Kumbukumbu mbaya za mapenzi: Mpenzi wangu kuchumbiwa na Mwanaume mwingine

Kumbukumbu mbaya za mapenzi: Mpenzi wangu kuchumbiwa na Mwanaume mwingine

josephdeo

Member
Joined
Nov 23, 2015
Posts
95
Reaction score
207
Nikiwa sina hili wala lile kwa siku hii iliyoanza vyema kuliko ilivyokuwa kwa siku mbili nyuma ambazo kiukweli ni ngumu kuzielezea lakini itoshe kusema zilikuwa mbaya sana. Asbuhi ikakucha huku ikionesha utofauti si unafahamu kuwa siku njema uonekana asbuhi basi na mimi niliweza kuiona kuwa siku hii ni njema kwa asbuhi ile.

Baada ya kuamka na kuzuga zuga ikafika wasaa wa kwenda kupata kifungua kinywa huku wataalam wa mambo wakiita breakfast au staftahi. Hali ya uchumi ilikuwa mbaya kiasi cha kutoruhusu kupata kile ambacho kinahitajika bali kilichotosha kiwango cha fedha.

Nikajivuta kutoka ghetto mpaka kwa mama muuza huku nikapata supu ya mia tano na kama kawaida ya supu kisukumio chake ni chapati na sikuwa wa tofauti na wengine bali chapati mbili zilinitosha kabisa kufunga ukurasa wa chakula hicho cha asbuhi.

Nilipomaliza kupata kifungua kinywa hicho nikawa narudi ghetto sikuwa na mchongo wowote si unajua kazi ya majobless. Hivyo nilikuwa narudi kubadilisha pozi ghetto baada ya kuwa kitandani sasa nilikuwa narudi kukaa kwenye sofa. Nikiwa nakaribia ghetto huwa kuna duka sehemu ambayo huwa tunafanyaga maemezi ya nyumbani kufika hapo nikakumbuka kununu vocha nilikuwa na kama siku tatu sikuwa nimeweka vocha kwenye simu yangu wala kutizama mambo ambayo yalikuwa yakiendelea kwenye ulimwengu.

Kujipapasa mfukoni nikakutana na mia tano ya sliva nami sikuchelewa nikamuamurisha muuzaji anipatie voda ya jero. Sikufuata amri ya hayati mzee baba kuwa jero tuuite mia tano bali niliendelea kile ambacho nimekizoea. Baada ya kukabidhiwa vocha ile kukatokea na vita ndogo akilini mwangu baada ya kutotosha kuunganishwa dakika pamoja na data hivyo ilinilazimu kuchagua kimoja kati ya hivyo.

Vyote vilikuwa muhumi kwa sababu dakika zilikuwa ni kwa ajili ya kumpigia bibie ambaye hatukuwa vizuri kwa siku za mwisho za mawasiliano yetu. Na data nayo iliniwezesha kutamba mitandaoni na kuona ni nini kinaendelea ulimwenguni si unajua sasa tuko kwenye ulimwengu wa teknolojia.

Baada ya mvutano nikapata majibu kuwa niweke data ili hata kama kumpigia nitampigia kwa whatsapp call. Kwenye wazo ili lilikuwa na logic yaani sababu za msingi nikajiunga chapu kwa haraka nikawasha data kwenye simu na kusubilia kwa dakika kadhaa ili notification zikate ili niweze kuona wapi pa kuanzia.

Dakika kama tatu hizi nibofya kitufe cha kwenda whatsapp ili kujua ni kipi kimewekwa kwenye status za watu. Kwani kwa kipindi hiki status zilikuwa zinawakilisha vyema hisia za mtu. Haraka haraka nikajibu meseji kadhaa nilizozituka pale kisha nikaswipe left kama watumiaji wenzangu wa android.

Zenyewe zikaanza kujipanga kwa kasi kidogo nami nikajipa subira ili kusubiri zitimie zote. Wakati nasubiri ikapita status ya bibie (jina kapuni) ikishuka chini kwa kuwa hatukuwa na maelewano mazuri nikaiona hii ndio ya kuiangalia kwani inaweza kuwa imeelezea vyema hisia zake. Sikutaka kuchelewa nikaanza kuscoll kwenda kuifuata nikaipata kisha kwa hamu kubwa nikaifungua nilichokutana nacho ndio kisanga kilichopelekea kuyaandika haya.

Ilikuwa video ya sekunde kumi na nane ikionesha kidole kilichokuwa na pete tena kidole ambacho kinatumika kuwekea pete ya ndoa. Moyo nao ni kama ulishitushwa na kitendo cha macho kuona kwani hali yangu ikabadirika ghafla huku mapigo ya moyo yakienda kwa kasi ambayo sikuweza kukadiria vyema ila kwa ufupi ni kuwa waliishinda ile ya kudunda mara sabini kwa dakika. Akili yangu ikawa na kazi ya kujiamisha kuwa ile haikuwa kweli bali ni maigizo tu.

Kwa kuwa kulikuwa na alama nyingine kumaanisha kuwa kuna stutus nyingine mbele ikabidi kuiweka huko sasa ndipo ambapo joto la mwili liliongezeka. Yalikuwa maneno machache sana ambayo niliyasoma vyema kwani nilijua kusoma na kuandika. "ukiona cha nini, wenzako wanawaza watakipata lini".

Maneno yale yakafanya kuiona siku ile kuwa siku mbaya kwangu kuwahi kutokea. Ila bado akili haikutaka kukubali kuwa jambo lile nililolishuhudia lilikuwa kweli ikanibidi kuswap left na kurudi kwenye charts hapo haraka nikaiona jina lake kwani nililiwekea pin chart yaani liwe juu ya convo yoyote pale kwenye charts zangu.

Kwa pupa niliyokuwa nayo nikapiga tena haikuwa voice call bali video ili niweze kumtizama kama ni yeye kweli aliyekuwa akiyafanya yale. Hakuchukua hata sekunde nyingi nikasikikia muungurumo kumaanisha kuwa simu ile ilipokelewa na upande wa pili ambapo mawimbi yalitumwa na yakafika. Kwenye kioo cha simu yangu akatokea mwanaume hali ambayo ilifanya nishituke kisha jamaa akauliza

"bro umesahau nini?". Huku nyuma yake nikiishuhudia sura ya bibie akiwa anafuraha sana juu ya kitendo kile. Kwa uharaka nikakata simu ile huku nikitumia mda kuzuia machozi ambayo kwa mbali nilianza kuhisi viashiria vyake.

Nikiwa bado niko kwenye tafakuri zito nikaona simu inawaka nikaiwahi ili kuona ni kipi kilifanya hayo. "tafadhali kuanzia sasa usinisumbue niko kwa mme wangu". Oooohps! Sauti ilinitoka huku sasa nikiwa sina unjanja tena machozi yalianza kuchuruzika huku yakitengeneza njia kushuka kwenye mashavu mpaka chini kwenye sakafu.

Hii ni baada ya kusoma ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa bibie yule.
 
Man down😔
Nikiwa sina hili wala lile kwa siku hii iliyoanza vyema kuliko ilivyokuwa kwa siku mbili nyuma ambazo kiukweli ni ngumu kuzielezea lakini itoshe kusema zilikuwa mbaya sana. Asbuhi ikakucha huku ikionesha utofauti si unafahamu kuwa siku njema uonekana asbuhi basi na mimi niliweza kuiona kuwa siku hii ni njema kwa asbuhi ile. Baada ya kuamka na kuzuga zuga ikafika wasaa wa kwenda kupata kifungua kinywa huku wataalam wa mambo
 
Nikiwa sina hili wala lile kwa siku hii iliyoanza vyema kuliko ilivyokuwa kwa siku mbili nyuma ambazo kiukweli ni ngumu kuzielezea lakini itoshe kusema zilikuwa mbaya sana. Asbuhi ikakucha huku ikionesha utofauti si unafahamu kuwa siku njema uonekana asbuhi basi na mimi niliweza kuiona kuwa siku hii ni njema kwa asbuhi ile. Baada ya kuamka na kuzuga zuga ikafika wasaa wa kwenda kupata kifungua kinywa huku wataalam wa mambo wakiita breakfast au staftahi.
Jamaa kachukua jiko jumla.! Wewe unalia nini
 
Ongeza bidii katika utafutaji wa kuongeza kipato chako.

Songa mbele kama injili ya Yesu wanawake wapo acha kujiliza liza utaumia wewe wakati yeye yupo kwenye mahaba mazito na jamaa
 
Nikiwa sina hili wala lile kwa siku hii iliyoanza vyema kuliko ilivyokuwa kwa siku mbili nyuma ambazo kiukweli ni ngumu kuzielezea lakini itoshe kusema zilikuwa mbaya sana. Asbuhi ikakucha huku ikionesha utofauti si unafahamu kuwa siku njema uonekana asbuhi basi na mimi niliweza kuiona kuwa siku hii ni njema kwa asbuhi ile. Baada ya kuamka na kuzuga zuga ikafika wasaa wa kwenda kupata kifungua kinywa huku wataalam wa mambo wakiita breakfast au staftahi.
Kawaida Sana broh. Tena Sana.
 
Nikiwa sina hili wala lile kwa siku hii iliyoanza vyema kuliko ilivyokuwa kwa siku mbili nyuma ambazo kiukweli ni ngumu kuzielezea lakini itoshe kusema zilikuwa mbaya sana. Asbuhi ikakucha huku ikionesha utofauti si unafahamu kuwa siku njema uonekana asbuhi basi na mimi niliweza kuiona kuwa siku hii ni njema kwa asbuhi ile.
Hilo dogo utayaona mengine mengi....Dunia ina mambo hii....pole sana
 
Back
Top Bottom