Pre GE2025 Kumbukizi: Viongozi Tabora CHADEMA walizichapa kisa uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
C
Tukio hili lilitokea November 17, lakini limeibuliwa jana 4/5/2024 kama tukio jipya. Je, walioibua tukio hili na kusema ni ya karibuni walikuwa na nia gani?

=====

Katibu wa baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA BAVICHA Mkoa wa Tabora amezuiliwa kufanya mkutano na wandishi wa habari katika ofisi za chama hicho na uongozi wa Kanda jambo lililozua vurugu.

Vurugu hizo zimeibuka nje ya ofisi za chama cha CHADEMA kanda ya Magharibi ambapo pia ofisi za mkoa ziko hapo huku sababu ikitajwa kuwa ni afisa wa chama kanda ya Magharibi Paul Ginery kuzuia mkutano wa wanahabari ulioitishwa na katibu wa BAVICHA Mkoa wa Tabora Emmanuel Simwanza.

Baada ya vuta nikuvute na hali kuwa shwari Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Manispaa ya Tabora Mathias Mush amesema kuwa sababu za vurugu ni majina yaliyoenguliwa kwenye usaili kufuatia uchaguzi uliokuwa unatarajiwa kufanyika Novemba 20 mwaka huu.

Naye Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Tabora Emmanuel Siimwanza akizungumza nje ya ofisi za chama baada ya kuzuiliwa kutumia ofisi hizo anendelea kusisitiza kutokuwa na imani na viongozi waliofanya usaili na kusema kuwa uchaguzi hawatauruhusu kufanyika bila kupata majibu yanayoridhisha.

Paul Ginery afisa wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kanda ya Magharibi amabaye amezuia mkutano wa kiongozi wa BAVICHA na wandishi wa habari anasema uchaguzi utaahirishwa kama itatoka amri ya mamlaka kutoka makao makuu.

Baraza la BAVICHA wanapigania kurudishwa majina ya viongozi mbalimbali walioenguliwa katika usaili akiwemo katibu wa chama, Mwenyekiti wa baraza la wazee na wagombea wa baraza la vijana BAVICHA ambao wameeunguliwa wote.
Chadema wanagombana sana,ndio furaha yetu na mtu tuliyempa kazi ya kuwapoteza Sultan Mbowe
 
Eti hao ndio wanataka Katiba Mpya 😁😁Uchaguzi ndani ya CDM unatumia rushwa ili kupata viongozi watakaopambana kuleta katiba mpya ya kupinga rushwa na ufisadi
 
Sikuwahi kudhani CHADEMA ni chama kikubwa hivyo mmana Kila mtu anata uongozi nani ya CHADEMA, Inawezekana mama kahaidi neema Kwa CHADEMA
 
Back
Top Bottom