Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Rais Samia hapa alimwambia Masauni umesema kuna mauaji yaliyotokea Mwanza na Mtwara, na kwamba kwa taarifa zilizopo ni Jeshi la Polisi ndio limefanya mauaji, na kwamba Jeshi la Polisi limetengeza kamati ya kufanya uchunguzi na kupelekea taarifa.
Akasema, "Haiwezekani Jeshi la Polisi lifanye mauaji halafu lichunguze lenyewe, nimemwelekeza Waziri Mkuu aende kuunda kamati nyingine na kufanya uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi halafu alete taarifa."
Akiagiza wakati hayo yanaendelea Jeshi lijitafakari waone kama kinachotokea ndio kisingi ya Jeshi ya Polisi au ni vinginevyo.
Rais Samia aliyasema hayo akiwasalimia wananchi wa Magu, Mkoani Mwanza tarehe 04 Februari, 2022 akiwa njiani kuelekea mkoani Mara katika ziara ya kikazi ya siku 4.
Leo baada ya serikali yake na Jeshi la Polisi kutuhumiwa kufanya mauaji ya maelefu ya Watanzania, anataka ajichunguze? Leo haoni kama kujichunguza kunazuia uwajibikaji?
Make it make sense Wakuu!