Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Historia yoyote inayoandikwa kutokana na simulizi ni historia ya mapokeo. Sisi wapenda simulizi, hupenda sana kusoma hadithi nzuri zinazosimuliwa na wasimulizi mahiri kama wewe Mkuu Maalim Mohamed Said, kiukweli simulizi zako ni mzuri. Kule mwanzo nilikuita mrongo, nikidhani urongo katika simulizi zako umeutunga wewe, but as days goes by, nimekuja ku realize, kumbe enda ikawa urongo hukutunga wewe, bali aliyekusimulia simulizi za urongo, hivyo wewe umeandika kile ulichosimuliwa ukidhani ndio ukweli, kumbe ulitanganywa na hao waliokusimulia.

Kwa vile wewe ni mzuri katika kufuatilia documentary evidence ya hicho ulichosimuliwa na ukweli unaujua, kwa vile maandishi yako ni maandishi ya a man with a mission, ( reffer
Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ...
) then nakuunga mkono endelea kuandika vile vile unavuoandika ili ile mission iwe accomplished. Naunga mkono kuandika kwa malengo na sio kujiandikia tuu, na nakiri mimi ni mmoja wa wafuasi wako wakubwa humu jf kwa vile natambua you have "the powers", kitu ambacho ninakiheshimu sana.

Endelea kutulisha kile ulicholishwa kwenye hizo simulizi, ingawa kuna urongo mwingi, lakini pia kuna ukweli mwingi, na kitu kikubwa kwangu sio urongo au ukweli wa makala zako, bali ni ilmu iliyomo ambayo kama sio wewe kutuandikia humu, akina sisi kama tusinge vifahamu visa vingi.

Asante kwa simulizi zako za hadith njoo, uwongo njoo utamu kolea.

Paskali.
Hahahaaa Paskali you killed....
 
Kaka Mohamed Said Hawezi kubadilika kwenye hayo masuala ya kutetea Dini yake, yeye anaandika hiyo historia akiwa na lengo kuu la kutetea dini yake, wala usijisumbue kumshauri chochote, humu ndani ya JF hakuna mwenye uwezo wa kumshauri, yeye ndio Alfa na Omega

Kuhusu Yericko, kweli anaonekana ni mwenye nia hasa ya kuandika na kufika mbali, ana shida kubwa ya kutokuwa na wigo mpana wa kuelewa mambo kwa kina, anajua vitu vingi kwa juju juu tu, hafanyi utafiti wa kina, akijirekebisha mapungufu machache hayo anaweza kuwa mtunzi au mwandishi mzuri
Mkuu unatoa majibu kitabu hata kukisoma hujakisoma?
 
UTANGULIZI

Naam. Ili mtu awe Afisa wa Idara ya Ujasusi yampasa awe mwenye akili zilizotulizana. Yaani, razini. Ndipo basi, pasi na kutafuna maneno, kitabu hiki ni mahususi hususan kwa wasomaji weledi. Kitabu hiki ni motifu, kinachoangazia masuala umuhimu ya ujasusi na jinsi yalivyo ya kipekee, kikitilia uzito umuhimu wake katika maisha ya wanadamu. Kutokana na upekee huo, taaluma ya ujasusi itumike kuleta ustawi katika jamii badala ya kudhuru kama ambavyo mashirkika mbalimbali ya ujasusi yamekuwa yakifanya kwa njia moja au nyingine, hii au ile. Ama kitabu hiki kinakusudiwa kutoa mwanga wa jinsi taaluma hiyo inavyopasa kuendeshwa pamoja na kuonesha uhalisia wa utendaji wake, kinyume na ilivyo kwa baadhi ya mashirika ambapo sasa imefikia hatua jasusi, kachero au afisa usalama kutangaza hadharani, “Unanijua mimi nani? Mimi ndimi, afisa usalama. Sichezewi!” Kwa lengo duni, ili kuwatisha watu kwa sifa za Mfalme Juha.

Mintarafu, kitabu hiki ni bashraf kwa baadhi ya mataifa yanayoendelea kuhusiana na suala zima la ujasusi, mathalani ujasusi wa kidola wa Idara ya Usalama wa Taifa la Tanzania (TISS) na Ujasusi wa Kimataifa unaofanywa na mashirika kama MOSSAD la Israel katika harakati zake za kutimiza dhamira ya kutawala eneo zima la Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla. Zaidi ya hayo, kitabu hiki kinatoa maarifa pevu ya kijasusi ili kuelewa misingi ya ujasusi na umuhimu wake pamoja na kukamilisha shughuli zake mbali mbali. Mathalani kuna Ujasusi wa Kiushindani (Competitive Intelligence) ambao zaidi hutumika katika ulimwengu wa biashara na harakati waweza kuainishwa kama utaratibu wa kiufundi wa kupata habari nyeti za biashara na harakati za malengo, wateja, washindani, maadui, teknolojia na mazingira ya jumla ya harakati na biashara. Habari hizi zaweza kutoka kwa mtu yeyote au vyanzo vyovyote katika eneo husika.

Ujasusi unatajwa kama ni taaluma ya pili kongwe duniani. Yaani, ulikuwapo tangu utanguni, ulimwengu ulipopata maarifa. Mashujaa katika vita vya kale wanasema kuwa ujasusi ni sehemu muhimu ya kimkakati, wakati wa vita. Kinachomuwezesha kamanda hodari kushambulia, kuteka na kufanya mambo yasiyo ya kawaida, yaliyo nje ya uwezo wa kawaida, ni ule ujuzi anaokuwa nao kabla ya pambano lenyewe. Na, ujuzi huo anaokuwa nao kabla, hautokani na uzoevu ama uhodari wa kufanya mahesabu, bali unatokana na taarifu za siri za adui ambazo hupatikana kutoka kwa watu wengine.

Aidha, ujasusi umekuwa sehemu muhimu ya taasisi za kijeshi na kibiashara. Na pia, ujasusi ulikuwa na hadi leo umekuwa ni chachu ya harakati za Kanisa Katoliki. Punde taarifu zinapopatikana, husambazwa kwa usahihi na kwa wakati kwa watoaji maamuzi wa ngazi zote. Ujasusi wa Kiushindani (Competeteve Intelligence) ni ujasusi unaoshughulika zaidi na harakati za kibiashara ambao unatofautiana kidogo na ule wa serikali. Hata hivyo, serikali pia huuwa na idara ya ujasusi wa kibiashara. Ujasusi wa Kiushindani unafuata taratibu na maadili ya biashara ambayo hayafuatwi na taasisi za ujasusi unaohami serikali. Ujasusi wa Kiushindani haufanywi chini ya mwavuli wa kidiplomasia bali, una lengo zaidi la kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuimarisha huduma na kukabili mikikimikiki ya ulimwengu kwa ajili ya kujipatia faida na ufanisi wa shughuli husika. Kadhalika, Ujasusi wa Kiushindani unatofautiana na ukachero mwingine wa kiserikali ambao huweza kukiuka au kupuuza sheria na taratibu za wengine.

Nyuma ya pazia, mara nyingi, ujasusi hautazamwi kwa wema. Badala yake, ujasusi umeonekana kama shughuli isiyo na uhalali wa kimaadili au utu. Kwa ajili hiyo, kitabu hiki kinatoa changamoto kwa wajuzi na wajuvi wa taaluma hiyo, washiriki na watu wa kawaida kuonesha iwapo fani ya ujasusi itafanywa kitaalamu, inaweza kuwa ya muhimu kwa kurejea mifano ya wakongwe hasa MOSSAD (Israeli), CIA (Marekani), KGB (Urusi), M16 (Uingrereza) na wengineo, wameweza kutawala nyanja hio na kuweza kudhibiti kila sehemu kwa minajili ya kulinda na kuendeleza maslahi yao sehemu mbali mbali duniani.
Wataalamu wa ujasusi wa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939-1945), wametoa tafsiri nyingi kuhusiana na neno ujasusi. Licha ya tafsiri hizo, tafsiri ambayo pengine yaweza kukubalika na wote ni inayoafanua ujasusi kama shughuli za uchunguzi wa mambo mbalimbali kwa njia za kificho, mienendo na harakati za siri za usakaji wa habari au nyaraka muhimu na za uhakika kuhusu watu na matendo yao, yaliyo ya dhahiri na ya uficho, yanayoyafanywa dhidi ya watu wengine, serikali, jumuiya, taasisi, nchi, taifa, kabila, biashara au maslahi ya wengine. Kwa upande mwingine, kitaaluma, ujasusi ni ufundi wa kunasa taarifu au uwezo wa kupata taarifu nyingi kutoka vyanzo tofauti zenye kulenga kuhami, kushambulia kwa ufanisi zaidi, na kuangamiza adui ni shughuli za kimyakimya zenye malengo mazuri au mabaya kwa maslahi ya mtu, kundi, jumuiya, taasisi au Serikali.

Kwa tafsiri ya kiutendaji, ujasusi ni ukusanyaji na uchambuzi wa data na taarifu zinazotoka katika chanzo chochote kile (iwe kwa mtu au chombo). Taarifu hizo huwa zenye mitazamo ya mbali na zinazotoa taswira ya dhamira, nguvu, harakati na athari au matokeo yanayoelekea kutokea. Shughuli za kijasusi ni muhimu katika maisha ya kila siku ya ulimwengu huu wenye matukio mengi.

Tanbihi: Upelelezi/Ushushu/Ukachero ama Ujasusi kamili, usiishie ndani ya vyombo vya Ulinzi na Usalama tu mathalani Jeshi la JWTZ, Usalama wa Taifa, Polisi, Magereza na Uhamiaji tu, bali uende mbali zaidi kama Vyuoni au kwenye kampuni mbalimbali kunatakiwa kuwe na wapelelezi; mashirika ya umma yanatakiwa kuwa na wapelelezi, viwanda vya ndani vinatakiwa kuwa na wapelelezi na wote hawa wanatakiwa kufanya kazi pamoja ili kuleta maendeleo kwa jamii ya watu wao hasa Watanzania. Nchi zenye maendeleo yaliyotia fora, zinaendelea na kuendeleza ushindani mkubwa kwenye nyanja hii. Mathalani, Taifa la Jamhuri ya Watu wa China, lilianzisha utaratibu wa kupeleka wapelelezi nchi nyingi duniani ili wakadukue na kuiba teknolojia/tunduizi na maarifa kuzileta kwao. Hivi sasa, China wana mafanikio makubwa sana si tu kwenye teknolojia bali na kwenye vitivo vingine. Mfano mwingine unaturejesha wakati wa Vita Kuu Pili ya Dunia ambapo Marekani waliiba wanasayansi wengi wa Ujerumani ambao walikuja kusaidia kujenga uwezo mkubwa wa jeshi lao na taasisi nyingine. Kwa ujanja huo, Marekani limekuwa taifa lenye nguvu duniani kwa kipindi kirefu.

Tunapaswa kukumbuka kazi za ujasusi ni ngumu na zenye siri nyingi na kubwa sana. Majasusi wengi pia wana mafunzo ya kujilinda, kupambana, kushambulia na kufisha maisha. Tendo la kufisha katika medani za kijasusi ni tendo la hitimisho katika misheni au zoezi lolote lile ikiwa kutakuwa na ulazima huo na halina kinga ya kisheria wala msingi wa huruma ya kiutu. Muhimu ni kuwa kufisha huwa ni kwa maslahi ya Taifa.

Kwa kuhitimisha, ujasusi hautumiki kutafuta taarifu mbaya tu. La hasha. La mara elfu la. Kuna taarifu nyingi nzuri zinazoweza kutumika Vyuoni au Ndakini, Wizarani, jeshini na sehemu nyingine kwa minajili ya kuimarisha au kujenga zana na vifaa vya kisasa katika utandawazi wa dunia mpya..............

Kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, hapa tatizo ni lugha tuu na tafsiri kati watu wanaoitwa waasisi na waanzilishi viongozi na mashujaa.

Kama AA iliasisiwa mwaka 1927 na rais wa kwanza ni Cecil Matola, Sykes akaupokea urais baada ya kifo cha Matola, kumtaja Skykes kuwa ndio mwasisi wa AA bila kumtaja Matola, huu ni urongo!.

Kama Mwaka 1948, AA iligeuka, kuwa TAA chini ya rais Dr. Vedastus Kyaruzi, Skykes kumtaja alikaimu tuu baada ya Dr. Kyaruzi kuhamishwa na 1953 aligombea na Mwl. Julius Nyerere akambwagwa vibaya, ni Nyerere ndie aliyeibadili TAA kuigeuza TANU, hivyo kama ni ushujaa, shujaa wa TAA ni Dr. Kyaruzi, chini ya hapo ni urongo!. Na shujaa wa TANU ni Nyerere, chini ya hapo ni urongo na shujaa wa Uhuru wa Tanganyika ni Nyerere, chini ya hapo ni urongo.

Kama lengo ni kutaja waasisi wa wazo, au mashujaa wa uhuru, then wote waliouhusika tangu wazo, watakuwa ni wanachama waanzishilishi na mashujaa, ila kila mahali shujaa mkuu ni mmoja tuu na sii Sykes popote tangu AA, TAA, TANU hadi Uhuru.

Ukiahadithiwa kisa cha urongo katika fasihi simulizi, na wewe ukauandika urongo ule katika fasihi andishi, mrongo ni sii wewe uliyeandika urongo, bali yule aliyekusimulia urongo!.

Ukweli na urongo katika fasihi simulizi ni very relative kama ilivyo imani ya dini za watu, watu wakiaminishwa dini fulani ndio dini ya ukweli dini nyingine zote ni za urongo, hivyo katika kujenga religious tolerance, tunafunza tuhubiri dini zetu tuu tunazoziamini bila kuwaeleza wengine wenye dini zao kuwa ni dini za urongo, hivyo ingekuwa hayo unayoyaandika kuhusu historia ya uhuru, ingekuwa unaandika juzuu, tusingesema lolote, lakini maadamu ni historia na sio dini, huwezi kuandika urongo, halafu kuna wanaoujua ukweli wakanyamaza, ila pia pia kuna kundi la akina sisi wapenda hadithi, hata kama tunajua tunadanganywa, maadam msimulizi ni hodari wa kusimulia, tunaona raha kusoma simulizi zake, tunajifunza mengi tusiyoyajua kuhusu simulizi hizo, japo simulizi nyingine ni za urongo, lakini watu humu tunaelimika,

Hivyo Maalim Mohamed Said endelea na simulizi za hadithi hadithi, uwongo njoo utamu kolea, tunafurahia!.

Paskali
Paskali umeongea mazito sana na kukandamiza kisu mfupani... Jambo hilo mzee wetu hapendi kabisa kulisikia,
 
Mag3,
Yericko
si makamo yangu kabisa.
Wewe unajua, yeye anajua na dunia nzima inajua.

Kama unafuatilia vizuri nadhani utaona ninapomwandikia na kumwekea
majibu ya maswali yake huwa harejei tena nyuma.

Mimi kwa ustaarabu huwa simkumbushi arejee kwani kufanya hivyo ni
kuleta ubishani.

Huwa nachukulia ukimya wake kuwa kajifunza kitu na huu ndiyo mtindo
wangu.

Maalim Haruna alikuwa akitufunza anasema mwanachuoni kalamu yake
haifedheheshi bali inasomesha.

Ukiandika lazima utakosolewa hili ni jambo la kawaida na mimi sikatai
kukosolewa khasa ukichukulia kuwa kazi yoyote ya binadamu lazima
itakuwa na makosa.
Nakupeni hapa utangulizi wa kitabu kinachotuweka kwenye mjadala huu....

UTANGULIZI

Naam. Ili mtu awe Afisa wa Idara ya Ujasusi yampasa awe mwenye akili zilizotulizana. Yaani, razini. Ndipo basi, pasi na kutafuna maneno, kitabu hiki ni mahususi hususan kwa wasomaji weledi. Kitabu hiki ni motifu, kinachoangazia masuala umuhimu ya ujasusi na jinsi yalivyo ya kipekee, kikitilia uzito umuhimu wake katika maisha ya wanadamu. Kutokana na upekee huo, taaluma ya ujasusi itumike kuleta ustawi katika jamii badala ya kudhuru kama ambavyo mashirkika mbalimbali ya ujasusi yamekuwa yakifanya kwa njia moja au nyingine, hii au ile. Ama kitabu hiki kinakusudiwa kutoa mwanga wa jinsi taaluma hiyo inavyopasa kuendeshwa pamoja na kuonesha uhalisia wa utendaji wake, kinyume na ilivyo kwa baadhi ya mashirika ambapo sasa imefikia hatua jasusi, kachero au afisa usalama kutangaza hadharani, “Unanijua mimi nani? Mimi ndimi, afisa usalama. Sichezewi!” Kwa lengo duni, ili kuwatisha watu kwa sifa za Mfalme Juha.

Mintarafu, kitabu hiki ni bashraf kwa baadhi ya mataifa yanayoendelea kuhusiana na suala zima la ujasusi, mathalani ujasusi wa kidola wa Idara ya Usalama wa Taifa la Tanzania (TISS) na Ujasusi wa Kimataifa unaofanywa na mashirika kama MOSSAD la Israel katika harakati zake za kutimiza dhamira ya kutawala eneo zima la Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla. Zaidi ya hayo, kitabu hiki kinatoa maarifa pevu ya kijasusi ili kuelewa misingi ya ujasusi na umuhimu wake pamoja na kukamilisha shughuli zake mbali mbali. Mathalani kuna Ujasusi wa Kiushindani (Competitive Intelligence) ambao zaidi hutumika katika ulimwengu wa biashara na harakati waweza kuainishwa kama utaratibu wa kiufundi wa kupata habari nyeti za biashara na harakati za malengo, wateja, washindani, maadui, teknolojia na mazingira ya jumla ya harakati na biashara. Habari hizi zaweza kutoka kwa mtu yeyote au vyanzo vyovyote katika eneo husika.

Ujasusi unatajwa kama ni taaluma ya pili kongwe duniani. Yaani, ulikuwapo tangu utanguni, ulimwengu ulipopata maarifa. Mashujaa katika vita vya kale wanasema kuwa ujasusi ni sehemu muhimu ya kimkakati, wakati wa vita. Kinachomuwezesha kamanda hodari kushambulia, kuteka na kufanya mambo yasiyo ya kawaida, yaliyo nje ya uwezo wa kawaida, ni ule ujuzi anaokuwa nao kabla ya pambano lenyewe. Na, ujuzi huo anaokuwa nao kabla, hautokani na uzoevu ama uhodari wa kufanya mahesabu, bali unatokana na taarifu za siri za adui ambazo hupatikana kutoka kwa watu wengine.

Aidha, ujasusi umekuwa sehemu muhimu ya taasisi za kijeshi na kibiashara. Na pia, ujasusi ulikuwa na hadi leo umekuwa ni chachu ya harakati za Kanisa Katoliki. Punde taarifu zinapopatikana, husambazwa kwa usahihi na kwa wakati kwa watoaji maamuzi wa ngazi zote. Ujasusi wa Kiushindani (Competeteve Intelligence) ni ujasusi unaoshughulika zaidi na harakati za kibiashara ambao unatofautiana kidogo na ule wa serikali. Hata hivyo, serikali pia huuwa na idara ya ujasusi wa kibiashara. Ujasusi wa Kiushindani unafuata taratibu na maadili ya biashara ambayo hayafuatwi na taasisi za ujasusi unaohami serikali. Ujasusi wa Kiushindani haufanywi chini ya mwavuli wa kidiplomasia bali, una lengo zaidi la kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuimarisha huduma na kukabili mikikimikiki ya ulimwengu kwa ajili ya kujipatia faida na ufanisi wa shughuli husika. Kadhalika, Ujasusi wa Kiushindani unatofautiana na ukachero mwingine wa kiserikali ambao huweza kukiuka au kupuuza sheria na taratibu za wengine.

Nyuma ya pazia, mara nyingi, ujasusi hautazamwi kwa wema. Badala yake, ujasusi umeonekana kama shughuli isiyo na uhalali wa kimaadili au utu. Kwa ajili hiyo, kitabu hiki kinatoa changamoto kwa wajuzi na wajuvi wa taaluma hiyo, washiriki na watu wa kawaida kuonesha iwapo fani ya ujasusi itafanywa kitaalamu, inaweza kuwa ya muhimu kwa kurejea mifano ya wakongwe hasa MOSSAD (Israeli), CIA (Marekani), KGB (Urusi), M16 (Uingrereza) na wengineo, wameweza kutawala nyanja hio na kuweza kudhibiti kila sehemu kwa minajili ya kulinda na kuendeleza maslahi yao sehemu mbali mbali duniani.
Wataalamu wa ujasusi wa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939-1945), wametoa tafsiri nyingi kuhusiana na neno ujasusi. Licha ya tafsiri hizo, tafsiri ambayo pengine yaweza kukubalika na wote ni inayoafanua ujasusi kama shughuli za uchunguzi wa mambo mbalimbali kwa njia za kificho, mienendo na harakati za siri za usakaji wa habari au nyaraka muhimu na za uhakika kuhusu watu na matendo yao, yaliyo ya dhahiri na ya uficho, yanayoyafanywa dhidi ya watu wengine, serikali, jumuiya, taasisi, nchi, taifa, kabila, biashara au maslahi ya wengine. Kwa upande mwingine, kitaaluma, ujasusi ni ufundi wa kunasa taarifu au uwezo wa kupata taarifu nyingi kutoka vyanzo tofauti zenye kulenga kuhami, kushambulia kwa ufanisi zaidi, na kuangamiza adui ni shughuli za kimyakimya zenye malengo mazuri au mabaya kwa maslahi ya mtu, kundi, jumuiya, taasisi au Serikali.

Kwa tafsiri ya kiutendaji, ujasusi ni ukusanyaji na uchambuzi wa data na taarifu zinazotoka katika chanzo chochote kile (iwe kwa mtu au chombo). Taarifu hizo huwa zenye mitazamo ya mbali na zinazotoa taswira ya dhamira, nguvu, harakati na athari au matokeo yanayoelekea kutokea. Shughuli za kijasusi ni muhimu katika maisha ya kila siku ya ulimwengu huu wenye matukio mengi.

Tanbihi: Upelelezi/Ushushu/Ukachero ama Ujasusi kamili, usiishie ndani ya vyombo vya Ulinzi na Usalama tu mathalani Jeshi la JWTZ, Usalama wa Taifa, Polisi, Magereza na Uhamiaji tu, bali uende mbali zaidi kama Vyuoni au kwenye kampuni mbalimbali kunatakiwa kuwe na wapelelezi; mashirika ya umma yanatakiwa kuwa na wapelelezi, viwanda vya ndani vinatakiwa kuwa na wapelelezi na wote hawa wanatakiwa kufanya kazi pamoja ili kuleta maendeleo kwa jamii ya watu wao hasa Watanzania. Nchi zenye maendeleo yaliyotia fora, zinaendelea na kuendeleza ushindani mkubwa kwenye nyanja hii. Mathalani, Taifa la Jamhuri ya Watu wa China, lilianzisha utaratibu wa kupeleka wapelelezi nchi nyingi duniani ili wakadukue na kuiba teknolojia/tunduizi na maarifa kuzileta kwao. Hivi sasa, China wana mafanikio makubwa sana si tu kwenye teknolojia bali na kwenye vitivo vingine. Mfano mwingine unaturejesha wakati wa Vita Kuu Pili ya Dunia ambapo Marekani waliiba wanasayansi wengi wa Ujerumani ambao walikuja kusaidia kujenga uwezo mkubwa wa jeshi lao na taasisi nyingine. Kwa ujanja huo, Marekani limekuwa taifa lenye nguvu duniani kwa kipindi kirefu.

Tunapaswa kukumbuka kazi za ujasusi ni ngumu na zenye siri nyingi na kubwa sana. Majasusi wengi pia wana mafunzo ya kujilinda, kupambana, kushambulia na kufisha maisha. Tendo la kufisha katika medani za kijasusi ni tendo la hitimisho katika misheni au zoezi lolote lile ikiwa kutakuwa na ulazima huo na halina kinga ya kisheria wala msingi wa huruma ya kiutu. Muhimu ni kuwa kufisha huwa ni kwa maslahi ya Taifa.

Kwa kuhitimisha, ujasusi hautumiki kutafuta taarifu mbaya tu. La hasha. La mara elfu la. Kuna taarifu nyingi nzuri zinazoweza kutumika Vyuoni au Ndakini, Wizarani, jeshini na sehemu nyingine kwa minajili ya kuimarisha au kujenga zana na vifaa vya kisasa katika utandawazi wa dunia mpya.
 
Mzee Said Mohamed! wakati wa kupigania Uhuru wa Nchi hii hakuna Mtu aliyewaza kuhusu Imani yake na nafasi ya Imani yake katika kulikomboa taifa Hili! waislam,wakristo,wapagani,wahindu,wachawi walisimama pamoja kudai uhuru wa nchi hii.
Ungelijua UAMUZI WA BUSARA WA TABORA Ulifanyikia Wapi? usinge litaja abadani suala la Udini ulioung'ang'ania.
Na kwakuongeza nikuwa chama cha AA kiliundwa kwa msaada wa Gavana wa kiingereza Sir D. Cameroun
 
AA iliasisiwa 1929.

Msome Kleist anaeleza kila kitu vipi aliasisi AA 1929 baada ya kukutana
na Dr. Aggrey 1924.

Cecil Matola hakukaa sana katika AA alifariki 1933 na President akawa
Mzee bin Sudi.
Kaasisi Kleist baada ya kukutana na Dr Aggrey!
Halafu kamchukua Cecil Matola kuwa Rais bila kushiriki uasisi

Tuendelee
 
Yericko mtakuwa mnazunguka hapo hapo kwenda na kurudi. Nimekuwekeeni mambo mengi ya historia yaliyopitika kati ya 1947 - 1950 mambo ambayo yaliyomfanya Abdul Sykes aingie katika uongozi wa TAA na Dr. Kyaruzi 1950 tena kwa msaada wa Schneider Abdillah Plantan ambae yeye kwake ni baba na anaetolewa madarakani kwa mapinduzi ni Mwalimu Thomas Saudtz Plantan na Clement Mohamed Mtamila. Mtoto wa Mzee Mtamila, Happy alikuwa Ulaya kwa miaka mingi sana na mwaka jana aliporudi alifika nyumbani kwangu kunishukuru jinsi nilivyorekebisha history ya TANU. Huyu Mzee Mtamila ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU 1955 na barua ya Father Walsh aliyomwandikia Nyerere baada ya kurejea UNO, Nyerere aliipeleka kwake na ikajadiliwa nyumbani kwake Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Kleist). Nyinyi mnaiogopa historia hii mmekwama na Cecil Matola 1933. Mimi sina shida na mnavyopenda kuamini lakini muhimu tusonge mbele. Mkasa wa Abdul Sykes, Hamilton na Barakat katika, "labour movement," na damu iliyomwagika nyie kwenu si historia muhimu. Wakati haya yakifanyika Dar es Salaam babu yangu Salum Abdallah alikuwa akiongoza mgomo wa Tanganyika Railway Tabora. Ndipo ninaposema mimi naijua historia hii ya TANU kwani chimbuko la chama hiki ni wazee wangu. Kitabu kipo miaka 20 bado kinajadiliwa usiku na mchana na hakuna aliyekuja na kitabu kingine kuhusu TANU. Tunakisubiri In Shaa Allah kitabu cha Jopo la Prof. Shivji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ritz uwanja uko kimya...
Kamsome Mag3 na kumbu kumbu alivyovuta 2011. Hakuna jipya unaloeleza isipokuwa majigambo. Nani ana interest na wewe kula na wazungu? Nani ana interest ya nukuu moja kwa maandishi mekundu yasiyo na maana!
Kuna nyakati tofauti inakuwa muhimu baina yetu

Ukitualika tutakuja, ni uungwana. Tuanze na hapa chini halafu tutareja katika viporo

Wanajamvi, kama mnamsoma vizuri Mohamed, anasema mwasisi wa TANU ni Abdul. Anasema hayo baada ya kushindwa kueleza nani aliandika katiba ya TANU

Hili la Uasisi kutoka kwa Abdul hana uhakika nalo! amesikia.
Muulizeni aweke ushahidi hapa jamvini. Narudia hana ushahidi amesikia na huo si ushahidi wala fact

Halafu harakati zote zinaishia kuundwa kwa TANU. Muulizeni nani aliunda AMNUT na kwanini haikupata mafanikio

Kuna sababu kwanini historia inaanzia 1929 hadi 1953! Heiendelei. Muulizeni kwanini
 
Yericko,
Paskali...hapana hawezi.
Kitabu changu kimefurtu ada.

Mwaka wa ngapi nimesimama na nyie hapa?

Nyie mnauliza maswali na mie ndiye msomeshaji.

Mliyajua haya kabla ya mimi kuandika? Ila inanishangaza hii chuki katika uandishi wenu. Hii historia imewauma sana. Mngependelea tubakie na historia ya Chuo Cha Kivukoni.

Lakini usomi ndiyo ulivyo kuwa kitabu kinarekebisha kitabu.

Nyie badala ya kumtafuta mwandishi na kugombananae mlitakiwa muandike kitabu kusahihisha, "uongo," wangu si kuandika kejeli na kuleta chuki na hasad.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unatoa majibu kitabu hata kukisoma hujakisoma?
Mathalani embu tuichambue hii picha hapa chini.
Hii picha wewe umeikopi kutoka sehemu na wala sio kitu kibaya kwani kwenye mwaka huo wa 1930 haukuwepo, lakini kwenye hii maada hoja yako unajaribu kuonyesha uhalisia wa nani hasa walikuwa waanzilishi wa AA na kikubwa kabisa ni kuonyesha umuhimu na ushiriki mkubwa wa Cecil Matola, swali la msingi kwenye hiyo picha Cecil Matola yupo wapi?, maana alikufa 1933 na hiyo picha ni ya 1930, lakini badala yake picha ina maelezo ya jina moja tu la Mr Kleist Sykes, kwa kukosa kwako umakini unazidi kuuonyesha umma kuwa Kleist Sykes ndio Baba wa hiyo AA na wala sio Matola kwani hajatajwa hapo, na shida kubwa umeikopi picha kutoka kwa mtu anawewadunisha Wapigania haki na uhuru wa mtu mweusi wote na kuwainua wazee wake wa Kariakoo na Dar ya Zamani wakina Sykes at el..

Hebu kwa ueledi wako tuonyeshe Cecil Matola kwenye hii picha

image.jpg
 
Ntamaholo,
Ikiwa unayo historia ya AICT katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa
Tanganyika iweke hapa Majlis tuisome.

Hapo chini nakuwekea namna wazee wangu walivyoliendea jambo hili la
kupigania uhuru.

Kila palipokuwa na ugumu walikaa kitako na kuomba dua:
''Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.''

Katika majiia hayo hapo juu nilifanya mahojiano na Sheikh Rashid Sembe na Mmaka Omari na hayo ndiyo waliyonieleza walipopanga mkakati wa Kura Tatu.

Ikiwa wewe una historia nyingine ya TANU na uhuru usisite kutuletea hapa ili sote tunufaike.
Soma historia ya Sheikh Rashid Sembe hapo chini:
Mohamed Said: SHEIKH ABDALLAH RASHID SEMBE: SHUJAA WA KURA TATU NA UAMUZI WA BUSARA WA TABORA

Hivi hao Waislam wote na Watoto wa Mzizima, iweje waangaike na Nyerere wa Kuja, tena Mkristo? Je Hiyo nafasi ilikuwa ya kina Syskes na Nyerere kaja kuwapokonya?
Yaani unajitahidi mno kumdunisha Nyerere lakini logic na ukweli zinagoma kabisa
 
In June, TAA headquarters announced its executive committee with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1]

[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

Mbona hii executive committee ya TAA ya 1953 imejaa Wakristo tu?, Wazee wetu wako wapi?
 
Hivi hao Waislam wote na Watoto wa Mzizima, iweje waangaike na Nyerere wa Kuja, tena Mkristo? Je Hiyo nafasi ilikuwa ya kina Syskes na Nyerere kaja kuwapokonya?
Yaani unajitahidi mno kumdunisha Nyerere lakini logic na ukweli zinagoma kabisa
Kituko,
Mimi nitakuwa mjinga ikiwa nitamdunisha Nyerere na heshima yangu
itaondoka.

Yapo mengi huyajui katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Hapaja kuwa na tatizo la kuporana nafasi na mfano wa hayo.

Pita kote katika historia hii hili hutalikuta popote.

Kabla ya Abdul kufahamiana na Nyerere Dar es Salaam, Abdul
alimshawishi Chief Kidaha David Makwaia kujiunga na TAA
wamchague president kisha waunde TANU.

French Institute for Research in Africa, Nairobi walifanya seminar
kuadhimisha uhuru wa Afrika, (Fiftieth Anniversary of the African
Independences) mwaka wa 2014 na nilialikwa kutoa, ''paper.''

Nakuwekea hapa, ''link,'' ya paper hiyo chukua muda uisome bila
shaka utaelewa nini kilitokea baada ya uhuru:
Mohamed Said: TANZANIA: A NATION WITHOUT HEROES (ZMO) BERLIN
 
Kituko,
Mimi nitakuwa mjinga ikiwa nitamdunisha Nyerere na heshima yangu
itaondoka.

Yapo mengi huyajui katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Hapaja kuwa na tatizo la kuporana nafasi na mfano wa hayo.

Pita kote katika historia hii hili hutalikuta popote.

French Institute for Research in Africa, Nairobi walifanya seminar
kuadhimisha uhuru wa Afrika, (Fiftieth Anniversary of the African
Independences) mwaka wa 2014 na nilialikwa kutoa, ''paper.''

Nakuwekea hapa, ''link,'' ya paper hiyo chukua muda uisome bila
shaka utaelewa nini kilitokea baada ya uhuru:
Mohamed Said: TANZANIA: A NATION WITHOUT HEROES (ZMO) BERLIN

Kaka hiyo nafasi aliyopewa Nyerere kweli ilimstahiki?, kwa nini Mkristo wa kuja apewe hiyo heshima? Yeye alikuwa na nini cha zaidi kuliko watoto wa Mjini waliompokea na "kumfundisha" Kiswahili
 
Bahati mbaya umechelewa sana katika mjadala huu.

Haya maswali yako yote nimeyajibu hapa siku za nyuma na katika
kitabu nimeeleza sifa za Nyerere kuenea katika uongozi wa juu
katika TAA kisha TANU.

Ikiwa kweli unataka kujua jiepushe na lugha za kejeli mfano wa hii
''kumfundisha Kiswahili.''

Mimi naona tabu sana mambo kama haya.
 
Nyie badala ya kumtafuta mwandishi na kugombananae mlitakiwa muandike kitabu kusahihisha, "uongo," wangu si kuandika kejeli na kuleta chuki na hasad.
Ukisoma makala gazetini ambayo haikupendezi jibu lake si kuanzisha gazeti kujibu makala hiyo
Ukisoma kitabu ukapingana na maudhui yake jibu lake si kuandika kitabu

Hili ni jibu jespesi na la haraka lisilojibu hoja na lisilo na mantiki the least to say.
Angejibu hivi mwanafunzi wa Makongo sec nisingemjibu
 
Kamsome Mag3 na kumbu kumbu alivyovuta 2011. Hakuna jipya unaloeleza isipokuwa majigambo. Nani ana interest na wewe kula na wazungu? Nani ana interest ya nukuu moja kwa maandishi mekundu yasiyo na maana!
Kuna nyakati tofauti inakuwa muhimu baina yetu

Ukitualika tutakuja, ni uungwana. Tuanze na hapa chini halafu tutareja katika viporo

Wanajamvi, kama mnamsoma vizuri Mohamed, anasema mwasisi wa TANU ni Abdul. Anasema hayo baada ya kushindwa kueleza nani aliandika katiba ya TANU

Hili la Uasisi kutoka kwa Abdul hana uhakika nalo! amesikia.
Muulizeni aweke ushahidi hapa jamvini. Narudia hana ushahidi amesikia na huo si ushahidi wala fact

Halafu harakati zote zinaishia kuundwa kwa TANU. Muulizeni nani aliunda AMNUT na kwanini haikupata mafanikio

Kuna sababu kwanini historia inaanzia 1929 hadi 1953! Heiendelei. Muulizeni kwanini
Mohamed hoja zipo hapa . Utazunguka zunguka lakini hoja ni hizi na wanajamvi wanaelewa
 
Back
Top Bottom