo haliwezekani kwa sababu halina utamu.

Halina kubishana, halina kulumbana, halina ujuaji na ubabe. Anasubiriwa mtoto mwenye mzazi walioachana na walio na dini tofauti. Huyu akifa, hasira na visasi vyote vya nyuma vinaishia kwenye mwili wake. Atasubiliwa yule ambaye alishakuwa kwenye dini yetu akatoka, huyo akifatuna sababu ya kugombea maiti. Kama nilivyosema, hapo kuna malumbano na ujuaji na kuoneshana. Halafu bado mnajiita mnatumikia dini, zipi? Ni ujinga tu.

Rest in Peace, Munga Tehenan.
Hakika ipo miamba ambayo ilifanikiwa kutimiza malengo yao katika makasha waliyopewa na sasa wameenda kutumika katika Ulimwengu mwingine...

Mbele yetu nyuma yako Mzee Munga
 
Habarini wapendwa poleni na msiba mkubwa wa kitaifa na misiba mingine ya ndugu jamaa na marafiki, ... Hongereni pia kwa sikukuu ya pasaka
Bado nakumbuka ahadi yangu kwenu ya kupata kazi za Munga na kuzirudufu kwa manufaa ya wengi.. Nitaendelea kuwapa updates hapa hapa kwenye hii mada yetu

SIJAWASAHAU....[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Ukiweka ahadi lazima uitimize..Ukiweka nadhiri ni lazima uitangue la sivyo itakutesa kifikra na kudai utanguzi.

Mwaka wa jana kwenye post moja, tukiwa na mjadala, tulimjadili gwiji wa falsafa maizi Hayati Munga Tehnan na nikaahidi kuna na mada maalum kwa ajili yake kumuenzi. Naomba sasa nitangue nadhiri na ahadi yangu hii kupitia mada hii.

Kwa wengi wasiomfahamu ndio alikuwa Mmiliki wa gazeti la utambuzi liitwalo JITAMBUE na MSHAURI. Humo ndani kulijaa madini tupu ya falsafa kindakindaki, saikolijia, mambo ya kiroho kijamii hata utani na simulizi za kufurahisha sana.

Mimi ni mmoja wa shabiki na mwanafunzi wake mkubwa... Wengine ninaoweza kuwakumbuka kwa haraka ni pasco na Mtambuzi ..Natambua list ni ndefu na kila mmoja atakuja na mchango wake

Uzi utakuwa updated kutokana na kadiri maudhui yatakavyokuwa yanapatikana ili hatimaye tuwe na mada iliyoshiba kumhusu Munga Tehnan.

Naamini kati yetu kuna wanaojua historia yake, maana mtandaoni haupatikani.

Ombi kwa Moderator Kama kuna uwezekano wa kuziweka mada zake pamoja kwenye mada moja kuu, zile zenye maudhui ya kufanana.

Ombi kwa wana JF kama kuna mwenye hard copy ya kazi zake kupitia JITAMBUE pls share.
Gazeti la JITAMBUE hakika lilikuwa na thamani kubwa kuliko almasi. Lala salama MUNGA TEHENAN. Hakika kizuri hadumu!
 
Wakaniambia 'shemeji piga mzigo'


Nilikutana na binti huyu mwaka 1990 wakati huo nikikaa na kaka yangu maeneo ya Mwenge. Siku hiyo nilikuwa nimetumwa maeneo ya Ubungo na nilikuwa naendesha gari la kaka yangu aina ya Toyota Mark II ambayo ilikuwa bado ina hali nzuri na mziki mnene. Nilikuwa nimepiga T-shirti na Jinzi na miwani ya jua. Niliamua kupitia barabara ya Chuo Kikuu lengo langu likiwa ni kujaribu bahati yangu kama nitakutana na binti yeyote anayesubiri usafiri nimpe lifti na kujaribu kutupia nyavu.

Ilikuwa ni kawaida yangu kila nikitumwa na kaka na kupewa gari napitia barabara ya Chuo Kikuu lengo langu likiwa ni hilo la kuopoa vimwana na mara nyingi nilikuwa sikosi kimwana wa kumpa lifti na kumtongoza. Wapo niliokuwa nikiwapata na wale niliokuwa nikiwaona washamba nilikuwa nawapotezea.

Siku hiyo nilibahatika kumpata binti mmoja. Alikuwa ni mzuri hasa kwa sura na umbo na weupe unaoashiria kuwa mambo yake ni mazuri. Nilisimama na kumtupia salaam, na yeye bila kusita aliniitikia na ndipo nikamwambia kama anaelekea Ubungo nimsogeze. Awali alisita lakini baada ya kumsisitiza alikubali kupanda nikaondoka naye. Njiani nilianza kumsomesha, hakuonekana kuwa mgumu, ingawa nilijishtukia kutokana na binti huyo kuonekana ni wa matawi.

Aliponiuliza ninaishi wapi na ninachofanya, nilimwambia ninaishi kwa kaka yangu ambaye ni mwanajeshi na nikamdanganya kwamba, ndio nimemaliza chuo kikuu mwaka uliopita na kwa sasa ninafanya kazi kama mwanadiplomasia pale wizara ya mambo ya nchi za nje. Nilimwambia kuwa, huwa nasafiri mara kwa mara nje ya nchi kwa shughuli za kikazi na kuonekana kwangu nchini ni mara chache sana. Aliponiliza kama huwa nasafiri nchi gani, nilimwambia, huwa natembelea zaidi nchi za Maziwa makuu. Hata hivyo nilimwambia kwamba, ndio ninajipanga nitafute nyumba ili nihame kwa kaka yangu kwa kuwa ndio nimeanza kazi nilikuwa bado najipanga ingawa kaka yangu hataki nihame hapo kwake.

Kwa upande wake alinijulisha kwamba na yeye amesoma nchini Uingereza na anafanya kazi katika ubalozi fulani wa mojawapo ya nchi za Scandinavia (naomba nisiutaje huo ubalozi) na anaishi na wazazi wake ambapo baba yake ni mhadhiri hapo Chuo kikuu. Alianza kunipigisha mastori yanayohusiana na mambo ya kidiplomasia ikabidi nimpotezee na kubadilisha stori ili asije akanishtukia.

Baada ya kumpa soma alikubali na kuniahidi nimtembelee hapo nyumbani kwao wiki ijayo mwishoni mwa juma ili tutoke out kwa ajili ya kufahamiana zaidi. Kwa kuwa simu za mkononi zilikuwa bado hazijaingia nchini alinipa namba ya simu ya nyumbani kwao. Tulipofika Ubungo aliteremka na kushika hamsini zake akiniacha na mimi nikifanya shughuli iliyonipeleka hapo Ubungo. Kwa muda mfupi nilioongea na yule binti alionekana kunipenda sana kwani hata wakati anashuka kwenye gari alinisisitiza sana tuonane hiyo wiki ijayo.

Ukweli ni kwamba nilikuwa sina kazi, na nilikuwa ndio nimemaliza kidato cha nne na kuangukia pua, yaani kwa kupata divisheni ya ziro. Wiki iliyofuata tangu nikutane na yule binti nilipata kazi ya kutembeza vitu na kuuza, maarufu kama promosheni. Siku hiyo nikiwa na furushi langu la vyombo na mwenzangu mmoja, yule binti aliniona. Alinikuta maeneo ya Kijitonyama akiwa kwenye gari. Mimi sikumwona, na alinipigia honi na alipoona sisikii alishuka. Alinikimbilia huku akiniita jina. Niligeuka na kugundua kuwa ni yule mpenzi wangu wa Chuo Kikuu niliyempa lifti na kumpiga fix.

Nilibabaika sana kwa kweli. Ilibidi hata kabla hajanisemesha, nimwambie Yule mwenzangu, ‘au labda ni nyumba hii hapa, maana nimechoka sana.' Yule binti akiwa ameshikwa na butwaa aliniuliza mbona niko kule na furushi kubwa. Nilimwambia, ‘ninamsindikiza huyu boy shamba wetu kwao. Ameacha kazi nyumbani nataka nimkabidhi kwa kaka yake. Ndio anajaribu kunionyesha nyumba, lakini naona kama naye kapasahau.' Nilimjibu nikiwa nimebabaika sana.
‘Oh, Nilishangaa kukuona na hilo furushi. Je nikupeni lifti ili tutafute hiyo nyumba yenyewe?' aliniuliza. Nilimwambia asisumbuke, tutatafuta hiyo nyumba na tutaipata tu. Aliniaga akionyesha kutoridhishwa na maelezo yangu.

Baada ya tukio lile niliona kazi ile haifai na nikaamua kuiacha. Nilipata kazi kwenye mghahawa mmoja uliopo mjini karibu na posta. Nilianza kazi pale kama mhudumu yaani waiter. Siku moja nikiwa nachukua order ya chakula waliingia wateja, sikuwatazama vizuri kwa sababu ya kashkash ya kazi mchana huo. Nilikwenda katika meza yao ili kuchukua order yao. Nilipofika pale walipokaa hao wateja nilikutana uso kwa uso na yule mpenzi wangu wa Chuo Kikuu. Niliishiwa pozi. Niligeuka haraka na kutaka kuondoka. Nilikuwa nataka kukimbilia jikoni. Lakini nilikuwa nimechelewa. Kwani aliniita kwa jina na kusema, ‘usijali, najua kinachoendelea. Ndio maana nimeamua kuja kula hapa. Chukua order yetu ya chakula na kuwa tu huru, kwani tangu wakati wa promosheni ya vyombo, nilikuwa najua….'

Aliposema hivyo aliwatazama wale wenzake. Mmoja wao aliniambia, ‘shem usijali piga mzigo, mapenzi kitu kingine na kazi zetu kitu kingine.' Nilienda jikoni, lakini sikurudi tena. Yaani ilikuwa ni kashfa kubwa ambayo sitakuja kuisahau mpaka leo hii niko na mama Ngina. Hadi leo sijui yule binti yuko wapi. Maana niliacha kazi na kwenda kusoma mkoani Arusha. Nashukuru hakujua ninaishi wapi pale Mwenge. Hata hivyo nilijifunza mengi, lakini kubwa zaidi nilijifunza kujiamini na ndio maana hadi leo mtu akiniliza nakaa wapi na ninafanya kazi gani ninamwambia ukweli kwamba ninaishi Mwanayamala kwa Kopa na ninafanyakazi ya Kuuza kahawa mjini.
Mtambuzi
Dah So sad Kupotea kwa Haya Magazeti.... Kiukweli ya kale Ni dhahabu
 
Kipindi hicho wenzangu wanasoma magazeti ya mwanaspoti,sani,n.k mie hela yangu kwenye jitambue tena ilikuwa mia 5,wenzangu wakawa wanadai nitazeeka mapema kwa kusoma mambo yaliyo juu ya uwezo wangu. Nakubali kabisa jitambue ilinijenga kwa kiasi kikubwa sana hivi nilivyo leo hii.

Upande wa kiuchumi kulikuwa na makala iliyosema "siku wananchi wakijua ujanja huu,mabenki yatafilisika". Ile mada ilileta wazo akilini mwangu hadi leo pamoja na wenzangu kadhaa tunamiliki kikoba/saccos ambayo inatufanya tuishi kwa kuamini kesho imeishapatiwa utatuzi. Sijawahi kukopa pesa benki.
Mkuu tushirikishe Kidogo Makala hiyo....
 
Ukiweka ahadi lazima uitimize..Ukiweka nadhiri ni lazima uitangue la sivyo itakutesa kifikra na kudai utanguzi.

Mwaka wa jana kwenye post moja, tukiwa na mjadala, tulimjadili gwiji wa falsafa maizi Hayati Munga Tehnan na nikaahidi kuna na mada maalum kwa ajili yake kumuenzi. Naomba sasa nitangue nadhiri na ahadi yangu hii kupitia mada hii.

Kwa wengi wasiomfahamu ndio alikuwa Mmiliki wa gazeti la utambuzi liitwalo JITAMBUE na MSHAURI. Humo ndani kulijaa madini tupu ya falsafa kindakindaki, saikolijia, mambo ya kiroho kijamii hata utani na simulizi za kufurahisha sana.

Mimi ni mmoja wa shabiki na mwanafunzi wake mkubwa... Wengine ninaoweza kuwakumbuka kwa haraka ni pasco na Mtambuzi ..Natambua list ni ndefu na kila mmoja atakuja na mchango wake

Uzi utakuwa updated kutokana na kadiri maudhui yatakavyokuwa yanapatikana ili hatimaye tuwe na mada iliyoshiba kumhusu Munga Tehnan.

Naamini kati yetu kuna wanaojua historia yake, maana mtandaoni haupatikani.

Ombi kwa Moderator Kama kuna uwezekano wa kuziweka mada zake pamoja kwenye mada moja kuu, zile zenye maudhui ya kufanana.

Ombi kwa wana JF kama kuna mwenye hard copy ya kazi zake kupitia JITAMBUE pls share.
Wakushi twamuenzi
 
Mkuu tushirikishe Kidogo Makala hiyo....
Nakala zangu zote za jitambue ziliharibiwa pindi nilipoondoka nyumbani. Ila ile mada ilihusu kujiwekea akiba kwa vikundi halafu mnajikopesha kulingana na uwezo wenu. Ila inahitaji nidhamu ya hali ya juu kufikia hili lengo.
Kwa ufupi tu ni hivyo mkuu.
 
Ndo Maana Nakukubali Sana... Wewe Ni Mmoja wa Member Muhimu Sana Mlionifanya nipende JF. Upo Wewe Bujibuji, Mkeo Faiza Fox, Preta na Mamndenyi.... Big up Sana Kaka kwa Mchango wako humu jamvini....
Mkeo Faiza Fox, [emoji16][emoji16][emoji16][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1548][emoji1752]
 
Mkuu mi niliyakuta humuhumu. Sasa Mimi Ni Nani nipingane na wahenga??? Ili Hali nilikuwa Mgeni?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3]sawa mkuu bi mkubwa yuko bukheri wa afya japo tumetengana kwa muda
 
Back
Top Bottom