"Mag3, post: 22924929, member: 10873"]
...Kuwa wakati Nyerere anahudhuria mkutano mkuu wa AA akiwakilisha jimbo la Tabora wewe ulikuwa hujazaliwa. Na kwamba viongozi wa AA walikuwa hawamjui Mwalimu Nyerere kabla ya mwaka 1953 alipohamia Dar es Salaam pia ni uongo.
Mtu ambaye yawezekana hakumjua Mwalimu Nyerere labda ni Abdul Sykes peke yake kwa sababu nyakati hizo hakuwepo...tunaanza kumsikia tu pale alipoongoza uvamizi wa ofisi za AA kuwatoa wazee wake!
Hili ni 'debunked' kwa kila kiwango.
Vipi HQ hawakujua wanawasiliana na nani katika tawi, wakati huo wasomi wakihesabika kwa kiganja
Hoja ya Mohamed kuwa aliyemwingiza Nyerere katika siasa ni Abdul ni uongo.
Nyerere akiwa Makerere tayari alikuwa na mwamko wa siasa, achilia mbali kwenda masomoni Ulaya
Tatizo kubwa alilo nalo
Mohamed Said ni kwamba tunapompinga kwa kukosoa hadithi zake, utetezi wake ni kuturejesha kwenye hadithi zile zile na porojo zile zile.
Historia ya Abdul ipo miaka ya 1940 hadi 1953 kisha giza linatanda hadi 1968 wakati wa kifo chake
Miaka husika anairuka kwasababu ina mambo yanayopingana na ngano kwa ujumla wake
Utaelezaje miaka 7 bila kutaja AMNUT na Abdul Sykes ukihusisha na umaarufu na failure ya kuijenga AMNUT kwa kutumia watu wale wale aliokuwa nao?
Ni wazi, kwavile tangu 1953 hadi 1968 takribani miaka 15 Abdul haijulikani alifanya nini katika siasa.
Kuna sababu za kulaumu coverage ya msiba wake?
Anapoweka picha zake ama za wazee wake kama ushahidi maana yake ni nini? Anapotumia ukurasa mzima kunukuu yale yale aliyoyaandika na tunayoyakosoa, anataka kufikisha ujumbe gani?
Amenimaliza jana wakati analeta ushahidi wa wajukuu wa wazee kama ndiyo facts. Kwamba, Wanzagi mjukuu wa Nyerere anakuwa shahidi wa Nyerere!
Nilimuuliza kama Abdul alianzisha TANU ushahidi upo wapi?
Ukisoma kitabu na JF kuna sehemu anasema 'it's said that...' kwamba inasemekana ndiye mwasisi.
Mbele ya safari anashadidia akijua watu hawakuona maneno hayo na mantiki yake.
it's said ni presumption siyo fact
Kuna video aliweka ukimsikiliza anawaambia wasikilizaji, kabla ya mkutano wa Tabora Nyerere alimchukua ''X'' na kumwacha 'Z' kwenda kwa Sheikh Sembe Tanga.
Halafu anasema sababu za kumwacha 'Z' wasikilizaji watafute wenyewe.
Alichokwepa ni kutosema sababu za udini kwasababu hana ushahidi wa hilo
Anawaachia wasikilizaji waje na majibu akiwa ametengeneza mazingira ya majibu
Ninapumzika na uzi nisiwakoseshe watu fursa ya kufyonza