Unavyopenda udini utafikiri una hatimiliki ya huko akhera.. siwezi kushangaa nikisikia unafuga majini km wazee wenzio wa kiswahili..
Yoso,
Hakika Uislam naupenda mno.
Huu ni mwaka wa 26 toka nilipoandika kitabu changu cha kwanza: ''The LIfe and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.''
Kitabu hiki kimebadili maisha yangu na kimebadili historia ya uhuru wa Tanganyika na kimebadili pia historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Jina la kitabu liliwashtua wengi.
Kama kupenda Uislam kuna uhusiano na kufuga majini mimi nimekuwa hivi toka udogoni na kuwa hivi ni malezi yetu.
Kufuga majini ni ilm maalum nimeelezwa watu wanajifunza.
Majini ni viumbe kama sisi wameumbwa na Allah.
Nilipokuwa mtoto nilimfahamu Sheikh mmoja jina lake Mwalimu Bakari.
Mwalimu Bakari alikuwa mtu maarufu mitaa ya Gerezani akiishi Mtaa wa Livingstone na Kirk Street (Lindi Street).
Mwalimu Bakari walimpa jina lingine wakazi wa Dar es Salaam.
Walimwita Mwalimu Bakari ''Sethabari.''
Maana ya hili jina lingine ni kuwa mjuzi wa yale ambayo hayaonekani na macho.
Mimi alitokea kunipenda kwa kuwa nilikuwa nimefiwa na mama yangu nikiwa na umri wa miaka minne.
Akiniona alikuwa ananishika kichwa na kuniombea dua na kunifariji kwa kunipa fedha.
Hii ilikuwa kawaida yake.
Mwalimu Bakari watu wakihadithia mengi kuhusu yeye kuwa alikuwa anaweza kuzungumza na majini na kuwatuma kazi na wakamtii.
Kwa hakika ni ilm ambayo sijakutana na mtaalamu akanieleza hasa undani wake.
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika Baraza la Wazee wa TANU alikuwa Sheikh Issa Nasr kutoka Bagamoyo.
Sheikh Issa Nasr nimeambiwa alikuwa ujuzi mkubwa wa ilm ya majini.
Katika utafiti wangu wa kitabu cha Abdul Sykes nilifahamishwa kuwa Sheikh Issa Nasr alikuwa mmoja wa ''walinzi maalum' wa Mwalimu.
Wanasema popote alipokuwa Nyerere yeye atakuwa karibu yake na mpashaji habari wangu anasema hapo yuko na ''askari'' zake ambao hawaonekani.
Huyu aliyekuwa akinipa taarifa hizi ameniambia yeye akimjua Sheikh Issa Nasr toka udogoni kwake Bagamoyo na wao walipokuwa watoto wakimuona Sheikh Nasr amekaa nje ya nyumba yake walikuwa wanabadilisha njia kwa kumuogopa.
Mimi nikaamua kufanya utafiti kuangalia picha za Nyerere kama nitamuona Sheikh Issa Nasr karibu ya Mwalimu akipiga doria na jeshi lake la askari maalum.
Niliweza kuona picha mbili na zote tawire.
Sheikh Issa yuko pembeni ya Mwalimu Nyerere.
Picha ya kwanza ni ile ya Baraza la Wazee wa TANU iliyopigwa mwaka wa 1957.
Angalia picha hiyo hapo chini Sheikh Issa Nasr ni huyo aliyechutama miguuni kwa Nyerere na fimbo begani.
Picha ya pili ni ya mwaka wa 1961 siku Ian Macleod Waziri wa Makoloni alipotoa siku ya uhuru wa Tanganyika Karimjee Hall mwaka wa 1961.
Angalia picha hiyo utamuona Nyerere kabebwa mabegani na Sheikh Issa Nasr yuko pembeni yake.
Sheikh Issa Nasr huyu chini ya Mwalimu Nyerere ni wa pili kushoto baada ya aliyevaa koti jeusi
Kulia ni Sheikh Issa Nasr