Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Paskali,
Ndiyo ibra kubwa ya kitabu cha Abdul Sykes.

Lipo kundi maalum akili zao zinakataa kabisa kukubali kuwa hivi nilivyoeleza
ndivyo ilivyokuwa.

Sasa Paskali unathubutu kumwita baba yangu, babu yangu watu ambao toka
siku ya kwanza African Association inaanzishwa walikuwapo ni waongo.

Kuwa zipo nyaraka nimezisoma mimi na Iliffe kazisoma na kazifanyia rejea ni
uongo.

Ingekuwaje kama hizi nyaraka zisingekuwapo?

Unakataa kuwa Chief Kidaha Makwaia hakuwapo na Abdul hakumshawishi aje
TAA wamchague president waunde TANU?

Ukweli ni huo wa Chuo Cha Kivukoni walioandika historia ya TANU na kuwafuta
wazee wangu.

Miaka 20 kitabu toka kichwapwe na tunakwenda toleo la nne bado kitabu kipo
katika mjadala tukirudia yale kwa yale mumo kwa mumo.

Wala hutaki kujiuliza ni sifa ipi iliyapelekea Kleist na wanae waingie katika lile
kamusi la wazalendo wa Bara la Afrika - Dictionary of African Biography?

Iko siku nitakuhadithia mshtuko waliopata Harvard na Oxford University Press
nilipowapelekea mswada wa Kleist.

Tunaweza tukajikumbusha:
Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)
 
Mag3,
Yericko
si makamo yangu kabisa.
Wewe unajua, yeye anajua na dunia nzima inajua.

Kama unafuatilia vizuri nadhani utaona ninapomwandikia na kumwekea
majibu ya maswali yake huwa harejei tena nyuma.

Mimi kwa ustaarabu huwa simkumbushi arejee kwani kufanya hivyo ni
kuleta ubishani.

Huwa nachukulia ukimya wake kuwa kajifunza kitu na huu ndiyo mtindo
wangu.

Maalim Haruna alikuwa akitufunza anasema mwanachuoni kalamu yake
haifedheheshi bali inasomesha.

Ukiandika lazima utakosolewa hili ni jambo la kawaida na mimi sikatai
kukosolewa khasa ukichukulia kuwa kazi yoyote ya binadamu lazima
itakuwa na makosa.
 
Mnabuduhe,
Ahsante sana.

Tusiende kwenye, ''intricacies,'' hapa si mahali pake hatuna watu hao.
Hili la kwanza.

Pili kama, ''review,'' zimeshaandikwa na wino umekauka.
Hiki si kitabu cha leo sasa kinaingia muongo wa tatu.

Hiki kitabu kimestua kila mtu.
The East African walifanya, ''serialisation,'' ya kitabu kwa wiki tatu mfululizo.

James Odindo aliyekuwa Managing Editor wa Nation aliponiona aliniambia
kuwa sisi Waswahili huwa hatujidhihirishi mpaka mtu atujue.

Nilikwenda kumuona ofisini kwake Nation House na picha ya kwanza iliyomjia
aliponiona kwa mara ya kwanza ni Mswahili natokea Mombasa.

Inabidi mzishinde nafsi zenu na mjue na kukubali kuwa historia hii ya TANU na
uhuru wa Tanganyika ni historia ya wazee wetu.

THE LIFE AND TIMES OF ABDULWAHID SYKES - 2nd January 1999
Michael Mundia Kamau
P.O. Box 17510
Nairobi
Kenya

Saturday, 2nd January 1999


The Group Managing Editor
Nation Media Group
P.O. Box 49010
Nairobi
Kenya

Dear Sir

RE: "THE LIFE AND TIMES OF ABDULWAHID SYKES"

This letter is again written in appreciation of the just concluded serialisation of "The Life and Times of Abdulwahid Sykes", in "The East African".

The book by Mohamed Said brings into focus very interesting details about the struggle for Independence in Tanzania. It was also curiously interesting to note that the signature tune of Kenya's ruling party, KANU, "Kanu yajenga nchi", is derived from a Nyamwezi victory song !

The Independence movement in virtually all African Countries was undoubtedley led by Men and Women of high intellect and vision, and we the later generations, are deeply indebted to the forebearers of the Independence movement.
 
Mzee wangu hao watu achana nao..utawafahamisha na utawapa mifano kutoka katika source tofauti bado wataendelea kuukataa ukweli na kutaka kuiandika historia kutokana na muono wa Imani yao..Tatizo la wanaloliona wao siyo kama hawafahamu na hizo sababu wanazoziandika hapa na hizo riwaya zinazoletwa hapa zote ni superficial na kiundani haswa sababu kuu ni kwa nini wawe wao? au kwa nini wawe watu wa pwani?
 

Kaka Mohamed Said Hawezi kubadilika kwenye hayo masuala ya kutetea Dini yake, yeye anaandika hiyo historia akiwa na lengo kuu la kutetea dini yake, wala usijisumbue kumshauri chochote, humu ndani ya JF hakuna mwenye uwezo wa kumshauri, yeye ndio Alfa na Omega

Kuhusu Yericko, kweli anaonekana ni mwenye nia hasa ya kuandika na kufika mbali, ana shida kubwa ya kutokuwa na wigo mpana wa kuelewa mambo kwa kina, anajua vitu vingi kwa juju juu tu, hafanyi utafiti wa kina, akijirekebisha mapungufu machache hayo anaweza kuwa mtunzi au mwandishi mzuri
 
Kituko ushauri katika nini? Mimi nimeandika historia ya wazee wangu walivyounda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika sasa wewe unipe ushauri katika lipi? Kwanini msiwashauri Chuo Cha Kivukoni walipoandika historia yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, hapa tatizo ni lugha tuu na tafsiri kati watu wanaoitwa waasisi na waanzilishi viongozi na mashujaa.

Kama AA iliasisiwa mwaka 1927 na rais wa kwanza ni Cecil Matola, Sykes akaupokea urais baada ya kifo cha Matola, kumtaja Skykes kuwa ndio mwasisi wa AA bila kumtaja Matola, huu ni urongo!.

Kama Mwaka 1948, AA iligeuka, kuwa TAA chini ya rais Dr. Vedastus Kyaruzi, Skykes kumtaja alikaimu tuu baada ya Dr. Kyaruzi kuhamishwa na 1953 aligombea na Mwl. Julius Nyerere akambwagwa vibaya, ni Nyerere ndie aliyeibadili TAA kuigeuza TANU, hivyo kama ni ushujaa, shujaa wa TAA ni Dr. Kyaruzi, chini ya hapo ni urongo!. Na shujaa wa TANU ni Nyerere, chini ya hapo ni urongo na shujaa wa Uhuru wa Tanganyika ni Nyerere, chini ya hapo ni urongo.

Kama lengo ni kutaja waasisi wa wazo, au mashujaa wa uhuru, then wote waliouhusika tangu wazo, watakuwa ni wanachama waanzishilishi na mashujaa, ila kila mahali shujaa mkuu ni mmoja tuu na sii Sykes popote tangu AA, TAA, TANU hadi Uhuru.

Ukiahadithiwa kisa cha urongo katika fasihi simulizi, na wewe ukauandika urongo ule katika fasihi andishi, mrongo ni sii wewe uliyeandika urongo, bali yule aliyekusimulia urongo!.

Ukweli na urongo katika fasihi simulizi ni very relative kama ilivyo imani ya dini za watu, watu wakiaminishwa dini fulani ndio dini ya ukweli dini nyingine zote ni za urongo, hivyo katika kujenga religious tolerance, tunafunza tuhubiri dini zetu tuu tunazoziamini bila kuwaeleza wengine wenye dini zao kuwa ni dini za urongo, hivyo ingekuwa hayo unayoyaandika kuhusu historia ya uhuru, ingekuwa unaandika juzuu, tusingesema lolote, lakini maadamu ni historia na sio dini, huwezi kuandika urongo, halafu kuna wanaoujua ukweli wakanyamaza, ila pia pia kuna kundi la akina sisi wapenda hadithi, hata kama tunajua tunadanganywa, maadam msimulizi ni hodari wa kusimulia, tunaona raha kusoma simulizi zake, tunajifunza mengi tusiyoyajua kuhusu simulizi hizo, japo simulizi nyingine ni za urongo, lakini watu humu tunaelimika,

Hivyo Maalim Mohamed Said endelea na simulizi za hadithi hadithi, uwongo njoo utamu kolea, tunafurahia!.

Paskali
 
Great words,rightly spoken.
Wacha nikitafute kitabu chake

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
huo msiba wa mudi,uongo huajawahi kumuacha mtu salama!
 
Haya hujayaona, au haujayapenda...

Ulikuwepo wewe au kuna mzee wako alikuwepo?

Kuna wazee wa mohamed Saidkwenye hiyo picha.

Hivi ukisoma huelewi basi hata picha huoni?
picha haimaanish kuasisi,ww picha za ccm unazokaa mbele kwenye kampeni,wajukuu zako ndo waje waseme wewe ndo ulikuwa 'kampeni meneja'?
 
Povu linakutoka nikafikiri umekuja na kitu kipya. Kumbe unatamani historia alivyoandika Mohamed Said iwe vingine.

Si uandike historia yako, uwaingize wote bila kuchukua chochote kutoka kwa Mohamed Said.

Thubutu.
Huwa nafuatilia uzi huu mara chachechache tu. Lkn hebu nieleze, kwa nini mnalazimisha ionekane harakati za tanganyika huru ni za waislam tu? Yaani kwa nini hata hamtaki kutambua watu wengine isipokuwa waislam pekee?

Tafta historia ya Independent church Movement in the movie, utagundua jinsi watu wengi walivyoshiriki. Mfano kanisa la AICT limeundwa pamoja na mambo mengine, kudai uhuru.

Haya basi nchi ni ya waislam, msitochoshe na ubaguzi wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Soma kisha useme walioachwa ni akina nani na utupe historia yao ya Uhuru. Halafu pia ukiona watu wametajwa au kuwekwa ambao hawakustahili basi utupe historia yao mbadala.

Yanini unaandikia mate na wino upo?
 


Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Ntamaholo,
Ikiwa unayo historia ya AICT katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa
Tanganyika iweke hapa Majlis tuisome.

Hapo chini nakuwekea namna wazee wangu walivyoliendea jambo hili la
kupigania uhuru.

Kila palipokuwa na ugumu walikaa kitako na kuomba dua:
''Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.''

Katika majiia hayo hapo juu nilifanya mahojiano na Sheikh Rashid Sembe na Mmaka Omari na hayo ndiyo waliyonieleza walipopanga mkakati wa Kura Tatu.

Ikiwa wewe una historia nyingine ya TANU na uhuru usisite kutuletea hapa ili sote tunufaike.
Soma historia ya Sheikh Rashid Sembe hapo chini:
Mohamed Said: SHEIKH ABDALLAH RASHID SEMBE: SHUJAA WA KURA TATU NA UAMUZI WA BUSARA WA TABORA
 
Mkuu, unapenda sana madua, kila kitu unahalalisha kwa dua. Kiwe heri au shari, unatanguliza dua kuhalalisha mbofu yako hiyo.

Mfano, umetangaza wazi kuwa walikuombea dua ili uoneshe historia inayowapendelea waislam. Kila kitu dua mzee hata kama haramu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma kisha useme walioachwa ni akina nani na utupe historia yao ya Uhuru. Halafu pia ukiona watu wametajwa au kuwekwa ambao hawakustahili basi utupe historia yao mbadala.

Yanini unaandikia mate na wino upo?
Maalim Faiza,
Waandike kutoka kwenye, ''source,'' ipi?
Hawana picha wala nyaraka hata moja.

Kwani pana ugumu gani?

Hawa hawana historia ndiyo maana wanaumwa sana ninapowaeleza
habari za wazee wangu na nini walifanya katika kuunda TANU na
kupigania uhuru wa Tanganyika.

Toka lini mtu akaeleza habari za babu yake wakaja watu wakakasirika?
Na wewe si ueleze habari za babu yako?

Hapo chini ni Dome Okochi Budohi ambae akinifahamu mimi toka
udogoni wakati yuko Dar es Salaam kabla hajakamatwa 1955 kwa
shutuma za kuwa Mau Mau.



Wamtazame hapa chini Budohi nini ilikuwa nafasi yake katika uongozi
wa TAA:

In June, TAA headquarters announced its executive committee with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1]

Budohi kadi yake ya TANU ni No. 6
Historia nzima ya Dome Budohi iko katika kitabu cha Abdul Sykes.

[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
 

Mzee Said Mohamed! wakati wa kupigania Uhuru wa Nchi hii hakuna Mtu aliyewaza kuhusu Imani yake na nafasi ya Imani yake katika kulikomboa taifa Hili! waislam,wakristo,wapagani,wahindu,wachawi walisimama pamoja kudai uhuru wa nchi hii.
Ungelijua UAMUZI WA BUSARA WA TABORA Ulifanyikia Wapi? usinge litaja abadani suala la Udini ulioung'ang'ania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…