Kumbukizi: Profesa Kabudi akimwita Magufuli Mheshimiwa Mungu

Salaam wanajukwaa la Great Thinkers.

Nimekuwa nikitafakari umuhimu wa katiba mpya, na mapungufu ya Katiba iliyopo, ambayo inampa Rais madaraka makubwa ya kufanya anachotaka bila kuhojiwa wala kuwajibishwa na chombo chochote mpaka anakuwa na ukuu kama wa Mungu katika nchi yake.

Na hiyo ilidhihirika urais wa nchi hii ulivyoangukia mikono ya Rais wa awamu ya 5 John Magufuli. Alikuwa ana uwezo wa kusema lolote, kumfukuza yoyote, kumdhalilisha yoyote,kumpa hela yoyote, kupindisha sheria yoyote bila kuhojiwa na yeyote. Mpaka ikafikia hata mawaziri wake na watumishi wa serikali kumuogopa na kumuona kama Mungu.

Mbaya zaidi wengine katika kutaka kumsifia ili kujipendekeza zaidi,walijisahau wakamuita Mungu. Hii video ni Profesa Kabudi anamwita Magufuli mheshimiwa Mungu.

Musiba na Kangi Walisema Magufuli ni Zaidi ya YESU
 
utakuta mletamada ni msomi mzuri tu,lakini ameshindwa kutambua kwamba kabudi alikosea.

hivi Mungu kabla atajwe huwa tunatanguliza neno"mheshimiwa"!!!

hawa ndio wapinzani aina ya mdude[emoji38][emoji38].
 
Inaonekana jpm ataendelea Kuishi moyoni mwako milele. Ingekuwa vyema kama 'ungemrelease' kwa faida ya afya yako maana yeye alikuwa adui yako na leo hayupo tena na unavyoendelea kumsema ndivyo unavyozidi kuumia.
Read between the lines ndugu yangu. Lengo la mtoa mada ni kuonesha umuhimu wa katiba mpya na sio kumsema mwendazake.
Pole sana
 
Salaam wanajukwaa la Great Thinkers.

Nimekuwa nikitafakari umuhimu wa katiba mpya, na mapungufu ya Katiba iliyopo, ambayo inampa Rais madaraka makubwa ya kufanya anachotaka bila kuhojiwa wala kuwajibishwa na chombo chochote mpaka anakuwa na ukuu kama wa Mungu katika nchi yake.

Na hiyo ilidhihirika urais wa nchi hii ulivyoangukia mikono ya Rais wa awamu ya 5 John Magufuli. Alikuwa ana uwezo wa kusema lolote, kumfukuza yoyote, kumdhalilisha yoyote,kumpa hela yoyote, kupindisha sheria yoyote bila kuhojiwa na yeyote. Mpaka ikafikia hata mawaziri wake na watumishi wa serikali kumuogopa na kumuona kama Mungu.

Mbaya zaidi wengine katika kutaka kumsifia ili kujipendekeza zaidi,walijisahau wakamuita Mungu. Hii video ni Profesa Kabudi anamwita Magufuli mheshimiwa Mungu.

Shida haina adabu
 
Nyie wanafiki Kabudi alikosea tu lakini mnavyokomaa sasa.
Mara nyingi makosa ya kutamka huathiriwa zaidi na kilichopo moyoni na akilini mwako.

Ulishawahi kukosea, ukamwita mtu yeyote yule Mungu?
 
Back
Top Bottom