KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

Late 90's to early 2000
Mkuu mshana, nimekaa na kutafakari!! kuwa sisi ni Roho tunaeishi ndani ya miili. Hivyo kuna kipindi tunaihitaji miili kama vile vifaranga vinavyohitaji ganda la yai!!

Na muda wa kifaranga ukisha isha wa kukaa ndani ya ganda, hutoka na kutokuhitaji tena ganda la yai!

Na kuna kipindi hatuhitaji hii miili, namanisha baada ya kufa. Kwahio Roho zetu huwa zinaendelea kuishi ktk mazingira mengine ambako, mwili hauhitajiki.
1 swali langu, je Roho zetu huwa zina roteti na kurudi tena dunia na kuvaa mwili mwingine??
2 je bado uumbaji wa Roho unaendelea kwa Muumba??( Namanisha Roho zinanazo kuja hapa duniani ni mpya kabisa) hazijawahi kuishi duniani?

Pia nimewahi kuota mji wa zamani kipi cha ukoloni, niliota jinsi huo mji ulivyokuwa na majengo yake yalivyokuwa!! wakati mji huu ulipikuwepo, Mimi nilikuwa sijazaliwa!! Nilipo msimulia Mama yangu kuhusu hio njozi, alinambia ni kweli! huo mji ulikuwepo!! na majengo niliyoyaona kwenye njozi ndivyo ulivyokuwa!!
Nauliza tena, Roho huwa zinarudi tena duniani??
 
Asante sana kwa kutoka nje ya box.... Roho ni nishati, roho ipo ilikuwepo na itakuwepo kifacho ni mwili uharibikao, kinachofanyika kwenye roho ni kubadili tu makazi (mwili) zaidi soma

Sanaa ya kifo
 
Asante sana kwa kutoka nje ya box.... Roho ni nishati, roho ipo ilikuwepo na itakuwepo kifacho ni mwili uharibikao, kinachofanyika kwenye roho ni kubadili tu makazi (mwili) zaidi soma

Sanaa ya kifo
Sawa mkuu, niendelee kusoma kwenye hii mada? au kuna vitabu vinavyofundisha zaidi??
 
Sawa mkuu, niendelee kusoma kwenye hii mada? au kuna vitabu vinavyofundisha zaidi??
 
Ngoja niendelee kuongea maarifa!!
 
Ukiweka ahadi lazima uitimize..Ukiweka nadhiri ni lazima uitangue la sivyo itakutesa kifikra na kudai utanguzi.

Mwaka wa jana kwenye post moja, tukiwa na mjadala, tulimjadili gwiji wa falsafa maizi Hayati Munga Tehnan na nikaahidi kuna na mada maalum kwa ajili yake kumuenzi. Naomba sasa nitangue nadhiri na ahadi yangu hii kupitia mada hii.

Kwa wengi wasiomfahamu ndio alikuwa Mmiliki wa gazeti la utambuzi liitwalo JITAMBUE na MSHAURI. Humo ndani kulijaa madini tupu ya falsafa kindakindaki, saikolijia, mambo ya kiroho kijamii hata utani na simulizi za kufurahisha sana.

Mimi ni mmoja wa shabiki na mwanafunzi wake mkubwa... Wengine ninaoweza kuwakumbuka kwa haraka ni pasco na Mtambuzi ..Natambua list ni ndefu na kila mmoja atakuja na mchango wake

Uzi utakuwa updated kutokana na kadiri maudhui yatakavyokuwa yanapatikana ili hatimaye tuwe na mada iliyoshiba kumhusu Munga Tehnan.

Naamini kati yetu kuna wanaojua historia yake, maana mtandaoni haupatikani.

Ombi kwa Moderator Kama kuna uwezekano wa kuziweka mada zake pamoja kwenye mada moja kuu, zile zenye maudhui ya kufanana.

Ombi kwa wana JF kama kuna mwenye hard copy ya kazi zake kupitia JITAMBUE pls share.
Nilimpenda sana huyu jamaa.Mungu arehem huko aliko..ninayo majarida yake mpaka leo..sijui alikuwa na kipaji gani.
Topic iliwahi sema.Je wajua mambo unayotahofia sana huwa hayatokei...
Ni ajabu siku nakutana na heading hii kwenye gazeti ndio nilikuwa nimetoka kutoa maelezo juu ya jambo fulani kubwa sana ambalo tutakiwa na wenzangu baada ya siku 3..twende na ilikuwa lazima tuwekwe ndani..njia moja tuu labda kutoroka..lakini sisi waadilifu sana tutatorokaje..
Nililinunua hilo gazeti nikiwa na hofuu kuu kuwa after 3 days ndio naondoka uraiani..
Nikasoma sikuamini nikasema huyu mtu labda mwehu hajui mkasa nilionao..nikasoma nikasoma wee wapi..

Nikapata tuu wazo la ku face problem siku hiyo liwalo na liwe..ingawa roho ya kutoroka imenijaa..siku ilipofika nikaenda nikijua ndio nimekwisha..kufika huko nikaingizwa chumba cha maelezo nikakuta jopo kubwa la wakunihoji nikijua leo sitoki humu.
Nikahojiwa sikukataa wala kujitetea ni ndio tuu..yaani walikuwa very friendly..ni maajabu..basi wakanipa ushauri kwa upendo ni kuniomba nifanye jambo fulani baada ya muda fulani..na sijalifanya mpaka leo..imepita zaidi ya miaka 16..
Niliamini mno hiyo kauli ya Marehemu Munga

Na ninalitunza lile gazeti mpaka leo.
Ila watu wengi walikuwa hawamwelewi kabisa ndio maana hakupata sapoti kabisa kwenye mamlaka mbalimbali na wadhamini..
 
Kipindi hicho wenzangu wanasoma magazeti ya mwanaspoti,sani,n.k mie hela yangu kwenye jitambue tena ilikuwa mia 5,wenzangu wakawa wanadai nitazeeka mapema kwa kusoma mambo yaliyo juu ya uwezo wangu. Nakubali kabisa jitambue ilinijenga kwa kiasi kikubwa sana hivi nilivyo leo hii.

Upande wa kiuchumi kulikuwa na makala iliyosema "siku wananchi wakijua ujanja huu,mabenki yatafilisika". Ile mada ilileta wazo akilini mwangu hadi leo pamoja na wenzangu kadhaa tunamiliki kikoba/saccos ambayo inatufanya tuishi kwa kuamini kesho imeishapatiwa utatuzi. Sijawahi kukopa pesa benki.
 
Mkuu Kama Inawezekana nina uzoefu na namna ya kurudifisha vitabu.Tuandae online platform watu wawe wanasoma huko.Namfuatilia Dr Hery Waminian yule wa Chomoza ya Clouds watu wanatoka Sana kwenye vifungo vya fikra.
Aisee nitakutafuta the soonest
 
Back
Top Bottom