Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Paskali,Historia yoyote inayoandikwa kutokana na simulizi ni historia ya mapokeo. Sisi wapenda simulizi, hupenda sana kusoma hadithi nzuri zinazosimuliwa na wasimulizi mahiri kama wewe Mkuu Maalim Mohamed Said, kiukweli simulizi zako ni mzuri. Kule mwanzo nilikuita mrongo, nikidhani urongo katika simulizi zako umeutunga wewe, but as days goes by, nimekuja ku realize, kumbe enda ikawa urongo hukutunga wewe, bali aliyekusimulia simulizi za urongo, hivyo wewe umeandika kile ulichosimuliwa ukidhani ndio ukweli, kumbe ulitanganywa na hao waliokusimulia.
Kwa vile wewe ni mzuri katika kufuatilia documentary evidence ya hicho ulichosimuliwa na ukweli unaujua, kwa vile maandishi yako ni maandishi ya a man with a mission, ( reffer
Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ...
) then nakuunga mkono endelea kuandika vile vile unavuoandika ili ile mission iwe accomplished. Naunga mkono kuandika kwa malengo na sio kujiandikia tuu, na nakiri mimi ni mmoja wa wafuasi wako wakubwa humu jf kwa vile natambua you have "the powers", kitu ambacho ninakiheshimu sana.
Endelea kutulisha kile ulicholishwa kwenye hizo simulizi, ingawa kuna urongo mwingi, lakini pia kuna ukweli mwingi, na kitu kikubwa kwangu sio urongo au ukweli wa makala zako, bali ni ilmu iliyomo ambayo kama sio wewe kutuandikia humu, akina sisi kama tusinge vifahamu visa vingi.
Asante kwa simulizi zako za hadith njoo, uwongo njoo utamu kolea.
Paskali.
Ndiyo ibra kubwa ya kitabu cha Abdul Sykes.
Lipo kundi maalum akili zao zinakataa kabisa kukubali kuwa hivi nilivyoeleza
ndivyo ilivyokuwa.
Sasa Paskali unathubutu kumwita baba yangu, babu yangu watu ambao toka
siku ya kwanza African Association inaanzishwa walikuwapo ni waongo.
Kuwa zipo nyaraka nimezisoma mimi na Iliffe kazisoma na kazifanyia rejea ni
uongo.
Ingekuwaje kama hizi nyaraka zisingekuwapo?
Unakataa kuwa Chief Kidaha Makwaia hakuwapo na Abdul hakumshawishi aje
TAA wamchague president waunde TANU?
Ukweli ni huo wa Chuo Cha Kivukoni walioandika historia ya TANU na kuwafuta
wazee wangu.
Miaka 20 kitabu toka kichwapwe na tunakwenda toleo la nne bado kitabu kipo
katika mjadala tukirudia yale kwa yale mumo kwa mumo.
Wala hutaki kujiuliza ni sifa ipi iliyapelekea Kleist na wanae waingie katika lile
kamusi la wazalendo wa Bara la Afrika - Dictionary of African Biography?
Iko siku nitakuhadithia mshtuko waliopata Harvard na Oxford University Press
nilipowapelekea mswada wa Kleist.
Tunaweza tukajikumbusha:
Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)