Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

? Kwamba nitengeneze watu wangu katika historia? Hicho si kiwango changu

Ahsante kwa maoni yako, wanaoweza kubumba watu wakaandika historia yao mpya wamekusoma
Mwaka wa 20.

Mlikuja na historia ya kivukoni mkawasahau waasisi, umesahau?

Tunangoja tuwasome akina Shivji na kazi yao mpya.

Wewe huwezi, labda uandike "love story" za kusadikika.
 
Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
Mkuu wangu, niseme nini basi mbona kila kitu umemaliza maalim wangu?
 
Mwaka wa 20.

Mlikuja na historia ya kivukoni mkawasahau waasisi, umesahau?

Tunangoja tuwasome akina Shivji na kazi yao mpya.

Wewe huwezi, labda uandike "love story" za kusadikika.

Maalim Faiza,
Ally Sykes
hapo chini anaeleza udugu baina yake na Julius Nyerere:

t_a31Ag_-B1AgxZeA1K1WYpTH-DVXmcg5X1D1lBlifyJt-GEtwJZ_fYBCjnazLAehRLfoSn9dVSUa5ko5FTQuXF7Sdb_sqnBm2EMZb_ZsBD9xvSX6w9anqua48UOL_nTpXPeAFAGoI_TvnIzgTRQMQRrtyY74jhtPDDut2cgqt38U9i1DPBcEoh3vwNa_1uu5OrWwTCROjpONjI0oJM-jI7L02fEEO18RrMr3GnvjFpPf32SlBLU3FfNbwq0phTbKgskOG2IMWUDkRTk2oGnDwkk_XkDU9AaF-yZQj3PkXzIbiCBrENVmhNPCSdct1Iw3cCdN9Vbttlr-QIXFDm3uOe2z5E53p-QmlpofGuS6fVAPrtUSTCyeQ8dfuJY408i8AqFdkTlTfaE_3wZnYWX9ad3mfLsHiW_AmfnRBGeHt6SgLFgd4ywyrGEb321uAePQmzyetFHTQzH_j3MDesUyAbvHPOLs4fE_i5Jw_EYVkYb_W9hyjdQVFbsc6rf9HFBuqPy4jp7oYn2mgGLnStnB2kcoX_ieOyu8wRRHZwq-Vdg6eYS6sFzm4l2UgU39VPVYXXlb465jOzPExAm1Gq8-MJQdC3zgAt9I6EcCS6fE5cUQoea9tcC=w867-h629-no


''In December 1960, we brought Masengo over to Dar es Salaam for a series of shows. The late Julius Nyerere, my friend and colleague, was the guest of honour at the show at Arnautoglo Hall. Colmore had come over from Nairobi for the show and I took the opportunity to introduce him to Nyerere. I took Colmore to Nyerere's house at Magomeni Majumba Sita.

We found Nyerere in a state of distress – he had just heard reports from Congo that Lumumba had been killed.

As members of Tanu and citizens of a country on the brink of achieving independence, we followed the news from Congo with great interest. And the events now unfolding were extremely distressing for most of us. I had a special interest, as at that time I believe I was the only person in TANU who had been to Congo and had first-hand experience of the ruthlessness of Belgian colonialism.

Masengo was also very sad to hear of the news that Katanga, his home province, had under Moise Tshombe seceded from the Congo Republic. So the only thing I can remember of that day when I took Colmore to Nyerere is how sad we all were about what had happened.

However, we took the opportunity while in Dar to have Masengo record his old songs with Tanganyika Broadcasting Corporation.''

Back in Nairobi, both Colmore and Masengo wrote to me, Colmore thanking me for introducing him to Nyerere and Masengo for successfully managing his tour and shows. Colmore told me how grateful he was to Nyerere for showing a firm stand on the Congo problem.

At that time, Masengo was incorporated into High Fidelity Productions as one of the directors. Colmore was a man of foresight; he realised that we would need the support of Nyerere if we were to expand our business in free Tanganyika. Our business interests there were already growing rapidly.

Colmore built a house in Moshi and used to drive over from Nairobi every weekend.''
 
Povu linakutoka nikafikiri umekuja na kitu kipya. Kumbe unatamani historia alivyoandika Mohamed Said iwe vingine.

Si uandike historia yako, uwaingize wote bila kuchukua chochote kutoka kwa Mohamed Said.

Thubutu.
Yaani aandike historia kwakuweka watu wengine awapendao ila sio hawa waliyopo?

Hizi akili nyingi hizi...
 
Yericko,
Abdul Sykes, ''alishirikishwa,'' katika kuunda TANU 1954.

Hii ndiyo raha niipatayo kila siku hata baada ya miaka 20 ya kutoka
kitabu cha Abdul Sykes.

Abdul anawakaribisha watu nyumbani kwake katika mikutano ya siri
ya kuunda TANU aliyekaribishwa ndiyo anakuwa kaasisi TANU na
mwenye nyumba anakuwa, ''kashirikishwa,'' na aliyemualika.

Inaleta raha sana moyoni kwangu.
Abdul alifikaje kuongoza TAA?

Jibu la haraka unaweza kusema kuwa hiyo African Association kaasisi
baba yake.

Ndipo Ahmed Rashhad Ali akamwambia Prof. Haroub Othman cha
ajabu kipi kwa Abdul kuasisi TANU?

Mbona hushangazwi kwa baba yake kuasisi African Association na Al
Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

Hakutosheka na jibu lile ikabidi aende kwa muhusika mwenyewe apate
kauli yake.

Matokeo yake ndiyo Prof. Shivji na jopo lake wanaandika sasa historia
ya Baba wa Taifa ili historia ikae vizuri.

Ibra kubwa ni kuwa jopo likaja kuzungumza na mwandishi awape habari
za Abdul Sykes na yeye akawapa nyaraka na picha za nyakati zile.

Jambo moja limezua jingine.

Wakati nafanya utafiti wa historia hii kila nilipomaliza mahojiano wale
wazee walikuwa wakinisomea dua kuiombea Mungu hii kazi ifanikiwe na
kweli dua zao zimekuwa makbul, yaani zimetakabaliwa, Allah kazikubali.

Huyu Abdul Sykes aliyefutwa katika historia ya TANU leo kila uchao yuko
midomoni watu wanamsoma na medali ya ''Mwenge wa Uhuru,'' kapewa.

Lakini Abdul aliingia vipi kuongoza TAA?

Ukitaka kujua inabidi urudi nyuma hadi mwaka wa 1947 Abdul akiwa na
miaka 23 alipoongoza mgomo wa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam.

Hiki ni kisa kitamu sana.

John Iliffe aliandika paper, '‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’'
katika Tanzania Notes and Records," 71 (1970) nzima lakini mengi yalimpita
sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Mimi nikafanya utafiti kuhusu chama cha makuli na mgomo ule na nikaandika,
''Dar es Salaam Dockworkers Movement 1947-1950,'' sikumuhurumia Abdul
Sykes
bali huruma yangu ilikwenda kwa Iliffe.

Mkasa huu ndiyo uliomfikisha Abdul Sykes katika uongozi wa TAA 1950 na
akapata kuungwa mkono katika kuunda TANU 1954.

Vipi jambo muhimu la kihistoria kama hili lilimpita akashindwa kuona umuhimu
wake katika mustakbali na mwelekeo wa siasa?

Wana Majilis,
Someni kile kilichopitika Dar es Salaam kati ya mwaka wa 1947 hadi 1950 ambao
ndiyo ukajakuwa msingi ambao TANU ilikuja kujengwa juu yake:
  1. Mohamed Said: The Book: Excerpts...Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part One
  2. Mohamed Said: Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part Two
  3. Mohamed Said: Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part Three
Mzee wangu unarejea makosa yale yale, AA haiwezi kuasisiwa na Kleist ukamtupa Rais wake Cecil Matola,

Hivi unajua maana ya Rais? Je maana ya Katibu?

Vivyo hivyo TAA haikuasisiwa na Abdul Sykes, ukamtupa Rais wake Vedasto Kyaruzi.

Hivi unajua maana ya Rais? Je maana ya Katibu?

TANU haikuasisiwa na Abdul Sykes ukamtupa rais wake Julius Nyerere, tena hapa utambue tanu imeanzishwa baada yq miaka 6 ya Julius Nyerere akiwa mwanachama hai na kiongozi wa TAA toka Makelele Uganda akiwa Katibu wa tawi 1948, Kisha akawa katibu wa Jimbo la Magharibi (Tabora), kisha akaja dar na kugombea urais na kushinda... Hivyo hakuwa mgeni na TAA kama unavyojaribu kuwaaminisha watu.
 
Yericko unadhani mimi hii historia nakulenga wewe?

Kuna maelfu ndiyo leo wananisoma na kusikia mambo mapya.

Hao ndiyo wataamua wewe tayari ushafanya uamuzi.

Hii ndiyo sababu naweka vitu vingi vya wakati ule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi

Kwa heshima ya jamvi ningependa kueleza machache yanayotufanya tuonekana ''Ignorant''
Nitatumia baadhi ya maneno ya lugha yangu ya std VIIB, asijekurupuka mtu na kusema ni matusi

Watu wanashangaa tunaposhindwa kujadiliana kwa hoja. Hoja inajibiwa kwa hoja
kuna majibu yanatowelewa au kuchangiwa kwa njia 'insane' hadi kuhoji weledi mhusika

1. Kwamba 'nendeni mkaandike historia yenu yenye kitu kipya'
Wanasema hayo ni illiterate. Historia ni 'dead subject' huwezi kuja na kitu kipya.
Tukio limetokea, hakuna anayeandika historia mpya isipokuwa anayefanya jambo la kihistoria kwa sasa au anayerejelea matukio kwa mtazamo tofauti na si kitu kipya

AA, TAA, Mwalimu Matola, Kleist, Rais wa TAA na mwanzilishi wa TANU abdul, Nyerere, Mtemvu, AMNUT, UTP n.k. vilikuwepo.
Unaandikaje historia mpya? Yaani utafute wahusika kutoka kichwani! mawazo gani haya!

Historia ya Tanganyika itaandikwa kwa wahusika wale wale, hakuna aliyekuja na kitu kipya wala atakayekuja na kitu kipya.

Wote watazunguka hapo hapo wakiwa na info za ziada ambazo si mpya.

2. 'Andikeni vitabu vyenu vya historia ya Tanganyika''
Kwamba ukisoma tahariri katika gazeti au makala na hukubaliani nayo basi suluhisho ni kuanzisha gazeti ili upinge au urekebishe mapungufu. Insane! insane!

Hatuwezi kuandika vitabu vya historia kila mmoja.
Hilo halizuii watu kusoma historia au wanaotaka kuandika kkufanya hivyo pia
Dunia ya sasa uelewa wa kila nyanja ni lazima si muhimu

Makosa ya zamani eti Dr hatakiwi kuwa mwanasiasa yamepitwa na wakati.
Anayepanga mshahara ni mwanasiasa vipi Dr asijue yanyoendelea katika siasa au kushiriki

Injinia anatakiwa ajue nini kinaendelea kisiasa, sayansi, uchumi na historia

Msomi mzuri ni yule anayejua nini kilichomzungumka kwa wakati husika.

Hivyo kusoma historia ni muhimu kama ilivyo kujua mambo mengine.
Hii si lazima kila mtu aandike kitabu cha histori, insane !

Kwamba usipokubaliana na mstari mmoja au aya moja au chapter, basi hutakiwi kuhoji bali unaelekezwa ukaandike kitabu chako kueleza concern! Inawezakaje

Ni mjinga ansyedhani anapaswa kutazama eneo moja tu.
Hivi utawaezaje kutafsiri trend ya stock market kama hujui kwanini zilianzishwa na lini. Hiyo tu ni historia sasa utakwepaje historia?

Kusema kwamba kila mtu akaandike historia ni njia nyepesi ya kutokuwa na majibu, na ni majibu yasiyo na maana kabisa

Elimu siyo certificate , ni uwezo wa kuchambu na kuchanganua mambo

Kama hujui namba 1 na 2 hapo juu, huja elimika hata kama una lundo la vyeti kutoka kule
 
Wana Majlis...
Ilikuwa sasa baada ya yale yaliyotokea katika mgomo ule wa makuli 1950 na hamaki zile za wananchi ndipo Abdul sasa akaelekeza macho yake TAA.

Hapa tayari alikuwa keshajiwekea uhalali wa uongozi wa kuwasemea Waafrika.

Haikuwa kama uongozi mpya katika TANU ulizuka tu, la hasha.

Ulitanguliwa na vumbi, jasho na damu.

Hii ndiyo historia ya kuibuka kwa hamu ya wananchi sasa kutaka chama cha siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana Majlis...
Ilikuwa sasa baada ya yale yaliyotokea katika mgomo ule wa makuli 1950 na hamaki zile za wananchi ndipo Abdul sasa akaelekeza macho yake TAA.

Hapa tayari alikuwa keshajiwekea uhalali wa uongozi wa kuwasemea Waafrika.

Haikuwa kama uongozi mpya katika TANU ulizuka tu, la hasha.

Ulitanguliwa na vumbi, jasho na damu.

Hii ndiyo historia ya kuibuka kwa hamu ya wananchi sasa kutaka chama cha siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu hoja hapo juu
 
Mkuu Yeriko, kwanza hongera sana kuandika kitabu, maana kuandika kitabu sio mchezo haswa kwa kuuzingatia utamaduni wa Watanzania na moyo wa kujisomea vitabu, yataka moyo sana kuandika kitabu ambacho hakitaingizwa kwenye ithibati yoyote!.

Umefanya kazi nzuri ila kwanza naomba uthibitisho, ni Bibi Sesilia Matola au ni Bw. Cecil Matola?. Nani aliyekudanganya Cecil Matola ni Bibi na jina lake ni Sesilia?!. Kama hiki ndicho ulichoandika kwenye kitabu chako hadi kutoa Hard Copy!, I wonder how many factual errors zitakuwepo kwenye the rest of kitabu hicho?!.

Kama jambo dogo kama hili umeshidwa to get the facts right, what about the credibility of the rest?.

Paskali

Ref:
A Modern History of Tanganyika
Google Books › books
John Iliffe - 1979 - ‎History
Its first president was Mwalimu Cecil Matola, the aristocratic Yao teacher educated at Kiungani who ...
Kleist Sykes - Wikipedia
Wikipedia, the free encyclopedia › wiki › Kleist...
Kleist Sykes (1894–1949) was a Tanganyikan political activist. ... along with friends including Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu and Raikes Kusi.
Mohamed Said: CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YABOMOA ...
www.mohammedsaid.com › 2015/02 › c...
14 Feb 2015 - Historia ya CCM inaanza mwaka 1929 katika nyumba ya Cecil Matola (sasa mali ya marehemu ...
A Place in the World: New Local Historiographies from Africa and ...
Google Books › books
Axel Harneit-Sievers - 2002 - ‎History
Matola, Cecil 1929. Cecil Matola Anatuhadithi Habari za Maisha Yake [ Cecil Matola tells us from his life]. Illambo Leo ...
Generations Past: Youth in East African History
Google Books › books
Andrew Burton, ‎Andrew Ross Burton, ‎Helene Charton-Bigot - 2010 - ‎History
March 1930], Kisarawe District Book, TNA). 16. Cecil Matola to Chief Secretary (CS), 22 April 1930, TNA 61/ 207/I/12.
Nyerere: The Early Years - Ukurasa 245 - Matokeo ya Google Books
Google Books › books
Thomas Molony - 2014 - ‎Biography & Autobiography
... Ujuzi Educational Publishers, 2006, pp.47–8 on the role of Martin Kayamba, Cecil Matola, Ramadhani Ali and Kleist ...
Miaka 48 bado tunaficha ukweli, kwa nini? – Raia Mwema
www.raiamwema.co.tz › miaka-48-bado-...
19 Mei 2012 - AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes ...
Mkuu Pascal, duuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko hii ndiyo historia ya mji huu wa Dar es Salaam na nimejitahidi kuieleza kadri ya uwezo wangu anaetaka aichukue asiyetaka aniachie mwenyewe.

Wala siko hapa kupingana na mtu nimshinde.

Kesho In Shaallah nitaweka habari kidogo ya Shamba kwa Mohamed Abeid walipojificha makuli na kufanya dua kabla ya mgomo.

Ni kisa cha kusisimua sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona unafyonza makabi na mbigiri
Ritz wanadhani TANU kaja mtu kaingia ofisi ya TAA New Street kaomba funguo za mlango kakaa kwenye kiti na vuuu! chama cha TANU kimetokeza pamoja na kadi zake na wanachama.

Ndipo ninapowaambia ijue kwanza historia ya mji wa Dar es Salaam ilikuwaje ndipo utaweza kutambua ukweli ni upi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungelitambua hilo usingetembea dunia nzima ukiwatukana... Hivi Kleist Sykes asingebadili dini yake ya ukristu kisa mwanamke akawa muislamu leo ungemlilia kila kona ya ulimwengu? Mbona Cecil Matola humsemi wala kumuenzi zaidi ya kumfifisha ilihali yeye ndie mwasisi wa vyama Tanganyika?

Nimefuatilia mjadala vema! Mzee Said Mohamed si wa kuupuuzwa hata kidogo,amesoma, anaelewa anachokifanya juu ya maandiko yake,He is a good writer!Hongera ,Lakini nina shaka kama aliandika vitabu vyake kwa kuzigatia Dhana pana ya wanahistoria kote duniani:-Objectivity and Subjectivity of History! Nilisoma Chapisho lake la Uamuzi wa Busara wa Tabora!kwenye gazeti la Daily Nation la kenya. Hisia zake na mapenzi mema ya Dini yake hayajamuacha salama! He is Subjective 90%! Arirekebishe hilo ajitafakari mwenyewe iwapo ameandika Yaliyokweli Tupu, Wanahistoria wengi wameshindwa kuitetea historia iliyoyakweli mbali na kuwa na Majina mengi makubwa!Hawakaishia kukosa thamani za kazi zao, Mzee Said Natumai waweza jifunza kwa yaliyomkuta Hugh Trevor Roper.(Natumaini unamfahamu huyu Mwanahistoria)
Yericko Nyerere Ni Kijana mwenye ari na nguvu ya uthubutu wa kuandika! Mimi nafurahi kuona tuna vijana kama hawa!Nampongeza sana! Makosa madogo madogo huwezi kuyakwepa,atakuwa bora na ataandika vema juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Nchi yetu!Msibeze amethubutu na katika kuthubutu kwake ndio maana hata mmeona hayo makosa.
Mnabuduhe
 
Naona unafyonza makabi na mbigiri
Achana na hao Yericko Nyerere, nasoma michango ya wafuasi wa Mohamed Said kama Ritz nabaki nacheka tu...jamaa ni msimuliaji mzuri sana wa hadithi na kwa upigaji wa soga hana mpinzani. Nawahurumia wenzetu wanaoamini hizo ngano zake lakini sishangai, kwa kweli kipaji anacho na kawapata wanaomeza tu kila anachoandika bila kutafuna kama FaizaFoxy.

Mengi anayaoandika kwa sasa ni marudio tu kwani tayari tulishayaongelea hapo awali na anachofanya ni kuyaibua baada ya muda fulani ili aendelee kuwa relevant hasa kwa wale ambao hawakufuatilia ya huko nyuma. Uzuri ni kwamba JF hutunza kumbukumbu...hebu ingieni hapa...!

 
Hapa mwenye historia hii ni mie hawa jamaa zangu wanasoma
kile niichoandika mimi kama historia nilivyoipokea kutoka kwa
wazee wangu.
Historia yoyote inayoandikwa kutokana na simulizi ni historia ya mapokeo. Sisi wapenda simulizi, hupenda sana kusoma hadithi nzuri zinazosimuliwa na wasimulizi mahiri kama wewe Mkuu Maalim Mohamed Said, kiukweli simulizi zako ni mzuri. Kule mwanzo nilikuita mrongo, nikidhani urongo katika simulizi zako umeutunga wewe, but as days goes by, nimekuja ku realize, kumbe enda ikawa urongo hukutunga wewe, bali aliyekusimulia simulizi za urongo, hivyo wewe umeandika kile ulichosimuliwa ukidhani ndio ukweli, kumbe ulitanganywa na hao waliokusimulia.

Kwa vile wewe ni mzuri katika kufuatilia documentary evidence ya hicho ulichosimuliwa na ukweli unaujua, kwa vile maandishi yako ni maandishi ya a man with a mission, ( reffer
Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ...
Wewe kama mwanazuoni, unapaswa kuwa totally impartial, ila kwa sababu niliwahi kusema humu kuwa 'you are a man with a mission', na 'the motive behind ni some ill motives', tuendelee tuu kuzipanda, tuzimwagilie zitamea, tusiwekee mbolea zimee vizuri, hadi zikomae tupate mavuno mengi!, nazungumzia zile 'mbegu' unazotupandia humu!.
Paskali
) then nakuunga mkono endelea kuandika vile vile unavuoandika ili ile mission iwe accomplished. Naunga mkono kuandika kwa malengo na sio kujiandikia tuu, na nakiri mimi ni mmoja wa wafuasi wako wakubwa humu jf kwa vile natambua you have "the powers", kitu ambacho ninakiheshimu sana.

Endelea kutulisha kile ulicholishwa kwenye hizo simulizi, ingawa kuna urongo mwingi, lakini pia kuna ukweli mwingi, na kitu kikubwa kwangu sio urongo au ukweli wa makala zako, bali ni ilmu iliyomo ambayo kama sio wewe kutuandikia humu, akina sisi kama tusinge vifahamu visa vingi.

Asante kwa simulizi zako za hadith njoo, uwongo njoo utamu kolea.

Paskali.
 
Back
Top Bottom