Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Dr...umekuwa mjadala mzuri, tunaendelea kujifunza na kutafiti ukweli wa hoja za pande mbili kinzani
Mwaka wa 20.? Kwamba nitengeneze watu wangu katika historia? Hicho si kiwango changu
Ahsante kwa maoni yako, wanaoweza kubumba watu wakaandika historia yao mpya wamekusoma
Mkuu wangu, niseme nini basi mbona kila kitu umemaliza maalim wangu?Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking
Kuna hoja mbili kuhusu hili
1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam
Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali
2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir
Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.
Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.
Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole
3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.
Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki
1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.
Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10
Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine
Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii
Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.
Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?
Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!
Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.
Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia
Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
Baada ya wale kufuta nawe ukawadogosha kabisaaa!!!Yericko hili neno, "kudogosha," nimelipenda. Una fikra gani na wale, "waliofuta?"
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka wa 20.
Mlikuja na historia ya kivukoni mkawasahau waasisi, umesahau?
Tunangoja tuwasome akina Shivji na kazi yao mpya.
Wewe huwezi, labda uandike "love story" za kusadikika.
Yaani aandike historia kwakuweka watu wengine awapendao ila sio hawa waliyopo?Povu linakutoka nikafikiri umekuja na kitu kipya. Kumbe unatamani historia alivyoandika Mohamed Said iwe vingine.
Si uandike historia yako, uwaingize wote bila kuchukua chochote kutoka kwa Mohamed Said.
Thubutu.
Baada ya wale kufuta nawe ukawadogosha kabisaaa!!!
Yaani aandike historia kwakuweka watu wengine awapendao ila sio hawa waliyopo?
Hizi akili nyingi hizi...
Mzee wangu unarejea makosa yale yale, AA haiwezi kuasisiwa na Kleist ukamtupa Rais wake Cecil Matola,Yericko,
Abdul Sykes, ''alishirikishwa,'' katika kuunda TANU 1954.
Hii ndiyo raha niipatayo kila siku hata baada ya miaka 20 ya kutoka
kitabu cha Abdul Sykes.
Abdul anawakaribisha watu nyumbani kwake katika mikutano ya siri
ya kuunda TANU aliyekaribishwa ndiyo anakuwa kaasisi TANU na
mwenye nyumba anakuwa, ''kashirikishwa,'' na aliyemualika.
Inaleta raha sana moyoni kwangu.
Abdul alifikaje kuongoza TAA?
Jibu la haraka unaweza kusema kuwa hiyo African Association kaasisi
baba yake.
Ndipo Ahmed Rashhad Ali akamwambia Prof. Haroub Othman cha
ajabu kipi kwa Abdul kuasisi TANU?
Mbona hushangazwi kwa baba yake kuasisi African Association na Al
Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
Hakutosheka na jibu lile ikabidi aende kwa muhusika mwenyewe apate
kauli yake.
Matokeo yake ndiyo Prof. Shivji na jopo lake wanaandika sasa historia
ya Baba wa Taifa ili historia ikae vizuri.
Ibra kubwa ni kuwa jopo likaja kuzungumza na mwandishi awape habari
za Abdul Sykes na yeye akawapa nyaraka na picha za nyakati zile.
Jambo moja limezua jingine.
Wakati nafanya utafiti wa historia hii kila nilipomaliza mahojiano wale
wazee walikuwa wakinisomea dua kuiombea Mungu hii kazi ifanikiwe na
kweli dua zao zimekuwa makbul, yaani zimetakabaliwa, Allah kazikubali.
Huyu Abdul Sykes aliyefutwa katika historia ya TANU leo kila uchao yuko
midomoni watu wanamsoma na medali ya ''Mwenge wa Uhuru,'' kapewa.
Lakini Abdul aliingia vipi kuongoza TAA?
Ukitaka kujua inabidi urudi nyuma hadi mwaka wa 1947 Abdul akiwa na
miaka 23 alipoongoza mgomo wa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam.
Hiki ni kisa kitamu sana.
John Iliffe aliandika paper, '‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’'
katika Tanzania Notes and Records," 71 (1970) nzima lakini mengi yalimpita
sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Mimi nikafanya utafiti kuhusu chama cha makuli na mgomo ule na nikaandika,
''Dar es Salaam Dockworkers Movement 1947-1950,'' sikumuhurumia Abdul
Sykes bali huruma yangu ilikwenda kwa Iliffe.
Mkasa huu ndiyo uliomfikisha Abdul Sykes katika uongozi wa TAA 1950 na
akapata kuungwa mkono katika kuunda TANU 1954.
Vipi jambo muhimu la kihistoria kama hili lilimpita akashindwa kuona umuhimu
wake katika mustakbali na mwelekeo wa siasa?
Wana Majilis,
Someni kile kilichopitika Dar es Salaam kati ya mwaka wa 1947 hadi 1950 ambao
ndiyo ukajakuwa msingi ambao TANU ilikuja kujengwa juu yake:
Jibu hoja hapo juuWana Majlis...
Ilikuwa sasa baada ya yale yaliyotokea katika mgomo ule wa makuli 1950 na hamaki zile za wananchi ndipo Abdul sasa akaelekeza macho yake TAA.
Hapa tayari alikuwa keshajiwekea uhalali wa uongozi wa kuwasemea Waafrika.
Haikuwa kama uongozi mpya katika TANU ulizuka tu, la hasha.
Ulitanguliwa na vumbi, jasho na damu.
Hii ndiyo historia ya kuibuka kwa hamu ya wananchi sasa kutaka chama cha siasa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Naona unafyonza makabi na mbigiriMudir!
Nafyonza Ilm taarrtibu huku nakunywa kahawa na faluda.
Mkuu Pascal, duuu!Mkuu Yeriko, kwanza hongera sana kuandika kitabu, maana kuandika kitabu sio mchezo haswa kwa kuuzingatia utamaduni wa Watanzania na moyo wa kujisomea vitabu, yataka moyo sana kuandika kitabu ambacho hakitaingizwa kwenye ithibati yoyote!.
Umefanya kazi nzuri ila kwanza naomba uthibitisho, ni Bibi Sesilia Matola au ni Bw. Cecil Matola?. Nani aliyekudanganya Cecil Matola ni Bibi na jina lake ni Sesilia?!. Kama hiki ndicho ulichoandika kwenye kitabu chako hadi kutoa Hard Copy!, I wonder how many factual errors zitakuwepo kwenye the rest of kitabu hicho?!.
Kama jambo dogo kama hili umeshidwa to get the facts right, what about the credibility of the rest?.
Paskali
Ref:
A Modern History of Tanganyika
Google Books › books
John Iliffe - 1979 - History
Its first president was Mwalimu Cecil Matola, the aristocratic Yao teacher educated at Kiungani who ...
Kleist Sykes - Wikipedia
Wikipedia, the free encyclopedia › wiki › Kleist...
Kleist Sykes (1894–1949) was a Tanganyikan political activist. ... along with friends including Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu and Raikes Kusi.
Mohamed Said: CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YABOMOA ...
www.mohammedsaid.com › 2015/02 › c...
14 Feb 2015 - Historia ya CCM inaanza mwaka 1929 katika nyumba ya Cecil Matola (sasa mali ya marehemu ...
A Place in the World: New Local Historiographies from Africa and ...
Google Books › books
Axel Harneit-Sievers - 2002 - History
Matola, Cecil 1929. Cecil Matola Anatuhadithi Habari za Maisha Yake [ Cecil Matola tells us from his life]. Illambo Leo ...
Generations Past: Youth in East African History
Google Books › books
Andrew Burton, Andrew Ross Burton, Helene Charton-Bigot - 2010 - History
March 1930], Kisarawe District Book, TNA). 16. Cecil Matola to Chief Secretary (CS), 22 April 1930, TNA 61/ 207/I/12.
Nyerere: The Early Years - Ukurasa 245 - Matokeo ya Google Books
Google Books › books
Thomas Molony - 2014 - Biography & Autobiography
... Ujuzi Educational Publishers, 2006, pp.47–8 on the role of Martin Kayamba, Cecil Matola, Ramadhani Ali and Kleist ...
Miaka 48 bado tunaficha ukweli, kwa nini? – Raia Mwema
www.raiamwema.co.tz › miaka-48-bado-...
19 Mei 2012 - AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes ...
Ritz wanadhani TANU kaja mtu kaingia ofisi ya TAA New Street kaomba funguo za mlango kakaa kwenye kiti na vuuu! chama cha TANU kimetokeza pamoja na kadi zake na wanachama.Naona unafyonza makabi na mbigiri
Ungelitambua hilo usingetembea dunia nzima ukiwatukana... Hivi Kleist Sykes asingebadili dini yake ya ukristu kisa mwanamke akawa muislamu leo ungemlilia kila kona ya ulimwengu? Mbona Cecil Matola humsemi wala kumuenzi zaidi ya kumfifisha ilihali yeye ndie mwasisi wa vyama Tanganyika?
Achana na hao Yericko Nyerere, nasoma michango ya wafuasi wa Mohamed Said kama Ritz nabaki nacheka tu...jamaa ni msimuliaji mzuri sana wa hadithi na kwa upigaji wa soga hana mpinzani. Nawahurumia wenzetu wanaoamini hizo ngano zake lakini sishangai, kwa kweli kipaji anacho na kawapata wanaomeza tu kila anachoandika bila kutafuna kama FaizaFoxy.Naona unafyonza makabi na mbigiri
Historia yoyote inayoandikwa kutokana na simulizi ni historia ya mapokeo. Sisi wapenda simulizi, hupenda sana kusoma hadithi nzuri zinazosimuliwa na wasimulizi mahiri kama wewe Mkuu Maalim Mohamed Said, kiukweli simulizi zako ni mzuri. Kule mwanzo nilikuita mrongo, nikidhani urongo katika simulizi zako umeutunga wewe, but as days goes by, nimekuja ku realize, kumbe enda ikawa urongo hukutunga wewe, bali aliyekusimulia simulizi za urongo, hivyo wewe umeandika kile ulichosimuliwa ukidhani ndio ukweli, kumbe ulitanganywa na hao waliokusimulia.Hapa mwenye historia hii ni mie hawa jamaa zangu wanasoma
kile niichoandika mimi kama historia nilivyoipokea kutoka kwa
wazee wangu.
) then nakuunga mkono endelea kuandika vile vile unavuoandika ili ile mission iwe accomplished. Naunga mkono kuandika kwa malengo na sio kujiandikia tuu, na nakiri mimi ni mmoja wa wafuasi wako wakubwa humu jf kwa vile natambua you have "the powers", kitu ambacho ninakiheshimu sana.Wewe kama mwanazuoni, unapaswa kuwa totally impartial, ila kwa sababu niliwahi kusema humu kuwa 'you are a man with a mission', na 'the motive behind ni some ill motives', tuendelee tuu kuzipanda, tuzimwagilie zitamea, tusiwekee mbolea zimee vizuri, hadi zikomae tupate mavuno mengi!, nazungumzia zile 'mbegu' unazotupandia humu!.
Paskali