Wanajamvi kwa mujibu wa Mohamed, maswali yamejaa lugha ya kughadhabika na shari. Maswali ni hayo hapo juu, kama kuna mahali lipo tatizo naomba mtu anionyeshe kughadhabika au shari, nitaomba radhi.
Kama hakuna Mohamed maswali yapo wazi ndani ya mada na maudhui, jamvi linakusikiliza
Kwa mara ya kwanza kabisa, labda katika maisha yako yote, ni leo tu umepata ujasiri wa kuukiri ukweli...kwamba wakati unazaliwa ndio harakati za uhuru zinaanza. Zile hadithi za babu zako kuanza harakati za uhuru ni porojo tu ulizozitunga kwa malengo unayoyajua wewe tu. Ni uongo uliopitiliza kudai kwamba AA iliyoanzaishwa mwaka 1929 na Gavana wa wakati huo Cameroun kama klabu ya starehe kwa wasomi weusi ilikuwa na malengo ya kudai uhuru.Mimi nimezaliwa wakati ule harakati za uhuru zinaanza na wazee wangu walikuwa pale Gerezani walipokuwa wanaishi hawa watu akina Aziz Ally, Kleist Sykes, Omari Londo kuwataja wachache na walishiriki katika TANU.
Mag3,Kwa mara ya kwanza kabisa, labda katika maisha yako yote, ni leo tu umepata ujasiri wa kuukiri ukweli...kwamba wakati unazaliwa ndio harakati za uhuru zinaanza. Zile hadithi za babu zako kuanza harakati za uhuru ni porojo tu ulizozitunga kwa malengo unayoyajua wewe tu. Ni uongo uliopitiliza kudai kwamba AA iliyoanzaishwa mwaka 1929 na Gavana wa wakati huo Cameroun kama klabu ya starehe kwa wasomi weusi ilikuwa na malengo ya kudai uhuru.
Hilo la kwanza na pili ni ukweli kuwa wakati Nyerere anahudhuria mkutano mkuu wa AA akiwakilisha jimbo la Tabora wewe ulikuwa hujazaliwa. Na kwamba viongozi wa AA walikuwa hawamjui Mwalimu Nyerere kabla ya mwaka 1953 alipohamia Dar es Salaam pia ni uongo. Mtu ambaye yawezekana hakumjua Mwalimu Nyerere labda ni Abdul Sykes peke yake kwa sababu nyakati hizo hakuwepo...tunaanza kumsikia tu pale alipoongoza uvamizi wa ofisi za AA kuwatoa wazee wake!
Tatizo kubwa alilo nalo Mohamed Said ni kwamba tunapompinga kwa kukosoa hadithi zake, utetezi wake ni kuturejesha kwenye hadithi zile zile na porojo zile zile. Je mtuhumiwa kujitetea kwa ushahidi wa yale yale anayotuhumiwa nayo inaingia akilini kama si sawa tu na kuzidi kujitia kitanzi. Anapoweka picha zake ama za wazee wake kama ushahidi maana yake ni nini? Anapotumia ukurasa mzima kunukuu yale yale aliyoyaandika na tunayoyakosoa, anataka kufikisha ujumbe gani?
Maalim Faiza,Alama Mohamed Said, hebu tupe mkasa ule wa Nyerere kutaka kupinduliwa na jeshi, japo kwa uchache.
Mag3,
Mimi sina tatizo kabisa na yote niandikayo.
Ikiwa wewe unaona ni porojo na unaamini historia rasmi ya Chuo Cha Kivukoni,
mimi sina tatizo.
Wala sijakulazimisha kunisoma.
Ukiona bandiko langu lipite tu kwa mbali ujisalimishe na porojo.
Atakae atasoma wewe usiotaka utakuwa umesalimika.
Hili ni 'debunked' kwa kila kiwango."Mag3, post: 22924929, member: 10873"]
...Kuwa wakati Nyerere anahudhuria mkutano mkuu wa AA akiwakilisha jimbo la Tabora wewe ulikuwa hujazaliwa. Na kwamba viongozi wa AA walikuwa hawamjui Mwalimu Nyerere kabla ya mwaka 1953 alipohamia Dar es Salaam pia ni uongo.
Mtu ambaye yawezekana hakumjua Mwalimu Nyerere labda ni Abdul Sykes peke yake kwa sababu nyakati hizo hakuwepo...tunaanza kumsikia tu pale alipoongoza uvamizi wa ofisi za AA kuwatoa wazee wake!
Historia ya Abdul ipo miaka ya 1940 hadi 1953 kisha giza linatanda hadi 1968 wakati wa kifo chakeTatizo kubwa alilo nalo Mohamed Said ni kwamba tunapompinga kwa kukosoa hadithi zake, utetezi wake ni kuturejesha kwenye hadithi zile zile na porojo zile zile.
Amenimaliza jana wakati analeta ushahidi wa wajukuu wa wazee kama ndiyo facts. Kwamba, Wanzagi mjukuu wa Nyerere anakuwa shahidi wa Nyerere!Anapoweka picha zake ama za wazee wake kama ushahidi maana yake ni nini? Anapotumia ukurasa mzima kunukuu yale yale aliyoyaandika na tunayoyakosoa, anataka kufikisha ujumbe gani?
Mohamed alisema haya ni mambo nje ya mada, au unabisha?Alama Mohamed Said, hebu tupe mkasa ule wa Nyerere kutaka kupinduliwa na jeshi, japo kwa uchache.
Mohamed alisema haya ni mambo nje ya mada, au unabisha?
Nimekuelewa.Maalim Faiza,
Ningelikupa mkasa ule lakini kwa bahati nzuri nimehariri kitabu
ambacho mwandishi kazungumza kuhusu haya maasi.
Maadili yananikataza kusema chochote katika kitu ambacho
mkono wangu ulipita.
Ulimi uliponza kichwa wanasemaHebu Mag3, Nguruvi3, Yericko Nyerere na wale mnaofanana nao, tupeni historia za wazee wenu na mitaa yenu japo "kiduchu", nyie kufyonza tu ya Kariakoo? Makwenu vipi, hakukuwa na harakati za Uhuru?
Ahaa nimekuelewa. Kabla ya uhuru kuna kiporo cha 1953-1961 kukihusisha AMNUT na Abdul.Labda nimeuliza swali nje ya mada kwa kutaka mada ihamie baada ya uhuru, unabisha?
Mimi, kwa upande wangu nina matatizo sana na unayoyaandika...acha kupotosha jamii na maandishi ya kichochezi yaliyojaa simulizi zinazoweza kutumika kutugawa kwa namna yoyote ile. Wazee wetu wote walijitolea nafsi zao katika harakati za kudai uhuru bila kubaguana Kikabila, Kidini wala Kiutamaduni. Mbegu ambayo umeweza kuipandikiza na unayoendelea kuipandikiza lazima ipigwe vita na wote wanaoitakia mema nchi yetu.Mag3, Mimi sina tatizo kabisa na yote niandikayo.
Naam ni ya Kariakoo, ndipo kitovu cha harakati za Uhuru.Ulimi uliponza kichwa wanasema
''Tunaambiwa hii ni historia ya kweli ya harakati za kupigania Uhuru Tanganyika''
Wewe unatuambia ni Historia ya Kariakoo, ulimi bwana!
Aaa kwetu nitaanzia Kiwanda, KM7 , Magila Muheza, Mkanyageni , Lusanga, Pongwe hadi 'Ndanga' au Tanga kwa Sheikh Sembe.Naam ni ya Kariakoo, ndipo kitovu cha harakati za Uhuru.
Si tupe basi ya kwenu? Vipi, kama hakuna, sema tu hakuna.
Wewe ulisikia wapi Nyerere akifanya harakati za kudai uhuru butiama au na wazee wa butiama?
Hao wazee wanaotajwa kwenye harakati za uhuru karibia wote ni wa Dar, 90% wazee wetu wa Kariakoo. Nyerere mwenyewe alipokelewa na kuwekwa Kariakoo kwa kina Abdul Wahid Sykes.
Leta raha za kudai Uhuru kutokea kwenu.
Haya tupe ya Kariakoo...usidandie ya wahamiaji wa Gerezani (Wazulu na Wamanyema) tupe ya Kariakoo ya Watanganyika.Naam ni ya Kariakoo, ndipo kitovu cha harakati za Uhuru.
Siyo Nansio?Aaa kwetu nitaanzia Kiwanda, KM7 , Magila Muheza, Mkanyageni , Lusanga, Pongwe hadi 'Ndanga' au Tanga kwa Sheikh Sembe.
Historia itakuchoma moyo, ngoja tumalize hii ya ''Tanganyika'' unayotuthibitishia ni ya Kariakoo
Mimi, kwa upande wangu nina matatizo sana na unayoyaandika...acha kupotosha jamii na maandishi ya kichochezi yaliyojaa simulizi zinazoweza kutumika kutugawa kwa namna yoyote ile. Wazee wetu wote walijitolea nafsi zao katika harakati za kudai uhuru bila kubaguana Kikabila, Kidini wala Kiutamaduni. Mbegu ambayo umeweza kuipandikiza na unayoendelea kuipandikiza lazima ipigwe vita na wote wanaoitakia mema nchi yetu.
Katika harakati zozote zile lazima wawepo viongozi lakini lazima awepo kiongozi moja anayewaunganisha na sisi kama Watanganyika aliyeweza kutuunganisha pamoja katika harakati za kudai uhuru alikuwa ni moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na katika hilo hana mpinzani. Ingawa ni kweli na hao wengine nao walitoa michango yao naomba tusiwaangalie kwa dini zao bali kwa utaifa wao.
Kama binadamu utawapata wengi sana watakaoamini hizo ngano zako na kuzimeza mazima mazima lakini pia wapo wengi ambao watatusoma na sisi wengine na kusikiliza upande wa pili na kujiuliza maswali kama haya tunayoyauliza. Kwa kejeli zako kwa wazee wetu Watanganyika kwa ujumla wao lazima watauliza lengo lako hasa ni nini? Ujumbe gani uliotaka kuufikisha kwa Watanzania wa leo.
Hata tupe ya Kariakoo...usidandie ya wahamiaji wa Gerezani (Wazulu na Wamanyema) tupe ya Kariakoo ya Watanganyika.
Ungekiri hivyo kutoka mwanzo wala hatungekuwa na ugomvi wowote...ni historia ya wazee wako, period. Ugomvi unakuja pale unapoanza kudai ni historia ya Tanganyika!Mag3,
Narudia kusema kuwa sina tatizo na mawazo yako kuhusu historia hii.
Lengo langu ni kuihifadhi historia ya wazee wangu isipotee na nikiondoka
niache kumbukumbu ambayo itawasaidia waliokuwapo kujua nchi hii wapi
ilikotoka.