Ndugu zangu,
Vipi mtu ataniita mimi muongo wakati nimeandika mengi kutokana na utafiti
niliofanya kwa miaka mingi:
Mohamed, sina uhakika kama umeshawahi kumsikia mtu anaitwa James Watson.
Sifa zake unaweza kuzi-google. Kwa ufupi ni nguli Dunia wenyewe wakisema, eminent scientists,Nobel prize winner. Ana sifa za utafiti maabara si kama tourist
Miaka takribani kumi akiwa mtafiti nguli alieleza utafiti wake.
Wenzake walimhoji na kumzuia kushiriki shughuli katika maabara maarufu US na duniani
James aliomba radhi kwa jambo hilo
Kufanya utafiti hakuku 'exonerate' kutoka katika tabia za kawaida za binadamu.
Ukiwa mtafiti una inherent characters zisizotegemea kazi ufanyayo, ni za kibinadamu tu
Usichukue utafiti kama kinga ya tabia za kibinadamu ambazo kila mmoja anazo kwa namna tofauti kutokana na maumbile n.k.
Kuwa muongo ni matokeo ya kusema uongo.
Je, wanaosema wewe ni muongo wanakuonea?
Upo katika rekodi ukisema mwanzilishi wa AA likuwa Kleist.
Hili lilidumu hadi ilipothibitishwa na wanajamvi Cecil Matola na wenzake waliasisi chama , Matola akiwa Rais si Kleist!
Upo katika rekodi ukisema, alimwingiza Nyerere katika siasa ni Abdul Sykes!
Hili lilidumu hadi ilipothibitishwa kuwa Nyerere alianza siasa akiwa 'Kampala'
Aliandika barua ya kisiasa akiwa huko , kabla hajaonana na Abdul
Upo katika rekodi ukisema Nyerere alikutana na Abdu kwa mara ya kwanza alipokuja Dar 1950 na kwamba Abdul hakumjua kabla ya hapo
Ilionyeshwa kuwa Nyerere alihudhuria mkutano mwaka 1948 akiwa katibu wa tawi kubwa Tabora na alikutana na watu mashuhuri wa TAA. Abdul kutomjua haikuwa kweli
Ukasema aliyeunda TANU ni Abdul Sykes na sub committee iliyoandika katiba
TANU ikiundwa Rais alikuwa Nyerere, Abdul aliunda vipi?
Kwa mujibu wako TAA-Rais alikuwa Nyerere na Vice Pres Abdul, Kwamba, VP aliweza kubadili TAA kuwa TANU , President akiwa hajui!
Katiba ya TANU ilinukuliwa na aliyenukuu ni Nyerere si Abdul Klesit Sykes Mbuwane.
Orodha ni ndefu ikionyesha ima kwa bahati mbaya au kwa makusudia umesema yasiyo kweli kwa i.e uongo na atendae ni muongo
Kwa tukio moja unaweza kupewa benefit of doubt, kwa series ya matukio hiyo ni pattern na sijui wanaosema muongo wanakosea wapi! Je wanakosea kwasababu wewe ni mtafiti!