Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jitahidi Mshana Jr. Yale magazeti ni hazina. Nina imani utavuka vizingiti vyote ili kumbukumbu za mpendwa wetu Munga zidumu kwa faida ya kizazi cha sasa a vizazi vijavyo.[emoji1545][emoji1545][emoji1545] kuna mwenzetu hapa amesema bado ana nakala karibia zote za gazeti la Jitambue, naangalia namna ya kufanya project tuhamishie kwenye soft copy...japo hapo kuna changamoto nyingi ikiwemo ya haki miliki
Na kifo chake kilikuwa na mkasa utujuze kikikuwaje?!Munga Tehenan Said, RIP , umenikumbusha mbali sana, sikuamini kifo chake mpaka leo.
Halafu kulikuwa na SIKU NILIYOFEDHEHEKA!Nakumbuka enzi hizo nilikuwa mwandishi mzuri sana wa Malala ya "Siku ambayo sitaisahau" ( Baadae, Siku niliyofedheheka)
Ukweli kabisa story nyingi nilizoandika zilikuwa "chai" tu lakini zilisisimua wengi sana. Siku hizi K Vant ishaharibu medulla yangu siwezi kuandika hata ubeti mmoja wa shairi...
RIP Munga Tehenan, the resting legend.
Ukiweka ahadi lazima uitimize..Ukiweka nadhiri ni lazima uitangue la sivyo itakutesa kifikra na kudai utanguzi.
Mwaka wa jana kwenye post moja, tukiwa na mjadala, tulimjadili gwiji wa falsafa maizi Hayati Munga Tehnan na nikaahidi kuna na mada maalum kwa ajili yake kumuenzi. Naomba sasa nitangue nadhiri na ahadi yangu hii kupitia mada hii.
Kwa wengi wasiomfahamu ndio alikuwa Mmiliki wa gazeti la utambuzi liitwalo JITAMBUE na MSHAURI. Humo ndani kulijaa madini tupu ya falsafa kindakindaki, saikolijia, mambo ya kiroho kijamii hata utani na simulizi za kufurahisha sana.
Mimi ni mmoja wa shabiki na mwanafunzi wake mkubwa... Wengine ninaoweza kuwakumbuka kwa haraka ni pasco na Mtambuzi ..Natambua list ni ndefu na kila mmoja atakuja na mchango wake
Uzi utakuwa updated kutokana na kadiri maudhui yatakavyokuwa yanapatikana ili hatimaye tuwe na mada iliyoshiba kumhusu Munga Tehnan.
Naamini kati yetu kuna wanaojua historia yake, maana mtandaoni haupatikani.
Ombi kwa Moderator Kama kuna uwezekano wa kuziweka mada zake pamoja kwenye mada moja kuu, zile zenye maudhui ya kufanana.
Ombi kwa wana JF kama kuna mwenye hard copy ya kazi zake kupitia JITAMBUE pls share.
Nimewahi kufanya naye kazi Business TimesLate 90's to early 2000
Hiki kitabu ninacho mkuu!! Pia nilikuwa msomaji wa gazeti la jitmbue!! jamaa alibadilisha sana mtazamo wangu!!My favorite bookView attachment 1724004
Hiki nakihitaji mkuu!!
Hiki pia nisaidie jinsi ya kukipata!
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1752][emoji1752][emoji1534][emoji1548]Good Sana! Sir Mshana Jr.
Munga Tehenan,Namkumbuka huyu Gwiji wa Habari,niliwahi msoma kwenye gazeti la RAI Nguvu ya Hoja.
Makala zake zilikuwa za kipekee sana.
Lakini nilikuja kununua kitabu chake ambacho nilijufunza kitu cha pekee sana! ambacho waandishi wengi hawafanyii kazi! Kuthibitisha Uzushi na Myth - Munga alikuwa Mwamba aisee.
Ni katika Kitabu cha SIRI ZA FIMBO YA MWALIMU NYERERE.
Aisee jamaa alikuwa scrutinizer mzuri sana sana.
RIP Munga.
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]Asante sanaKama kumbukumbu zangu zitakuwa nzuri Munga Tehenani alianzia kwenye chombo cha habari kinachomilikiwa na Chama kifupi kilijulikana kama SMC.... na Mwalimu wake ni Mzee Joe Nakajumo, wa chumba cha habari (Huyo Mzee Nakajumo amewapika malejindari hawahesabiki) mwanzoni mwa 90' kabla hawajahamia vyombo vingine vya Habari. Kwa uchache sana kwasasa wote ni Waandishi wa Habari, Waandamizi... Masoud Sanani, Nicodemus Ikonko, Jane Mihanji, Neli Msuya, Agnes Kabigi, Salva Rweyemamu, Mwina Kaduguda, Cosmas Mlekani, Bahati Mollel... nk... kama kuna mwenye mawasiliano na hao malejindari wawashirikishe kwa hili la nakala za Jitambue au chochote kinachomhusu Munga Tehenani itakuwa jepesi.