Kumbukumbu: prof. kighoma ali malima (15 december 1938 - 6 august 1995)

*..Waislam kusimama na kuuliza nini kimetokea kuwafanya wao juu ya mchango wao mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika leo wamekuwa raia daraja la pili?'*

Nikiwa chuo lecturer wetu wa Historia aligusia kua, waislamu kupitia chama chao waliwaomba wakoloni wasiachie kwanza madaraka kwakua waislamu wengi hawakua wamepata elimu na hawana nafasi za juu katika TANU.

Kama historia inasema hivi, na huu uzi umesema vingine. Je hii inamaanisha kulikua na kundi la waislamu lililopigania uhuru na kundi jingine likizuia uhuru usitolewe kwanza?
 
Tatizo ndugu zangu waislam hawajiamin na din yao, sasa kama waislamu wa saudia nao wanalalamika kunyanyaswa, nan awasaidie
 
Ni mengi na wala si ya kuambiwa. Alikuwa anapendelea kiuwazi waislam na kuwanyongelea mbali ambao si waislam. Usinichokoze nitoe vidhibiti hata kutaja mengine. Tuishie hapo mtetezi wa uislam
Wacha uongo. Malima hajawahi kumnyonga mtu.

Wapi alipompendelea Muislam?

Weeee uanze kuchokoza Waislam halafu ujidai usichokozwe?

Hatupigwi la kulia sisi tukageuza na la kushoto. Sisi tunalipa kisasi papo kwa papo. Kumbuka hilo.

Nyinyi roho ziliwauma sana alipobadili mfumo wa kuchaguana kwa majina. Huo ndiyo ukweli.
 
Nahisi "lecturer" wako alikuwa anakujaza ujinga.

Kama hauufahamu mchango wa Waislam kuhusu kudai Uhuru wa Tanganyika ngoja tumuombe mwanahistoria Allama Mohamed Said aje kutupa darsa kidogo kuhusu hayo.

Allama tunakuomba utusaidie kujibu hili swali.
 
Mama yangu hata kama ulipotokea kuna moto ukifika kwenye kisima hauna sababu ya kuhisi bado upo kwenye moto.

Maneno matupu nisingeyapokea. Maneno yenye rejea zake ni nitayapokea. Nilichoandika hapo hata yeye hakukitoa hewani alitoa kwenye vitabu.

Na swali langu halijasema waislamu hawana mchango. Soma vizuri tena.
 
Castr,
Naomba nami nikuulize swali na nakutaka radhi sana kwa kuwa wajibu wangu
ni mimi kukujibu si kukuulza swali.

Nipe kwa mukhasari hicho, ''chama chao ni kipi?''
Ikiwa unakusudia AMNUT hicho hakikuwa ''chama chao.''

Chama cha Waislam kilikuwa TANU.
Ningependa kujua kama mwalimu alifundisha historia hii.
 
Rest in Protons Dr. Malima.

Wazee waliokula ice cream za Princeton Junction hao.Nakumbuka kipindi chake Mipango na Uchumi tumekula sana lunch boxes za fish and chips na chicken and chips za Kilimanjaro Hotel.

Mohamed Said

Umemsoma Francis Fukuyama katika kitabu chake kipya "Identity: The Demand For Dignity And The Politics of Resentment" ?

Nimekisoma kimenikumbusha wewe sana.


 

Maalim Faiza,
Nami nilipokuwa mwanafunzi Mlimani kulikuwa na somo linaitwa
''Government and Politics in East Africa,'' lililohusu nationalist politics.

Walimu wakisomesha historia ya TANU wanaanza na TAA kisha wanaingia
kwa Julius Nyerere.

Hawataji kaingiaje au madaraka ya uongozi wa TAA aliyachukua vipi.
haijapata kusemwa hata siku moja kuwa Nyerere alipokelewa na Abdul
Sykes
au waligombea pamoja nafasi ya urais wa TAA mwaka wa 1953.

Picha iliyokuwa ikinijia ni kama vile kwa makusudi walikuwa wanakikwepa
kipande hiki au hawajui historia hii.

Katika semina nikichangia majadiliano nilikuwa namwambia mwalimu wangu
kuwa mimi naijua vizuri sana historia ya TANU kuanzia African Association,
kuja TAA hadi TANU yenyewe na sababu ya kujua kwangu ni kuwa TANU
imeundwa na wazee wangu.

Kwanza ilikuwa kubezwa na kuonekana kama kichekesho si na mwalimu bali
hata na wanafunzi wenzangu.

Lakini nilipokuwa nawatajia majina na mambo yaliyotokea na kuwaeleza kuwa
hawa watu mimi nimewaona kwa macho yangu taratibu akili zao zikawa zinajiuliza
maswali.

Sasa sijui kama bado wanafundisha historia rasmi au wamebadilika.
 
Kiranga,
Sijamsoma ndugu yangu.
Wapi kaka leo utapata vitabu vizuri kama hivyo?

Tumebakia kukodolea macho tu ukimuona Mzungu kashika kitabu.
 
Ni kweli nimekusudia AMNUT. Nilisema "chama chao" kwakua hiki kiliundwa kutetea maslahi ya Waislamu.

Kwa kadri ninavyojua TANU ilikua inaundwa na wote, waislamu kwa wakristo. Na hakikujisema kama kinatetea maslahi ya watu fulani pekee.

Ila hata kama TANU nayo ilikua ni ya waislamu watupu bado swali langu lina maana.
 
Weka rejea wacha porojo za kisimani.
 
Castr,
AMNUT waasisi wake walitoka TANU ukitoa Ramadhani Mashado Plantan hao wengine kama Hamisi Hunde na Abdulkarim Abdulwahid walikuwa watu wasio na nguvu yoyote katika ulingo wa siasa.

Kwa kiwango chochote hawa hawawezi kuwa ndiyo wawakilishi wa Waislam wa Tanganyika walipenda TANU.

Bahati mbaya Sheikh Hassan bin Ameir amefutwa katika historia rasmi kama alivyofutwa Abdul Sykes na miamba mingine katika historia ya uhuru.

Hawa kwa kuwataja wachache ndiyo walikuwa viongozi ambao laiti wangesimama kumpinnga Nyerere athari yake ingeonekana.

Ningependa kufahamu ulisoma historia ipi ni hii ya kweli au ile historia rasmi?
 
Nimesoma historia rasmi. Kuna majina umeyataja na kusema ukweli ndiyo nayasikia hapa.

Ndiyo kusema AMNUT lengo lao haswa lilikua ni uhuru usitolewe kwa TANU kwakua hiyo ingepelekea TANU kujiimarisha? Na hii inamaanisha kua sababu zilizotajwa, za kuzuia uhuru kisa waislamu kukosa nafasi za juu TANU, ni sababu za kupikwa?
 
Castr,
Niwie radhi lakini hujui sababu ya kuundwa kwa AMNUT.

AMNUT haikuanzishwa kwa sababu Waislam hawakuwa wameshika
nafasi za juu katika TANU.

Hadi kufika mwaka wa 1958 hapakuwa na tatizo wala chokochoko
yoyote ndani ya TANU.

Chokochoko ndani ya TANU na kuanza kwa minong'ono ya hali ya
baadae ya Waislam Tanganyika ilianza kusikika baada ya Uchaguzi
wa Kura Tatu uliofanyika mwaka wa 1958.

Waingereza waliweka masharti ya kibaguzi katika kupiga na kuchagua
wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria la kikoloni (Legislative Council).

Mpigaji kura alitakiwa kwanza awe na elimu ya darasa la 12, awe na
kipato cha pauni 400 za Kiingereza kwa mwaka, awe na kazi ya maana
na kura kupigwa kuwa kufuata utaifa, yaani kura kwa mgombea Mzungu,
Muasia na Mwafrika.

Baadae sharti la elimu ya darasa la 12 likabadilishwa ikawa darasa la 10.

Wanachama wengi wa TANU walipinga masharti haya ya ubaguzi kiasi
walikuja na kauli mbiu isemayo, ''kuingia katika Uchaguzi wa Kura Tatu
ni sawasawa na kujipaka kinyesi.''

Wanachama wa TANU wengi waliokuwa mstari wa mbele kupambana na
ukoloni hadi mwaka wa 1958 walikuwa Waislam na waliona masharti haya
yalikuwa yameletwa ili kuwaondoa wao katika kugombea na pia katika
kupiga kura.

Lakini katika mkutano wa Tabora juu ya pingamizi iliyokuwapo TANU ilipiga
kura kuamua kuingia katika Uchagzi wa Kura Tatu.

Hili liliwezekanaje ilhal viongozi wakubwa katika TANU kama Sheikh Suleiman
Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Zuberi Mtemvu, na wajumbe
takriban wote wa Baraza la Wazee, walikuwa wanapinga Kura Tatu?

Nyerere hakupata kueleza ni mkakati gani aliweka akishirikiana na uongozi wa
TANU Tanga wa Sheikh Rashid Sembe, Hamisi Heri, Mwalimu Kihere, Abdallah
Rashid Sembe, Ng'anzi Mohamed, Mustafa Shauri na Abdallah Makatta kutafuta
kuungwa mkono kuiingiza TANU katika Uchaguzi wa Kura Tatu.

Wala hakupata kusema kwa nini katika kwenda Tanga kutafuta kuungwa mkono
alimweka pembeni Zuberi Mtemvu Katibu wa TANU badala yake akamchukua
Elias Kissenge na ndiye aliyekwendanae kwenye mkutano wa Tabora.

Uamuzi wa kuingia kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu ulipita kwa tabu kuonyesha
upinzani uliokuwapo.

Matokeo ya TANU kuingia katika Uchaguzi wa Kura Tatu ikawa kuwa Waislam
kwa kuwa hawakuwa na elimu hawataweza kugombea wala kupiga kura na ili
TANU ipate wagombea wa kuingia katika uchaguzi ule lazima sasa wawapate
watu nje ya TANU kuja kugombea nafasi zile, watu ambao hawakushiriki hata
kidogo kuifikisha TANU pale ilipofika.

Haya ya kuleta sura mpya ndani ya TANU na kupewa nafasi za uongozi
ndiyo yaliyosababisha kuundwa kwa AMNUT.

Historia hii ya Uchaguzi wa Kura Tatu haiwezi kukamilika bila ya kueleza ugomvi
uliozuka kati ya Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere na matokeo yake
Sheikh Suleiman Takadir akafukuzwa chama kwa kosa la ''kuchanganya dini na
siasa.''

Historia hii ya Sheikh Suleiman Takadir inaogopwa kuelezwa hadi hii leo kwa
sababu ambazo sasa ziko wazi.

Nisimame hapa kwani bado yako mengi ya kueleza.

 
Kumbe ni lengo lako na ulikuwa unazuwa tu kuwa ni "lengo lao"! Maana umekiri hata majina mengine hujapata kuyasikia. Hayo majina ni yepi ulioanza kuyasikia "hapa tu"?

Naona juu hapo umeanza kupata darsa na linaanza kukuingia tartiibu.

Hayo majina ambayo hujawahi kuyasikia awali sasa umeyasikia na elewa kuwa hao ni wazee wetu.

Allama Mohamed Said mwaga darsa kaka yangu, aliyesema hatujui kitu tutulie kumbe hata majina ndiyo kaanza kuyasoma "hapa".
 
Sijakutana na mtu anapenda ugomvi kama wewe.

Sikumbuki kusema 'hamjui' nakumbuka kukwambia wewe 'haujui'

Majina ambayo nimeyasikia hapa hayajatajwa katika historia niliyosoma. Ndiyo maana nimesema nayasikia hapa.

Mama uwe unasoma basi. Hivi unavyofanya unakua kama ukikaa ukishikwa na hamu ya ugomvi ni kulog in kutafuta post kuijibu unavyojisikia kisha kusubiri majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…