Yericko,
Abdul Sykes, ''alishirikishwa,'' katika kuunda TANU 1954.
Hii ndiyo raha niipatayo kila siku hata baada ya miaka 20 ya kutoka
kitabu cha
Abdul Sykes.
Abdul anawakaribisha watu nyumbani kwake katika mikutano ya siri
ya kuunda TANU aliyekaribishwa ndiyo anakuwa kaasisi TANU na
mwenye nyumba anakuwa, ''kashirikishwa,'' na aliyemualika.
Inaleta raha sana moyoni kwangu.
Abdul alifikaje kuongoza TAA?
Jibu la haraka unaweza kusema kuwa hiyo African Association kaasisi
baba yake.
Ndipo
Ahmed Rashhad Ali akamwambia
Prof. Haroub Othman cha
ajabu kipi kwa
Abdul kuasisi TANU?
Mbona hushangazwi kwa baba yake kuasisi African Association na Al
Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
Hakutosheka na jibu lile ikabidi aende kwa muhusika mwenyewe apate
kauli yake.
Matokeo yake ndiyo
Prof. Shivji na jopo lake wanaandika sasa historia
ya Baba wa Taifa ili historia ikae vizuri.
Ibra kubwa ni kuwa jopo likaja kuzungumza na mwandishi awape habari
za
Abdul Sykes na yeye akawapa nyaraka na picha za nyakati zile.
Jambo moja limezua jingine.
Wakati nafanya utafiti wa historia hii kila nilipomaliza mahojiano wale
wazee walikuwa wakinisomea dua kuiombea Mungu hii kazi ifanikiwe na
kweli dua zao zimekuwa makbul, yaani zimetakabaliwa, Allah kazikubali.
Huyu
Abdul Sykes aliyefutwa katika historia ya TANU leo kila uchao yuko
midomoni watu wanamsoma na medali ya ''Mwenge wa Uhuru,'' kapewa.
Lakini
Abdul aliingia vipi kuongoza TAA?
Ukitaka kujua inabidi urudi nyuma hadi mwaka wa 1947
Abdul akiwa na
miaka 23 alipoongoza mgomo wa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam.
Hiki ni kisa kitamu sana.
John Iliffe aliandika paper, '‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’'
katika
Tanzania Notes and Records," 71 (1970) nzima lakini mengi yalimpita
sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Mimi nikafanya utafiti kuhusu chama cha makuli na mgomo ule na nikaandika,
''Dar es Salaam Dockworkers Movement 1947-1950,'' sikumuhurumia
Abdul
Sykes bali huruma yangu ilikwenda kwa
Iliffe.
Mkasa huu ndiyo uliomfikisha
Abdul Sykes katika uongozi wa TAA 1950 na
akapata kuungwa mkono katika kuunda TANU 1954.
Vipi jambo muhimu la kihistoria kama hili lilimpita akashindwa kuona umuhimu
wake katika mustakbali na mwelekeo wa siasa?
Wana Majilis,
Someni kile kilichopitika Dar es Salaam kati ya mwaka wa 1947 hadi 1950 ambao
ndiyo ukajakuwa msingi ambao TANU ilikuja kujengwa juu yake:
- Mohamed Said: The Book: Excerpts...Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part One
- Mohamed Said: Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part Two
- Mohamed Said: Abdulwahid Sykes and Dar es Salaam Dockworkers’ Union, 1948 Part Three